Hivi hii imekaaje, ni kwangu tu au kwa wote?

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
3,466
8,281
Habari zenu.

Ni kwamba nimekua na kawaida ya kuamka saa sita usiku na kukaa macho hadi saa kumi hadi saa kumi na moja alfajiri ndio usingizi huja tena hadi saa moja kasoro.

Imekuwa hata nikilala saa tano lazima iwe hivyo. Na nikiamka nikisema labda huo muda nitanye Mambo mengine siwezi kabisa zaidi ya kugalagala kitandani. Hata nikiamka kuangalia tv nashindwa na usingizi unaweza nipitia ila nikirudi kitandani usingizi unakimbia wote

Na pindi nitakapo kuwa macho basi akili inaanza kuchakata matatizo yalio nishinda kwa mfano kuna kipindi nilikua nafanya maswala ya programming kwa wataalam wa computer watanielewa...! Utakuta program labda imegoma ku compile mchana kutwa nashinda natafuta solution naishia kugaili ila usiku utashangaa nimestuka Kama kawaida na akili inaanzia palepale kwenye statement inayonisumbua au function na inakumbuka mistari yote hadi Kama nilisahau ku terminate statement vyote vinakuja na nikiamka nakuta kweli Kuna mstari sikufanya sawa nabadirisha mambo yana tiki.

Sawa ni kitu kizuri ila Mimi sitaki napenda muda wa kulala nilale na muda wa kazi nifanye kazi.

Alafu kubwa kuliko huo muda ninakua na roho ngumu na maamuzi magumu yaani kiasi kwamba ukanizingua Kama nina kitu Cha hatari nakuzuru nacho bila kujiuliza Mara mbili.

Na Mimi ni mtu wa utani Sana ila huo muda sipendi kabisa ujinga wowote (au sijui ndio maana watu wanasema akili za usiku). Yaani hata ikitokea Kuna tatizo la kijamii au kifamilia linataka maamuzi laini ila huo muda solution ninazo zionaga ni za kikatili. Nilisha wahi fikiria kumzingua baba yangu mzazi kwa mambo ya kijinga tu ila nilivyo amka asubuhi mawazo yakaja mengine na kuanza kujishangaa kwa nini usiku nilifikiria vile na ingetokea ninge onana na mzee usiku ule aisee ningemzingua ukweli sio

Jaman naivhukia hii hali Kama Kuna idea jinsi ya kurudi kawaida naombeni
 
Na mimi ni hivyo hivyo sema nahisi kwasababu nasoma sana vitabu usiku ndo maana. Ila unaweza kujitune ukalala kama kawaida.
 
Akili yako umesha iseti kuamka muda huo na kufanya mambo hayo uyafanyayo,

Unatakiwa ucheze na akili yako wewe mwenyewe ili ibadilike,

Jaribu pia kufanya mazoezi hasa muda wa jioni,kula ushibe kabla ya kulala.
 
Back
Top Bottom