Biashara ya waste engine oil (oil chafu)

Nyingine Inapelekwa kiwandani wanatengeneza oil mpya, Inafanyika hivyo kupunguza uchafu wa mazingira. Ila huwa wanaoyesha kama hiyo oil ni recycled.
 
Nijuavyo mimi ni kwamba oil chafu hutumika kwa kazi hizi
1. Kupakwa kwenye mbao hasa za kupigia paa kuzuia mchwa na wadudu wala mbao na hii ndio kazi kubwa
2.hutumika kumwagia kwenye vyoo vyenye harufu chafu hasa vya shimo ili kupunguza harufu
3. Kina mama hupenda kutumia kusafishia nyumba kwani baada ya kusafisha nyumba hungaa sana hasa nyumba zenye flour ya cement chini na sio marumaru
4. hutumika kwenye nguzo/ mistimu humwagiwa chini pale ili kuzuia mchwa
5. Hutumiwa kuwekwa kwenye miti ya mtunda au miti ya fance kuzuia miti hiyo kuliwa na mchwa na kusababisha miti hiyo kukauka

Hivyo baada ya kuonekana kuwa oil chafu imepata matimizi muhimu hasa hilo la mbao za ujenzi ndipo ilipo anza kuuzwa na kuwa dili lakin zamani ilikuwa ina mwagwa tu bila kujali
Samahani, mtunda ni nini?
 
Pia unaweza kuitumia kwa kumwaga kuzunguka nyumba ili kuzuia wadudu hasa Nyoka
 
Habari zenu wanajukwaa.
Mimi ni kijana ambae nipo mkoani mtwara nawajibika ili mkono uingie kinywani. Leo nimekuja kwenye jukwaa hili ili nipate ushauri juu ya Mada kuhusu biashara ya mafuta ya injini machafu/yaliyotumika ( waste/used engine oil).
Kikubwa ninachotaka kufahamu ni soko lake linaweza kupatikana (ndani ya mkoa wa Mtwara au nje ya Mtwara) wapi na inanunuliwa kwa bei gani kwa kila lita moja.
Nimevutiwa kujua undani wa biashara hii baada ya kuona oda nyingi ya mapipa ya hii bidhaa kutoka ndani na nje ya mtwara, hivyo basi nimeona nije na mada hii ili nipate mawazo yenu niweze kuchangamkia fursa.
Nawasirisha hoja karibuni kwa mchango wenu.

E. S. NGALAMA
MTWARA

Asante
 
Habari zenu wanajukwaa.
Mimi ni kijana ambae nipo kiwanda cha dangote cement nawajibika ili mkono uingie kinywani. Leo nimekuja kwenye jukwaa hili ili nipate ushauri juu ya Mada kuhusu biashara ya mafuta ya injini machafu/yaliyotumika ( waste/used engine oil).
Kikubwa ninachotaka kufahamu ni soko lake linaweza kupatikana (ndani ya mkoa wa Mtwara au nje ya Mtwara) wapi na inanunuliwa kwa bei gani kwa kila lita moja.
Nimevutiwa kujua undani wa biashara hii baada ya kuona oda nyingi ya mapipa ya hii bidhaa kutoka ndani na nje ya mtwara, hivyo basi nimeona nije na mada hii ili nipate mawazo yenu niweze kuchangamkia fursa.
Nawasirisha hoja karibuni kwa mchango wenu.

E. S. NGALAMA
DANGOTE CEMENT TANZANIA MTWARA

ASANTENI
Ulivyo weka iyo anuani ya hapo mwisho utadhani kiwanda ni chako
 
Sasa kana unaona oda nyingi kutoka hapo mtwara si uwaulize hao hao kwamba nyie binadamu hii oil mnayotoa oda mnapeleka wapi...
Watakueleza A-Z tuache uoga vijana sio kila kitu ni kuuliza kwenye mitandao wakati wahusika unao hapo hapo ulipo..
 
asante kwa ushauri wako mkuu
 
Navyojua ukitaka kirahisi oil Chafu nenda Dsm Oil chafu kwa wingi inapatikana za motor engine.... Garage zote huwa wanazikusanya kwa ajili ya kuuza.

Nilipokuwa mdogo sikuelewa wale wakusanyaji wakizunguka kukusanya ni wapi walikuwa wakizipeleka kuna siku nikaona mbao za kenchi zikipakwa nikajua ndio matumizi yake makuu na matumizi ya pili ni kumwaga kwenye vyoo vya shimo ili harufu isienee na tatu ni kuimwaga barabarani haswa zile zenye vumbi jingi basi barabara inakuwa shwari.

Kumbe oil chafu inakazi moja matata sana... haswa viwanda vya kuyeyushia vyuma n.k huwa inachanganywa na kerosene nadhani au hivi hivi na huwaka sana kwa kutoa joto kali sana kwenye taruru na hutumia muda mrefu kuisha... Unavyoona vitu kama Masufuria,Makarai Pasi za Mkaa n.k jamii hiho basi moto wa kuyeyushia hivyo vyuma au mabati Oil chafu hutumika sana kuchochea moto mzito.

Nadani kuna watu oil chafu ndio deal zao hukusanya karibu garage zote kama ilivyo malighafi yeyote inayotumika haikosi matumizi
 
asante mkuu nimekuelewa vizuri, mm nilikua nahitaji kujua soko lake likoje cz kuna mapipa kadhaa hapa ya hiyo malighafi. nashindwa kutoa maamuzi cz ipo naweza ipata kiurahisi shida inakuja kwenye wapi nitaipeleka kwaajili ya kuuza
 
sasa mkuu kwanini usiulize hapo hapo unapoona kuna mapipa mengi wao watakwambia wanatoa wapi na wanaifanyia nini!!
 
Back
Top Bottom