Biashara ya vipuri vya pikipiki: Ushauri, michango, mawazo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya vipuri vya pikipiki: Ushauri, michango, mawazo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by marandu2010, Aug 23, 2010.

 1. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Boda-Boda-Riders-In-Juba2.jpg

  Wakuu kwa mara nyingine tena:

  Pikipiki zimeenea sana sasa hasa katika jiji letu la Dar es salaam.Hii inanifanya nione biashara ya spea za pikipiki itakuwa inalipa sana?

  Sijajua upande mwingine wa shillingi. Hebu nipate mawazo yenu wakubwa.

  Mna maoni gani katika hili?

  Asanteni sana wakuu.

  ===
  2.
  => Maoni na Ushauri


   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Muzee una mawazo mengi sana ya biashara! vp uko konfyuzd? nina wasiwasi hautafanikisha! (kidding!).

  Kwani wewe una ujuzi gani, kama ni mstaafu, ulikkuwa unafanya kazi gani?

  Jaribu kuangalia biashara ambayo unaaidia nayo kidogo (Kama haujui hata plagi itakuwa ngumu kufanya biashara ya spea za auto-japo inawezekana).

  Kama ulikuwa mwalimu ni heri ufungue twisheni senta, au duka la vitabu!
  Vinginevyo karibu shambani!
   
 3. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Hello amoeba,,hilo ndio tatizo tulilo nalo sisi binadamu,,ni wepesi wa kuhukumu wengine,,na wenye macho yaliyopewa uwezo kuona ubaya wa wengine na si uzuri wao,,kuna shinda gani ikiwa mimi nitakuwa nina business ideas nyingi?

  Je, mtu mtu anayetaka informations kuhusu biashara mbalimbali ambazo ni halali yuko confused?

  Siku zote ni vyema kufikiri kabla ya kutenda,,lakini hii haimaanishi tuzungumze bila kufikiri,,kuzungumza pia ni mojawapo ya matendo kwa hiyo tufikirie pia kabla hatuja zungumza.

  By the way nakushukuru kwa vipengele vichache vyenye tija katika meseji,but accept to change in the others.

  Asante sana.
   
 4. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mimi kwa upande wangu nafurahi kuona idea mbalimbali za biashara kwani hiyo inasaidia hata wengine na
  kupata changamoto katika kuanzisha biashara.
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Dont quote me wrong mkuu!,
  soma tena msj yangu, kwenye mabano nimeweka "natania", hata hivyo nisamehe if you cant take a joke!
  1Love!
   
 6. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Tunahitaji mawazo mbalimbali kuhusu biashara najua humu kuna wataalamu wa kila aina na wenye uzoefu
  wa muda mrefu kwenye biashara
   
 7. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  i love you too amoeba
   
 8. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hii biashara itazidi kukua everyday, naamini pikipiki bongo zitakuwa kama India au china maana watu wengi ndo wataweza kuafford.
   
 9. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Exactly,,unajua nilikuwa nafikiri akili hiyo ninayo mimi tu,,kumbe hata mwenzangu unaliona hilo,asante sana tuendelea kuweka wazi mambo watu tufanye biashara vizuri zaidi,,nadhani hilo ndio lengo la kuwa hapa katika forum hii ya biashara,itusaidie kimawazo wote kwa pamoja..

  asante sana mkuu enny.
   
 10. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  asante sana kang kwa kuweka wazi hili,,tuko pamoja mkuu..
   
 11. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,360
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Pikipiki,na spea zake zina soko,ila lazima ununue spea feki za china,siyo feki ila ni spea zisizo madhubuti,inalipa sana kwa mtazamo wangu,hasa ktk miji midogo ,siyo dar,in dar itakulzzimu uuze bei ya jumla.
   
 12. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  asante sana mzalendo
   
 13. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  100% nakuunga mkono kabisa ulichoandika....ukitaka kuendelea ku-survive kwenye soko lazima uweke bidhaa feki za kichina, na sababu ni:
  1. Watanzania walio wengi ni wako sensitive kwenye price....ukiweka kifaa genuine automatically bei yake lazima iwe juu ...sasa basi waliowengi wana opt kununua za bei ya chini...ambazo ni brand za kichina ( Nimejifunza haya kutokana na biashara ninayoifanya ya vifaa vya ujenzi)
  2. Pikipiki zilizo nyingi nchini ni za kichina ( affordable kwa kila mtu) - hivo tumia simple formula Pikipiki za kichina= spea za kichina......hapa unakuwa uwewapa wateja kitu wanachokipata
  3. Suppliers wa spea za Pikipiki hasa za kichina ni wengi........ila kaka inatakiwa uwe makini sana kwenye manunuzi ......hiki ndo kitu nilichojifunza. Unaweza ukakwea pipa mwenyewe ukaingia China au Ukanunua kwa whole salers walioko kariakooo. Si kila muuza spea kariakoo anasafiri...wengine ni misheni town tu af maduka yao wame-display kama wholesalers
   
 14. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,360
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Payuka ,umeshafanikiwa kufika china kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa za biashara yako,if yes,labda utupe dira jinsi ya kwnenda na kupata suppliers wa ukweli ili marandu2010 afungue duka lake la spea za pikipiki,
  marandu mimi ntakufungulia e-shop ya spea za pikipiki ili wenye viduka mikoani waweze kuorder online.
  it will be a win-win situation,unanunua bidhaa ,mimi nakupa infrastrakcha ya kuweza kuuza online
   
 15. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Natumaini hamjambo wanajamii wa JF especially jukwaa hili,

  Mimi ni kijana niliyeajiriwa sekta ya umma..nimeamu nijitose kwenye ujasiriamali...hasakwenye sekta ya usafirishaji hususani spea za pikipiki kama nilivyoainisha.

  Kwa kuanzia nimefanya uchunguzi wa kutosha sehemu ninyaoishi ina pikipiki nyingi ila spea ndio hamna...sehemuitapatikana ila nahitaji kama kuna yeyote anaefahamu zaidi jins ya kuplan business hii anaipe some inputs.

  Kama starting capital,vifaa vizur vya kuanzia kununua,bei na mengineyo.

  Ninachukua mkope hivi karibuni nimeonelea bora nitimize iyo ndoto ya ujasiriamali maana uthubutu tayari ninao.

  Pia niatanunua pikipiki kama 2.

  Nimetenga nusu ya mkopo wangu wa 8mil ndio nianzie busness is it enough?

  Asanteni.
   
 16. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #16
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  mkuu hongera sana kwa hili na mungu akusaidie. But huja sema uko wapi. Eneway ushauri wangu.

  Kama utakuwa umepata eneo la kuuzia hizo spea fanya yafuatayo.

  1. Nenda kule kariakoo, pale utakutana na waagizaji nje wa spea za piki piki wale wamespecialize kama ni toyo utakuta waagizaji wa toyo, kama ni sunlg utakuta waagizaji wa vifaa vya sunlg na kazalika kila aina ya pikipiki ina waagizaji wake wakuu wa spea nje na hawa sanasana ni wahindi

  2. Ongea nao na chukua bei za kila spea za pikipiki zinazo patikana mtaani kwenu

  3. Waambie unataka kufungua duka la kuuza spea na kama hutaweza kuspecialize unaweza chukua spea za kila aina ya pikipiki

  4. Patana nao, hawa jamaa wanaweza kuwa wanakuletea yaani unawatumia hela benk then unawatumia sumary ya spea unazo taka wao watazichua na watazifunga kwenye box then watakutumia either kwa njia ya basi mpaka mahali unafanyia biashara means mji, haina haja ya kufuata mwenyewe bongo.

  Yangu ni hayo tu
   
 17. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  KomandoO,

  Asante sana ndugu yangu mi nipo dsm il anataka nifungue biashara hiyo maeneo ya ubungo...i hope ulishawahi kuifanya nawe pia..nitajitahidi mkuu unajua ten amaisha nayo yamebana inabidi kujipanga kweli kweli
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #18
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  KomandoO,

  Mkonowapaka, watamkwamisha au kumgonga bei. Kwa achunguze ni pikipiki za aina gani ndiyo nyingi kwenye soko. Angie kwenye website ya hawa wazalishaji na awombe uwakala wa kuuza spea watampa!

  Pia awe anatengeza pia vijana wapo amuajiri moja au wawili. Asimamie mwenyewe! Akimwachia mtu amekwisha!

  Nawasilisha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. n

  naft Member

  #19
  Sep 16, 2013
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huu mjadala uliisha vipi jamani??
   
 20. gkileo

  gkileo JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2013
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 977
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 60
  ImageUploadedByJamiiForums1387767815.738142.jpg ImageUploadedByJamiiForums1387767840.424193.jpg ImageUploadedByJamiiForums1387767873.808937.jpg
  Wadau hongereni kwa kazi.
  napenda kutambulisha duka langu la spare parts za pikpiki lililoko kariakoo mtaa wa Sikukuu/Amani. tuna vifaa vingi vizuri sana kwa bei nzuri.
  tafaadhali wasiliana nami kwa no. 0658131333, email ni gkileo@gmail.com. pia no. yangu imesajiliwa kwa whatsapp ,we chat nk.
  ndugu mdau utakaesoma hapa yawezekana ukawa huna duka wala pikipiki ,lakini mtaani kwako lipo. tafadhali mfahamishe kuhusu duka letu na mpe namba yangu pia waweza kunitumia namba ya simu ya mmiliki wa duka
   
Loading...