Biashara ya Uwakala na upotevu wa pesa

Malyakishu

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
1,968
2,339
Habari Wanajamvi

Naomba mnisaidie jambo moja kwa watu wenye uelewa na hili swala la mambo ya wakala wa huduma za kifedha katika mitandao ya simu na huduma za Kibank.Mimi nafanya huduma hizi jambo linalonisumbua wanajamvi ni upotevu wa pesa .kwamfano nina mtaji wa M20 nazungushia pesa hizo katika wakala huduma za kibenk na mitandao ya simu.

Kutoa na kuweka pesa sasa kila ninapofunga hesabu lazima nikute pesa pungufu Mara elf 20, 18, 30, 40, juzi nimepata loss ya laki 3. Wanajamvi nashindwa kuelewa shida inakua ni nini najitahidi kuwa makini kwa kila muamala lakini.

Bado hali ni hiyo hiyo naomba mnisadie hata mbinu au mawazo maana sijui tatizo linakua wap kwa wenye uelewa nipeni mbinu yakutokupata hasara za mara kwa mara.
 
Si mnapata statement ..weka utaratibu wa kuandika unachopata na kutoa

Mfanoo...andika (DR) zote ulizotoa..ulizolipa cash

Kisha (CR) kwa ulizo ingiza (pokea)

Uwe na daftali

Baadaye piga hesabu ya toatl kwa kila muamala utajua kosa lipo wapi...badaye unavuta statement ya siku utaona makosa yako na kama umelipa vibaya utaona
 
Kwa miamala ya kibank wateja huwa nawajazia fomu za bank husika nabaki na copy na miamala ya simu huwa siandikishi ....nakua makini kwa kila hatua ya kufanya muamala napesa cash mtu anapotoa lakini nikipiga hesabu jioni hasara inakuwa ipo
 
Itakuwa wazee wa "Ndele" wanapita na mashuka ya Mmasai! Muda wa kufanya kazi na wazee wa Bagamoyo umewadia. Biashara ni ngumu sana kibongobongo maana kanuni za vitabuni pekee hazitoshi. Lazma uende nje ya box kistaili. Wanasema vipande vya mkaa kwenye droo ya pesa husaidia.
 
Pole sana,waulize ma teller wa kwenye mabenki wanavyokula shot na kuishi kwa madeni kisa ni nini!Ombea hiyo sehemu yako kila unapofungua,omba kwa kumaanisha ili uvunje nguvu za giza vinginevyo utaendelea kulia kila siku na kuona biashara hailipi...
 
Case closed!

Ongezea ndimu au limao kwenye droo au chombo uwekacho pesa.

Mimi siyo mshirikina ila inenaisaidia baada ya kupoteza elfu 10 kimaajabu
 
Itakuwa wazee wa "Ndele" wanapita na mashuka ya Mmasai! Muda wa kufanya kazi na wazee wa Bagamoyo umewadia. Biashara ni ngumu sana kibongobongo maana kanuni za vitabuni pekee hazitoshi. Lazma uende nje ya box kistaili. Wanasema vipande vya mkaa kwenye droo ya pesa husaidia.
Asante. Nitajaribu kuweka mkaa
 
Pole sana,waulize ma teller wa kwenye mabenki wanavyokula shot na kuishi kwa madeni kisa ni nini!Ombea hiyo sehemu yako kila unapofungua,omba kwa kumaanisha ili uvunje nguvu za giza vinginevyo utaendelea kulia kila siku na kuona biashara hailipi...
Shukrani ..nitafanya hivyo
 
Back
Top Bottom