Biashara ya sehemu za makaburi binafsi Tanzania inaweza kuwa fursa ya kibiashara

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,681
46,371
Katika nchi zilizoendelea na nyingi za Latin America na Asia au hata jirani zetu Kenya kuna biashara kubwa ya sehemu za makaburi inayofanywa na makampuni binafsi. Unakodishiwa kaburi unakuwa unalipia kwa kipindi fulani kama mpangaji au unalinunua moja kwa moja kabisa.

Hapa nchini makaburi mengi ya Jumuiya kama sio yote bado yanaendeshwa na serikali, kanisa, misikiti, mahekalu au familia. Sekta bado haijafunguka vya kutosha, inabidi michakato ifanyike ifunguliwa watu wenye ardhi kubwa wapige pesa.
 
ardhi tumetumia asilia 15 nchi nzima bado sehemu za kuzika na kujenga zipo
Hata Marekani sehemu za kuzika na kujenga zipo, kuna vitu vingine vingi vya kutazama zaidi ya ukubwa wa ardhi iliyo wazi.
Halafu kama ardhi tunayo kubwa hivyo kwa nini kila mahali nchi nzima kuna uvamizi, uporaji na migogoro ya ardhi isiyoisha??
 
kama nchi ambayo maendeleo yana sua sua tu ilo litashindikana
 
Hata Marekani sehemu za kuzika na kujenga zipo, kuna vitu vingine vingi vya kutazama zaidi ya ukubwa wa ardhi iliyo wazi.
Halafu kama ardhi tunayo kubwa hivyo kwa nini kila mahali nchi nzima kuna uvamizi, uporaji na migogoro ya ardhi isiyoisha??
kuna watu wana uelewa mdogo au wengine wanang'ang'ania maeneo fulani
nchi ni kubwa sana
 
Kuna siku nilipiga mahesabu rough nikaona kuwa ikiwa kila mtu ataamua kuzikwa, katika miaka 100, makaburi ya dunia ya watu watakaozikwa katika miaka hiyo yatachukua sehemu kubwa kama nchi nzima ya Gambia.
Baada ya miaka 50 nafikiri, sera si huwa ipo ya sehemu ya makaburi kuwa sehemu ya wazi au ni story?
 
Anzisha tutafuata
Tuweke kwanza sheria na mifumo vizuri isiwe rahisi watu kuiba, kupora, kunyang'anywa au kuuziwa ardhi za hata mara nyingi kitapeli na maofisa ardhi na watawala. Lazima mfumo wa usimamizi ardhi uaminike kama tunataka kuvutia zaidi uwekezaji mzuri katika ardhi.
 
Back
Top Bottom