Biashara ya internet

dar sasa karibuni kwenye mkongo wa taifa kasi ni kubwa mno
 
Jamani ninataku kuanzisha biashara ya internet cafe maeneo ya chuo kimoja hapa jijini, naomba munisaidie nitumie inetrnet service provider wapi wazuri ambayo watanipa speed nzuri kwa ajiri ya wateja wangu kwa gharama inayofanana na huduma wanayonipatia. Nimepita kwenye sasatel, vodacom, zantel huko kote pasua kichwa. Tyari nimeishalipia pango la mwaka mmoja lkn nimeshindwa endelea maana service providers waote niliowaorodhesha hapo pasua kichwa. Wanaofanya hii business naomba msaada wenu
 
Jaribu Selcom, sina uhakika ofisi zao wako wapi lakini ninafahamu internet cafe ambayo wanatumia huduma zao na wanasema ni nzuri na bei sio mbaya.
 

Mkuu wenye c@fe wengi wanatumia TTCL kwa hiyo na wewe kimbilia huko huko
 
Wakuu poleni sana na kazi:

Naomba dhahabu,,msishangae namaanisha mawazo yenu,,kama mlikuwa hamfahamu hayo ni zaidi ya dhahabu lakini inategemea kama unalitambua hilo..kikubwa ni kwamba nahitaji kuanzisha biashara ya internet cafe hivi karibuni,,,ila changamoto kubwa ni location ya mahali pa kuiweka hii biashara katika jiji la dar es salaam..

Naomba mchango wenu wa mawazo(zaidi ya dhahabu) kuhusu hili..

Natanguliza shukurani zangu wakuu..asanteni sana
 
Tafuta location karibu na Shule za secondary, vyuo pia hata kwenye mkusanyiko wa watu wengi.
 
Biashara ya internet sio lazima hapa Dar ,nilikuwa Morogoro Ifakara kuna Internet Cafe moja tu na kuna wateja kibao
 
Biashara ya internet sio lazima hapa Dar ,nilikuwa Morogoro Ifakara kuna Internet Cafe moja tu na kuna wateja kibao
asante sana mkuu kwa wazo zuri hili,,bila shaka yeyote nitalifanyia kazi.
 
habarini za kazi wanajavi!
Ninaomba kufahamishwa kwa wale wenye uzoefu wa biashara ya internet cafe kama inalipa na inaitaji mtaji wa kiasi gani kwa kuanzia

na je stationary inalipa na inaitaji mtaji wa kiasi gani kwa kuanzia na iwe maoneo gani kwa dar es salaam?
Ntashukuru kwa msaada wenu wa ufafanuzi
 
Sasa hapo unatakiwa uwe umeshaandaa mchanganuo wa kibiashara(Business plan), kujua eneo la kufanyia hiyo biashara, ukubwa wa chumba au fremu uliyopata, computer ngapi unaweza kuingiza, na sehemu ya stationary vivo hivo...
the ndo wadau tuchangiie uhalisia wa biashara, lakn kimsingi huwa hiyo biashara inalipa
 
Inalipa ukipata eneo ambalo computer inatumika muda mrefu....labda si chini masaa 8 hivi kwa siku yaani tangu saa 2 asubuhi na saa 4 usiku,ukiwa na pc kama 5 hivi ina maana 500*5*8 unapata 20,000 kila siku,kwa mwezi unapata 600,000/ hy upande wa internet tu,bado stationary nako kuwa na flow nzuri photocopy etc.
Hapo utalipa kodi labda 200,000 na wahudumu....
Mtaji labda 5m plus
 
 
hello wajasiliamali wenzangu

nimetoka kulipia frem jana ili soon nianze mradi wa internet cafe.......nataka niachukue internet ya TTCL na kwa kuanzia nianze na computer kama 4 ivi...nitaweka pia printer;huduma ya passport size na mpesa tigo pesa....

naombeni uzoefu wa jinsi ya kumanage biashara hii kwa wale ambao mmeshaifanya au mnaifanya...changamoto na mambo mengine kama hayo
 
ukitaka fanya biashara vizuri hakikisha una walau knowledge flani ya mambo ya comp. Hakikisha internet speed iko fast walau 250kb/sec.
Mimi hapa nauza pia software, cd za windows na mtu akitaka update antivirus pia analipia ela tofauti ambayo ni 3000.
mimi nina computer 6 kwa siku sikosi elfu 30000 sometime hadi napata 90 au hata laki kwa kuwa mimi nauza pia movie mpya ninazo download toka internet na softwares pia na kila movie mpya mtu akitaka namuuzia 5000 moja kwa 3000 kama anachukua zaidi ya 5.
Ubunifu wako kaka
 

umeniimpress mkuu..ofkoz nina knowledge na mambo hayo maana niliyasomea pia.nimependa suala zima la ubunifu lilivyotumika hapa,,,,,,,,,,kwamba naweza lets say jumamos 1 nikaweka bango 'surf 3hours get one free'... au labda naweka tangazo la movie mpya ilivozinduliwa jan ayakwe kwenye theatre marekani 'get it now on ur screen'..na mambo mengine kama hayo...safi sana mkuu!!watu tunaweza tukiweka longolongo kando na kuwa comitted...hongera sana kutengeneza laki kwa siku.
 

Hapo sasa kama utakuwa na ubunifu na hiyo elimu yako na kama location ni nzuri utawadaka sana na hakikisha comp zako safi zisiwe zna stuck stuck
 
 
biashara ya internet cafe,mi nilianza na internet cafe kisha nikafungua biashara nyingine nyingi,pamoja na hayo internet cafe siwez acha inalipa sana siku hizi kila mtu yuko facebook,na watu wanaemail,weka na mashine ya kuscan na kuprint,pamoja mkuu
 
Hivi Internet ya TTCL ndio gharama zake ni nafuu?
Na vipi sehemu ambayo nyaya za TTCL hazijapita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…