Biashara ya gesi ukaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya gesi ukaa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ndele, Sep 4, 2011.

 1. N

  Ndele Member

  #1
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ndugu wanajamvi! ninaomba msaada wa kitaalamu ikiwezekana kupata mawasiliano ya wataalamu wa kudhaminisha kiasi cha hewa inayozalishwa kutokana na miti ya kupanda na pia kuniunganisha na watu ambao wananunua hiyo gesi ukaa, ili waweze kununua kutokana na kiasi fulani cha mazingira ninayotunza! kwani mzee wangu ana ekari zaidi ya mia nne za miti ya kupandwa zenye hati. lakini haijafikia hautua na kuvunwa.
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Angalia hii article ya kwenye business times nina uhakika inaweza ikausaidia kuona ni nini cha kufanya na wapi pa kwenda (kuna simu hapo chini ya jamaa alieandika hii article nadhani ni vema ukimtafuta)
  Source: Carbon trading: why Tanzanians fail to take full advantage of CDM

   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama hati yenu haina noma,jitahidi sana mpaka uvuke vikwazo. Mimi nimeshindwa kwa sababu mashamba yangu hayana hati, na ili nipate hati inabidi niwe na mpunga mwingi, na nikipata mpunga huo naona bora kuongeza shamba zaidi, kwa hiyo imekuwa mtindo, nikipata hela sitafuti hati naongeza shamba na kuliendeleza !!!!!.

  Mtafute Edson, yuko humu ndani anaweza akakupa abc kidogo. Niliwahi kufika kwao na nikaongea na mtu mmoja muhimu, akasema kama una hati ya shamba anaweza kunisaidia. Vikwazo ni vingi ila pambana. Ukifanikiwa mpunga wake ni mwingi mkuu. Kule wilayani kwetu tuliwahi kuandikisha majina ya watu wenye misitu. Mpaka leo kimyaa, sijui ilikuwa kampeni au ndio longo longo za kila siku.
   
 4. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  hilo shamba liko maene gani? tukifahamu lilipo tunaweza kusaidia kukuunganisha na watu wanohusika. otherwise waweza kwenda ubalozi wa norway, ndio wanahusika na miradi mingi ya kununua hewa ukaa. ukifika pale waweza kupata taarifa zaidi.
   
 5. N

  Ndele Member

  #5
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  shamba lenyewe lipo mbeya maeneo ya igoma kama unaelekea kitulo-makete
   
 6. N

  Ndele Member

  #6
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kaka nimeisoma hiyo artcle duhh mbona gharama kubla sana? pia nimewasiliana na alieandika anasema yupo nje ya nchi kurudi mpaka oktoba lakini kaniambia niende wizara ya mazingira watanipatia taarifa zaidi. hivi siwezi pata wafadhili wa kufanya utafiti huo?
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Wakati unamsubiri huyo jamaa, piga kwata mpaka ubalozi wa Norway au ingia hizo ofisi za mazingira pale Wizarani.
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Je miti hiyo ina umri gani? na ni aina gani?
   
 9. M

  MANAKE MKARI Senior Member

  #9
  Sep 4, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wazo lako ni zuri sana mkuu. Hewa ya ukaa ni biashara ambayo inasumbua kidogo lakini mambo yanawezekana ukiwa serious and ujicomit vizuri. Nchi nyingi za Africa hazifaidika kabisa na hii biashara kutokana na ukweli kwamba wengi wetu hatupendi kujihangaisha na vitu vinavyoumiza kichwa kidogo.
  Kuna vitu unatakiwa uvijue mwanzoni ili hata ukimwambia mtu akuelewe vizuri:
  • Kilichofanyika kwenye hilo shamba ni aforestation/reforestation au unataka kufanya sustainable forest management ambayo itachangia kuconserve/enhace carbon stock.
  • Unataka msaada wa ku develop huo mradi au unatafuta mtu wa kununua credits(hewa ya ukaa)
  • Aina ya miti na umri.
  • Unategemea kuvuna hiyo miti lini.
  • Jamii itafaidikaje na huo mradi.
  Ni kweli Norway wanafungu linalohusiana na mambo ya hewa ya ukaa kwenye misitu lakini wanaohusika na technical issues ni UDSM-IRA, Tanzania Forest Conservation Group (TFCG), Mpingo Conservation na Ofisi ya makamu wa rais-idara ya mazingira. Hawa walipewa hela na Norway ili kuone ni jinsi gani hii biashara inaweza kufanyika ingawa preference ni kwenye misitu ambayo itakuwa na faida kwa community.
  Mradi wako unaweza kuudevelop chini ya compliance Clean development Mechanism (CDM) au chini ya Voluntary carbon markets. Compliance ni kwa ajili ya aforestation and reforestation projects only wakati voluntary ni kwa zote. Bei ya compliance credits ni kubwa kuliko voluntary ingawa inakuwa na long and complex preocedures. Ni vizuri ukaangalia voluntary market kwa sababu haina mlolongo na kuna standard mbali mbali na vile vile Tanzania haina "definition" ya forest itakayokuwezesha kuchagua compliance.
  Ushauri:
  • Jaribu kuwasiliana na hao watu hapo juu.
  • Pia Green Resources (Iringa) wana miradi kama huu so unaweza kuwasiliana nao wakakupa ushauri.
  • Ukikwama ni pm tuone tutakachoweza kufanya.
   
 10. N

  Ndele Member

  #10
  Sep 4, 2011
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mkuu kilichofanyika kwenye shamba hilo ni kwamba maeneo mengine tulifanya reforestation na maeneo mengine tumefanya aforestation kikubwa hapa nahitaji msaada wa kitaalamu na kifedha kudevelop mradi huu kwani kuna makala moja nimesoma inaonyesha inahitaji fedha nyingi sana na mimi sina mtaji huo labda niuze baadhi ya miti! kitu ambacho sio kizuri. pia aina ya miti kwa kiasi kikubwa ni mi-pines na inaumri kati ya miaka mitano na kumi na mbili. hivyo kuvuna kutafanyika baada ya miaka sita hadi kumi na tatu. je uaweza kuwa na mawasiliano na hao jamaa?
   
 11. M

  MANAKE MKARI Senior Member

  #11
  Sep 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sawa. Kuhusu gharama usijali sana. Kuna aina mbili za kudevelop mradi.Moja ni wewe kuingia hizo gharama (transaction costs) na kuuza credits baadaye au kutafuta mnunuzi wa hizo credits (forward selling) kwa sasa ambaye atacover hizo gharama kwa makubaliano ya kulipana baadaye. Option ya pili ni nzuri kwa mtu ambaye hana fedha pamoja na uzoefu. Unaweza kuandika 1 or 2 pages kuhusu hilo shamba? Hii itasaidia wakati unapowasiliana na mtu ili aweze kuelewa kwa urahisi. Hakikisha unaonyesha ni kwa jinsi gani jamii inayokuzunguka itafaidika na huo mradi maana hii ndiyo interest ya wengi!!!!Ukisha andika tuwasiliane kwa hatua ya pili. Hii kitu inawezekana maana hata watani wetu wanafanya mambo sisi wala hatuhangaiki. Nina uzoefu wa kutosha kwenye hii kitu na huwa nafurahi sana ninapoona mtu akijaribu.
   
 12. N

  Ndele Member

  #12
  Sep 5, 2011
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ok mkuu nashukuru sana basi nipe mda kama wiki moja hivi ili niweze kukupa taarifa kamili kuhusu shamba hilo
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2014
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  wiarani watam frustrate tu..watu wako busy kula vitumbua na uji wa ulezi
   
 14. u

  utinotino Senior Member

  #14
  Sep 29, 2014
  Joined: Jan 23, 2014
  Messages: 120
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Since 2011!! Wakuu mmefikia wapi kwa hili?
   
Loading...