Kaulize wenye daladala ndo wenye uzoefu.
Yupo kwenye ukumbi sahihi, so kama umekosa jibu la swali alilouliza hapa ni vyema kukaa kimya na si urojo unaoandika hapa!!! Wengi tunaelimika kupitia humu na si kumbi za walevi kama unavyofikiria!!
Mwenyewe nina caravan hapa Iringa na nimepata mawazo mazuri sana hapa ikiwamo kuipeleka Arusha aisee Iringa route zake fupi fupi sana na abiria bado ni tatizo!!
Kamundu mkuu, Ahsante sanaMarkach: Ushauri wa bure usifanya biashara ya daladala!!. Mimi nilibahatika kufanya hii biashara miaka ya 1996-1997 na kuna matatizo mawili makubwa (a) Huwezi kupanga bei na bei inapanda polepole kuliko mfumuko wa bei. serikali inapanga bei hivyo ni biashara mbaya sana (2) Huwezi kupanga bei ya mafuta hivyo kama bei ya mafuta ikipanda huwezi kupandisha bei kwasababu bei inapangwa na serikali. Hali hii ilisababisha Isuzu NPR na Costa zishidwe kufanya biashara na hali ya daladala ni ya duni kuliko 1996!!.
Unaweza ukafanya biashara ya tender, fungua kampuni halafu katafute shele zinazohitaji magari halafu ingia mkataba na shule wa kuwapeleka watoto majumbani baada ya shule. Vilevile kama unamagari mazuri peleka card zako balozini ili uweze kuchukuwa wagani mbalimbali wanaokuja na group zinazotoka nje. Hii itakusaidia uhakika wa biashara, kukua kwa biashara na target yako ya watu ni nzuri badala ya kukimbizana na makondakta na matrafiki. Mimi nashauri usiige badilisha kidogo utaona matunda! Huu ni ushauri wangu ndugu
i did it and saw it pays...though trafick police are the major hindrance to the business....NA BILA RUSHWA BIASHARA ITAKUWA NGUMU...HIVYO NAKUSHAURI UTOE RUSHWA KWA TRAFIKI BIASHARA YAKO ITAFANIKIWA....! I DONT JOKE KATIKA HILI
PM ME FOR MORE
Mkuu,
Naomba kujua hiyo rushwa haiwezi epukika? Ni nini hasa hutokuwa nacho ili utoe rushwa? Ina maana ukifuata masharti yoote yaani yoote bado inabidi utoe rushwa??? Kama gari imelipiwa kila kitu, ina fire extinguisher nzuri, reflectors, dereva anafunga mkanda, anasimama vituoni tuu, hajazi watu what will make him pay rushwa?? Naomba kuelimishwa ingawa sifanyi hiyo bness. Mimi naendesha private car napita popote tz hii sitoi hata senti moja kwani nina kila kitu kwenye gari langu labda kwenye speed ya 30 aur 50 ndo wanikamate lakini nitatoa elfu ishirini na wanipe notification na risiti ya malipo. Otherwise sitoi chochote....
isipotimia ni deni, na asipolipa deni? Ukimshtaki dereva kwa madeni ya buku nne buku kumi utalipia zaidi kufungua kesi kuliko madai.masharti yako moja kutunza gari,hesabu kila siku icpotimia deni
dereva wa daladala akisababisha damage ya milioni 2, atakulipa nini mjomba? Hukuweka bima?akigonga kwa uzembe wake analipa,
akipigwa notification za uhakika na asipotoa anaswekwa lupango, utamfata mwenyewe kumdhamini na kulipia gari lako litoke. Upende, ukatae, huwezi kusema "makosa ni yake," itakula kwako.akikamatwa na makosa ya uzembe kama kutokuvaa uniform akiandikiwa ni yake, kusimama juu kwa juu akiandikiwa ni yake alafu
Na dereva mwenye uelewa hawezi kukubali kizunguzungu cha "mtaji wa full tank." Mtaji wa full tank ndio shilingi ngapi? Mafuta yanapanda bei asubuhi mchana na jioni, there is no such thing as "mtaji wa full tank."wape mtaji wa full tanki na kila siku akirudisha iwe full
JF MEMBERS,
biashara ya dala dala inanipasua kichwa,gari ziko mbili.(24 seats)
tatizo :madereva kila siku story,mafuta hawaweki.(utaskia Boss msingi wa mafuta umekata)wakiweka mafuta quality ya mafuta mbovu nahisi ni mafuta ya videbe.
Ma-Traffic ndo usiseme pasua kichwa.
Nimegundua kuwa hata nami naanza kubadilika tabia nakuwa kama machizi wa hii Dala-Dala industry.
Kama kuna mtu ameweza kuifanya hii biashara successfully anisaidie kumanage hii biashara kwa makato ya management fees.
raha ya ngoma uingie ucheze,huwezi jua Adha ya matrafiki kwa daldala mpaka uwe mdau ktk hii bizness.
trafic wa dar huwa wana targets za kila siku mtu apate revenue ya 50,000 and above.
so kila dreva wa daladala anakuwa analipa kitu inaitwa dambwe daily.around elfu4-10. sasa do the math. kwa daldala za ubungo posta zipo 200X6000=`1,200,000 gawa kwa trafic 12, wanaosimamia hiyo ruti for that day.kila mtu anapata laji moja. hapo tena kila mtu anatakiwa apelelke kwa bosi ,anagalau 15% of mapato.
nadhani sasa picha umeipata.