newmzalendo
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 1,388
- 583
Mkuu NM; hizo gari ziko kwenye condition gani? na zinafanya route ipi?
Asante sana kwa ushauri,zinapiga root ya mbagala -buguruni. nimeamua kuzitoa nitafute njia nyingine. kweli Mkuu inachanganya na kupasua kichwa ukichanganya hii biashara na kazi zingine.Tuwasiliana hata mie ninazo hapa mjini nitakupa uzoefu wangu,usichanganye hii biashara na kazi zako zingine .Awali nilikua nafanya hivyo nilitaka kuchanganyikiwa.
mkuu hii biashara ni nzuri sana tena inalipa aswa pale unapoisimamie 100% utaipenda hakikisha gari zipokwenye hali nzuri na umekamilisha vibali vyote shukuru upate madereva wazuri ucwape hesabu kubwa sana ingia nao mkataba wa maandishi kabisa umpe masharti yako moja kutunza gari,hesabu kila siku icpotimia deni,akigonga kwa uzembe wake analipa, akikamatwa na makosa ya uzembe kama kutokuvaa uniform akiandikiwa ni yake, kusimama juu kwa juu akiandikiwa ni yake alafu wape mtaji wa full tanki na kila siku akirudisha iwe full yani antakiwa aendeshe kama ofisi ila inatembea ni pm kwa mengi zaidi
mkuu ndo hivyo,dawa yake ni kutafuta management,ninazo 15,nina management team ya watu wanne.Huwa hatuwasiliani hadi mwisho wa mwezi,ndo tunapeana mahesabu,nimewakabidhi mamlaka yote.Ila kwa hili unahitaji mtu mwaminifu hasa ndugu wa karibu itakua vizuri zaidi,maana si unajua wabongo kwa kuchakachua.Asante sana kwa ushauri,zinapiga root ya mbagala -buguruni. nimeamua kuzitoa nitafute njia nyingine. kweli Mkuu inachanganya na kupasua kichwa ukichanganya hii biashara na kazi zingine.
Mkuu unazongapi.Je unaweza kufanya management on my behalf.
Leo nimeingia ktk majadiliano na rafiki yangu mmoja yeye ana Taxi7 in town,amenieleza jinsi anavyomanage ,ameoffer kufanya management .hatujaafiki Management Fees.so bado nipo ktk mchakato ,ntatoa feedbak soon.
Wakuu, naona mpo kadhaa wenye biashara hiyo hapa JF kwa nini msiorganize muanzishe kampuni na muwe professional? Nafikiri hii ingekuwa endelevu zaidi na haya matatizo mtayatatua pamoja na kuweka strategies nzuri na mtakuwa mfano wa watu wengine kufanya biashara ya daladala kama kampuni, kwa mtazamo wangu naiona hii ni industry ambayo haijapata watu wenye mtazamo mkubwa wa kueploit vizuri zaidi ya kila mtu kujichukulia kijipande chake akale kwake!
Inaweza ikawa ni initiative mpya kabisa ya kuanza kuleta watu kuumiza kichwa na ikaleta solution nzuri ya usafiri na msongamano wa Dar!
Sijui kama nimeenda mbali nje ya topic, nawakilisha!
mzuzu ... nakubaliana na wewe ... south africa wao bishara ya dala dala wanaita Taxi .... na kuna association ya Taxi owners kubwa sana ambayo basically inaoperate management wise ..... kama una taxi(daladala) unaipeleka kwenye umoja huo ... halafu unaingia mikataba na unapangiwa route ya daladala yako na mnakubaliana mapato ... hutokaa kuumiza kichwa hata siku moja na wala hata hautajua dereva ni nani... pesa zako utazikuta benki kila wiki zinaingia bila usumbufu[/QUOTE]
mkuu hapo kwenye red mfumo huu ukijaribu tu hapa umekwisha
mkuu ndo hivyo,dawa yake ni kutafuta management,ninazo 15,nina management team ya watu wanne.Huwa hatuwasiliani hadi mwisho wa mwezi,ndo tunapeana mahesabu,nimewakabidhi mamlaka yote.Ila kwa hili unahitaji mtu mwaminifu hasa ndugu wa karibu itakua vizuri zaidi,maana si unajua wabongo kwa kuchakachua.
Toyota hiace inafaasana kwa daladala inahimili na inafaa sana,ila caravan usiguse ndugu zinawahi kuchokasana na haziwezi kuhimili vishindo vya kazi ya dala5.
Kwa mikoa uliotaja, Toyota Hiace ndo inafaa lakini kwa Dar Toyota Hiace Diezel ndo inafaa. Kwa Mwanza pia inategemea ni njia gani uta prefer. Kama ni njia ya Igoma chukua Hiace ya Petrol. ANGALIZO: Kwa uzoefu nilioupata, Toyota Hiace petrol ni bora sana kwa Tz coz ni cheaper 2 maintain.Asante sana mwera kwa ushauri wako. mkoa tutachagua kati ya mwanza na Dar