Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Hivyo vigezo we unavyo? Biashara ya kuchangia watu wawili inachangamoto zake kumbuka, tena wa kumtafuta JF hata hamfahamiani background na mengineyo! Nenda katafute pesa zilizobaki kisha rudi fanya biashara, we ndo unaanza halafu unataka uanze na kila kitu! hata kavu kwanza zinatosha, ukitaka labda na mishkak then kusanya hela ndo ukuze mtaji.
 
Wakuu nataka kuanza biashara ya chipsi hapa Dar. Kwa anaefahamu sehemu nzuri yenye watu wengi inayofaa kwa biashara tajwa kwa maeneo ya Ubungo,Kimara, Mwenge,Makumbusho au sehemu nyingine yeyote inayofikika kiurahisi anisaidie.
 
Nadhani sehemu nzuri ni maeneo yenye wanafunzi wengi!!! Kama karibia na hostels na vyuo. Pia vituo vya daladala
Ko fanya utafiti ujue wapi pana hizo sifa.
 
Kijana kwanz umefanya vizuri kuomba ushauri, achana na watu wenye mawazo mgando, mimi ninauzoefu kiasi flan juu ya biashara ya chips. Biashara ya chips inaweza ikakulipa sana tu bt katika mazingira ya fuatayo mbali na mtaji.1: LOCATION: hiki ni kitu cha msingi sana unaweza kuwa na mtaji wa kutosha bt ukikosea location inakula kwako-tafuta hasa eneo ambalo lina traffic ya watu au sehem za biasha na maofisi: 2 Usimamizi wa karibu-usimamie wew mwenyewe au mtu wako wa karibu sana la sivo vijana watakuliza, kuwa makin kutafuta vijana wa kukusaidia kazi zingatia hasa uaminifu: 3:good customer care na ubunifu kwenye biashara: ukizingatia haya biashara hii inaweza kukulipa net profit ya laki mbili kwa siku :NB itatemeana na eneo utakalotafuta bt m3 inatosha sana
Naweza kukupata 0769635970
 
Mgahawa wa Aljazeera uliopo Kigogo, Dar es Salaam unawatangazia vijana wote wajasiriamali kuwa kunahitajika kijana mchapakazi atakaeendesha shughuli za kuuza Chips hapa mgahawani. Vifaa vya kazi vyote vipo. Kwa walio tayari na wenye uzoefu na nia basi tunawakaribisha waje hapa mgahawani tuelezane kwa kirefu. Au piga 0757528827.
 
Natanguliza salam kwanza,

Mimi ni kijana ambae nimetoa aibu na uoga ili nisake pesa nikafungua banda la chipsi mitaa flani hivi Temeke DSM, kwa bahati nzuri nikaotea sehemu ambayo ni nzuri kidogo na uhakika wa kumaliza debe kwa siku upo yaani kuanzia saa 6-4 usiku mixer na mayai trei, kuku1na mishkaki.

Sasa ugumu upo kwenye kuicontrol hii biashara mana mimi nasoma chuo saivi tupo kwenye mafunzo kwa vitendo, nikishinda mimi siku za weekend uwa napata mauzo kama elfu 90 hivi nikitoa mtaji nakuta na faida kama 30-35 nagawa kwa vijana wawili 5000 kwa kila mmoja na nabaki na kama 20 hivi.

Sasa nikimpa kijana aongoze jaazi nakuta napata faida 12 hata biashara ikiwa mbaya naipata 10 so nikubaliane na hali kama nikiwaachia vijana au nifanyeje wakuu ushauri wenu ni muhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko mwaka wa ngapi mkuu?

Sent from my Dell Laptop using Jamii Jorums mobile app
 
kwanza acha ulofa na ufala. kufanya biasha ya chips haiamanishi lazima ujitoe aibu na uoga. hujui chips ndiyo zinawapa mimba kila siku watoto kike toka shule za msingi, sekondari hadi chuo?.
pili tulia faida ya 12000 hadi 10000 kwa siku wakati unamambo yako ni kubwa sana. hii pesa kwa mwezi ni sawasawa na 300000. hapa unalingana na wafanyakazi wengi sana wamaofisini ambao wanatumia na nauli kwenda makazini.
 
Kuna kitu hujakiweka wazi,umesema ukikaa wewe faida inayopatikana ni kubwa na wakikaa madogo wanazingua, ni kwamba wanaiba au mauzo ndo yanapungua tu.?
1. Wape motisha vijana hata kuwaongezea pesa unayowalipa maana wanajua mauzo ya hapo, so lazima itakuwa utendaji wao unashuka sabab wanaona wanalipwa kidogo.
2.usikae mda mrefu bila kuzungukia maeneo sio wikiend hadi wikiend angalau basi ukitoka kwenye mishe zako hata kuanzia moja usiku unakaa hadi saa 4.
3.fanya uchunguzi ujue tatizo liko wapi japo hii ilitakiwa iwe la kwanza kulifanya
4.Nishawahi kutana na changamoto kama yako mwisho wa siku nikatafuta ndugu yangu ninae mwamini nikamweka na mambo yakaenda poa sana
 
kwanza acha ulofa na ufala. kufanya biasha ya chips haiamanishi lazima ujitoe aibu na uoga. hujui chips ndiyo zinawapa mimba kila siku watoto kike toka shule za msingi, sekondari hadi chuo?.
pili tulia faida ya 12000 hadi 10000 kwa siku wakati unamambo yako ni kubwa sana. hii pesa kwa mwezi ni sawasawa na 300000. hapa unalingana na wafanyakazi wengi sana wamaofisini ambao wanatumia na nauli kwenda makazini.
poa mkuu thanks for your advice

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa harakatii unazozifanya mana huwa naziona thread zako nyingii ukiomba ushauri wa biashara....vilee na ilee saloon ipoooo bado...???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom