Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Mkuu au niingie mwenyewe mzigoni nimpige kwanza huyu mfanyakaz pending?
Ndo itakupasa ufanye uchunguzi kwanza kabla ya ku conclude.

Tafuta wauza Chips uwaulize kwao inakuaje, wakifanyaje wanapata loss wakifanyaje wana gain.

Yaonyesha huku survey vizuri
 
Mswahili bana, we mwenyewe umechoka halafu unataka kujifanya ofisa uje kukusanya hesabu tu?

Hivi ni lini mtajifunza kwa wahindi? Hebu pita migahawa ya wahindi kama hujawakuta mke na mume wanakaba wenyewe cashier.
Hapana nilikuwa bize kidogo na issue fulan nafatilia hvyo ilibid niweke mtu kwanza.
 
Wadau naomben mnisaidia nimefungua kasehem kwaajili ya kuuza chipsi na huu ndo mwanzo yaani naelekea kukata tamaa maana kila siku nakula loss na nilikuwa nimeweka mtu nakosa hata pesa ya kumlipa em nisaidieni nifanyeje ili niikuze hiyo biashara? Maana wateja nnao wapata niwachipsi kavu tu hasa hata faida ikija nikidogo au kwakuwa ndo mwanzo au nifanyeje ili nikuze biashara yangu.
Hii biashara ina changamoto sana mkuu!
But kwa experience yangu, niliwahi kuifanya kwa takribani miezi 8 hivi iko hivi..
1. Biashara ya chipsi huwezi ukaona faida kwa kuuza chipsi peke yake, hapo ni lazima uweke products zingine mfano. Mishikaki, ndizi, sausage, samaki, kuku, sambusa, kacholi...etc
2. Chipsi huwa zina hasara kwasababu ya upimaji wa chipsi kavu ni tofauti chipsi mayai hapo inabidi upate sahani zenye plain surface ( isiwe imeingia kwa ndani) pia lazima umbane muuzaje na Mara kwenye viazi mfano Mimi ndoo kubwa nilikua nanunua kwa elfu 15-17 nikiuza mpaka vikiisha napata Faida ya elfu 14-16 (hapo ni chipsi kavu tu nimepigia hesabu)
3. Weka kipimo ambacho hakimfurahishi mteja wala hakimfukuzi mteja ( pima kipimo ambacho ni average kwa kila sahani).
4. Kupunguza gharama usitumie mkaa Mwanzo mwisho unaweza tafuta jiko la maranda au Kuni mkaa tumia kwenye kukaangia chipsi mayai, kuchoma mishikaki, na kupashia chipsi.
Pia viazi nunua gunia kama mtaji unaruhusu, mafuta ya kukaangia nunua walau kindoo cha lita 10 na mayai kama trei tano, then piga kazi hapo utaona mabadiliko na faida utapata.
N.b kumbuka faida ya chipsi ni ngumu kuiona kwa sababu ina gharama nyingi za ziada mfano. Mkaa ( gas), mafuta, tomato, kachumbari, pilipili etc.
 
Hii biashara ina changamoto sana mkuu!
But kwa experience yangu, niliwahi kuifanya kwa takribani miezi 8 hivi iko hivi..
1. Biashara ya chipsi huwezi ukaona faida kwa kuuza chipsi peke yake, hapo ni lazima uweke products zingine mfano. Mishikaki, ndizi, sausage, samaki, kuku, sambusa, kacholi...etc
2. Chipsi huwa zina hasara kwasababu ya upimaji wa chipsi kavu ni tofauti chipsi mayai hapo inabidi ipate sahani zenye plain surface ( isiwe imeingia kwa ndani) pia lazima umbane muuzaje na Mara kwenye viazi mfano Mimi ndio kubwa nilikua nanunua kwa elfu 15-17 nikiuza mpaka vikiisha napata Faida ya elfu 14-16 (hapo ni chipsi kavu tu nimepigia hesabu)
3. Weka kipimo ambacho hakimfurahishi mteja wala hakimfukuzi mteja ( pima kipimo ambacho ni average kwa kila sahani).
4. Kupunguza gharama usitumie mkaa Mwanzo mwisho unaweza tafuta jiko la maranda au Kuni mkaa tumia kwenye kukaangia chipsi mayai, kuchoma mishikaki, na kupashia chipsi.
Pia viazi nunua gunia kama mtaji unaruhusu, mafuta ya kukaangia nunua walau kindoo cha lita 10 na mayai kama trei tano, then piga kazi hapo utaona mabadiliko na faida utapata.
N.b cha muhimu zaidi usitegemee chipsi pekee ndio zikupe faida, ongeza makorokoro mengi kama niliyokutajia.
Mkuu naweza ingia pm nawe?
 
Mnaosema biashara ya chips ina faida kubwa ni kwamba hamjawahi kuifanya. Hiyo biashara ina changamoto kubwa sana kuliko inavyodhaniwa. Kwa pamoja tusome comment ya NAREI maana kaandika points za muhimu
 
Yaan inachangamoto nying mno.
 
Usiuze chips kavu kama ilivyo, bali ichanganye na hoho, carot etc.
Mtu akitaka mishkaki, mdondoshee na vichips kavu 6, afu uja hapa or thank me later.
 
Nilifungua hiyo biashara lkn hamna kitu nilifungua maeneo ya chuo lakini wanafunzi wanaenda sehemu walizozizoea hadi nikaamua kufunga,,,so kwa ushauri wangu japo wengi mtanizodoa lkn tafuta njia za pembeni za kuvuta wateja walau kwa mwezi,baada ya hapo km chipsi nzuri watabaki tu kwako
 
Wadau naomben mnisaidia nimefungua kasehem kwaajili ya kuuza chipsi na huu ndo mwanzo yaani naelekea kukata tamaa maana kila siku nakula loss na nilikuwa nimeweka mtu nakosa hata pesa ya kumlipa em nisaidieni nifanyeje ili niikuze hiyo biashara? Maana wateja nnao wapata niwachipsi kavu tu hasa hata faida ikija nikidogo au kwakuwa ndo mwanzo au nifanyeje ili nikuze biashara yangu.
Mimi sijui mambo ya chipsi, lakini ninachojua biasha Yoyote ili ikulipe sharti la kwaza demand ya bidhaa iwe juu.
Wanunuzi wawe wakutosha hiyo sehemu.

Ikiwa kama wanunuzi ni wengi ila ni wakugombania, basi jitahidi uwe tofautiktk kutoa huduma yako, kwa kuzingatia usafi, upikaji mzuri wa chips na ujazo. Siwezi kula ma Chips yako kama unapika ovyo!!

Jitathimini wewe na muuzaji wako na huduma zako, je zina kidhi haja ya walengwa?? Na kama zina kidhi na bado una lamba loss, je unaibiwa???

Pambana na hali yako mkuu
 
Nilifungua hiyo biashara lkn hamna kitu nilifungua maeneo ya chuo lakini wanafunzi wanaenda sehemu walizozizoea hadi nikaamua kufunga,,,so kwa ushauri wangu japo wengi mtanizodoa lkn tafuta njia za pembeni za kuvuta wateja walau kwa mwezi,baada ya hapo km chipsi nzuri watabaki tu kwako
Hahahahah eti wengi mtanizodoa”
Nimecheka balaa.

Njoeni kwangu nina dawa za kuvuta wateja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom