Habarini wana jukwaa,najua ni usiku wengine tupo tunakunywa mbili tatu na huku kukiwa na hali ya hewa murua sana nyanda za juu kusini kama mjuavyo.
Siyo kila anayekesha bar anasherekea m, wengine tunatumia muda kuwaza jinsi mambo yanavyokuwa magumu kwenye mitikasi yetu.
Biashara ngumu jamani!, au hapa nlipo mzunguko wa hela ndiyo mdogo,mbona watu wanapesa sana huku lakini.. Watu mkitoka Chunya kwani hela mnazipeleka wapi mpaka zipitize huu mji wetu?🙂
Anyway,point yangu imekuwa mbali,lakini naomba unipe moyo wewe uliyefanikiwa kwenye biashara yako,ilikuchukua muda gani mpaka ikaanza kukuingizia faida? Naona yangu hii inaenda kumaliza zaidi ya miezi mi4 nikipiga operational costs bado sioni faida. Nliifungua kwenye eneo ambalo linahitaji promosion sana watu kupafahamu,lakini naamini watu huwa wanafuata huduma na kwangu watapafahamu,lakini itachukua muda gani?😐😐😐
Watu wa Mbeya tumieni hela jamani mnaweza nilenga namimi bila kujua.
NOTE: sitaongelea ni biashara ya aina gani,wewe toa ushauri wako kwa general experience yako tu ita cross-cut pote.
Haya ngoja nirudi kwa wife kama ntafunguliwa mlango🏃🏃🏃🏃
Ngoja nikupe ushauri general watu wanaofanikiwa kwenye biashara wanakuwa na sifa zipi au wanafanyaje kwenye biashara zao hadi unawaona wanafanikiwa,nina imani biashara yako ni mpya na ndio maana umekuja kuomba ushauri.
1.Kitu cha kwanza kabisa unatakiwa ujue watu wa katika eneo lako wanahitaji nini au wana tatizo gani linalowasumbua halafu wewe ndio ulete utatuzi wa jambo hilo usiuze biashara ya vitu ambavyo umeviwaza wewe tu kichwani kwako.
Kwa mfano kama unaishi kwenye eneo ambalo watu wana shida ya maji wewe anzisha mradi wa kuuza maji utapata wateja.
2.Kitu kingine wakati unaanza biashara ukishatenga pesa ya mtaji na kodi zote hakikisha una pesa nyingine ya ziada kwa ajili ya kuendesha maisha yako kwa muda hata wa mwaka mmoja bila ya kutegemea biashara ndio ihudumie familia utakwama maana kwa kipindi cha mwanzo faida itakuwa ni ndogo na itaishia tu kwenye kuhudumia biashara tu ili isife.
3.Hakikisha umejipangia malengo yako ya muda mrefu,kwa mfano umeanza na biashara ya mgahawa lakini malengo yako ni kuja kumiliki hotel so usibweteke hadi lengo lako la kumiliki hotel litimie.
4.Jitangaze/fanya marketing usingoje hadi mteja aje mwenyewe hii staili imepitwa na wakati siku hizi biashara yoyote inahitaji utengeneze connection kuanzia kwa marafiki,ndugu,majirani ukiwaalika kuja kupata huduma na huduma yako ikiwa nzuri watakuletea na wateja wengine.
Ongea na watu vizuri,usidharau mtu wa aina yoyote ongea hata na bodaboda wawe wanakuletea wateja au unawapa vipeperushi wanavisambaza kisha unawalipa hela ndogondogo.
Tangaza na mitandaoni pia facebook,Instagram,Tiktok weka mawasiliano yako.
5.Hakikisha bidhaa zako ziwe zina upekee fulani ukilinganisha na wapinzani wako lakini bei pia iwe na unafuu kidogo kulinganisha na wapinzani wako hapo utawavutia wateja na wataanza kusimuliana kuhusu bidhaa zako.
6.Uvumilivu-Hapa ndipo pagumu na wafanyabiashara wengi wanaoanza biashara huishia kati na kunyoosha mikono juu.
Mtu anafanya kwa miezi 3 akishaona hapati hela alizotarajia anaachana nayo anarukia kitu kingine hakikisha unakuwa king'ang'anizi hadi utengeneze jina faida zitakuja mbeleni.