Biashara ndogo ndogo zinachangamoto kubwa

Labda utusaidie.umewezaje kudhibiti uaminifu wa wafanyakazi.au unakaa mwenyewe

Moja niko mwenyewe nyingine ndo ina mtu.......
Siku zote mi napenda kufanya biashara ya vitu vinavyohesabika! ukiweka mtu hesabu mali yako muachie muuzaji afanye kazi.
sio umetoka kazini umepitia hela ya mafuta ya gari sijui hela ya kula nyumbani! tenga muda kama ni baada ya kila wiki2 fanya hesabu na mfanyakazi ujue hasara yako na faida
 
Hili la wizi ndo tatizo namba moja kusema ukweli hata watu ambao unaweza kusema wana professions za maana ukiwaacha kwenye duka wanaiba, kuna Accountant alikuwa anakuja kupiga mahesabu ya duka yaani ukigeuka tu anachomeka bidhaa kwenye soksi! Hadi ndugu tatizo ni hilo hilo.

Wahindi inaonekana family members hawaibi kwao na nina wasiwasi wanapeana space kwa bei nafuu wenyewe kwa wenyewe kwenye hizi sehemu za uindini maana bishara zengine ukiziangalia ni shida kusupport hata rent ya hilo eneo.
 
30m daah pole mkuu!mi kiukweli nilikata tamaa sana kwa yaliyonikuta 2013,niliwekeza Mpesa na Modern Hair dressing salon,nakumbuka kwa mwaka nilipata faida 30,000 kwenye salon.usimamizi hafifu kazi za ofisi zilibana.2014 nikawekeza kwenye nyumba,imeisha kodi laki 2 si haba regarding no hurt running cost.na boda boda zangu 2 kwa ajili ya recurrent expenditure.Naungana na wewe vibiashara vidogo vinaumiza kichwa sana.hakuna realistic profit,daaah sijui muuza duka rejareja anapataje faida
 
zanzibar. spices mkuu nimekuelewa sana kaka safi sana ayo ndo matunda ya mtuu kua msomi naona ushauri wako upo kisomi zaidi shukurani sana mkuu.. nimetoka na kitu apo
 
Hili la wizi ndo tatizo namba moja kusema ukweli hata watu ambao unaweza kusema wana professions za maana ukiwaacha kwenye duka wanaiba, kuna Accountant alikuwa anakuja kupiga mahesabu ya duka yaani ukigeuka tu anachomeka bidhaa kwenye soksi! Hadi ndugu tatizo ni hilo hilo.

Wahindi inaonekana family members hawaibi kwao na nina wasiwasi wanapeana space kwa bei nafuu wenyewe kwa wenyewe kwenye hizi sehemu za uindini maana bishara zengine ukiziangalia ni shida kusupport hata rent ya hilo eneo.
Aisee!!! :teeth: huo ni ufundi!! Sasa hebu fikiria huyo bwana "accountant" ndo umemuajiri kumanage mifedha, aisee
 
Tatizo letu sisi waswahili tunafanya biashara kwa kuiga tu na pia watu wengi wanafanya kwa ajili ya kuganga njaa tu ili kupunguza ukali wa maisha ambapo unakuta mtu ameajiriwa halafu wanafanya haya mambo ambayo wanaita kujiajiri wakati umeajiriwa tofauti na wahindi ambao binafsi kwenye mambo ya kuajiriwa na kujiajiri hivyo vitu kwao havi exist
 
Mkuu unasema biashara ndogo ndogo zinachangamoto nyingi !ni vizuri kwa kua umeona ni changamoto na sio matatizo!basi bila changamoto hakuna biashara!
 
iMind hata mimi yamenikuta nimejitahidi karibu mwaka na nusu sasa ila kwa sasa nimemwaga manyanga yaani nimeshindwa kwanza wafanyakazi pasua kichwa unamtumia nauli anakaa miezi miwili anadai kuondoka anaondoka anaacha sehemu ya biashara imefungwa mpaka ukija kufungua tena wateja washasahau khs uwo wizi ndio usiseme mpaka najiuliza wenzangu wanaweza vipi mbona mimi nashindwa kabisa jamani nao pia wanategemea wafanyakazi kama mimi jamani mwenye maujuzi atujuze na sisi nimeshindwa biashara ndogondogo ingawa nilikua na fursa nzuri sana mtaani kwangu ila naona nimeshindwa kabisa
 
Sasa Dada yangu Sharifa kwenye biashara kuna sehem mbili za kuangalia.
Tatizo la muajiriwa na muajiri.
Sasa maelezo yako hapo juu ni kwamba muajiriwa hana tatizo ila wewe muajiri ndio tatizo na ndio janga.
Sasa dawa ya tatizo lako unayo mwenyewe.
Inakuwaje biashara inayokulipa vizuri mtaani kwako halafu usema inakushinda kwa kudai wafanyakazi pasua kichwa.
Mbona wakati walipokuwa wakifanya biashara hadi wewe kugundua inakulipa hukusema asante kwao na badala yake ukala bata peke yako.
Kama biashara yako inakulipa vizuri kama umevyosema basi ajiri watu wawili hasa kipindi huyo anapokuwa anaeda likizo au anaumwa.Watu watu kibao unaweza kuajiri kwa muda wa mwezi,ni bora umlipe pesa nyingi lakini sehem ya biashara iwe wazi.

Na pia tujifunze kutoa motisha kwa wafanyakazi wako,kama mfanyakazi utampa motisha nzuri wakati wa kurudi likizo basi anaweza hata mwezi usifike akarudi kazini.Kuna wafanyakazi wangapi humu wapo likizo lakini wanaenda kazini hata kupiga story kulingana na mazingira ya kazi na muajiri wake.

Nakumbuka mie wakati naenda nyumbani kuoa,muajiri wangu alinipa Ticket ya ndege kwenda na kurudi na wife.
Sasa lengo sikwamba ananipa offer bila malengo,la, lengo lake ni kwamba nikitumia usafiri wa train ni siku mbili,na pia lazima ni book kwa wiki kadhaa ndio nipate.Sasa akajua kwamba kama akinipa bonus hiyo lazima nitakuwa na hashuo la ndege na nitarudi mapema.Na kweli trip hiyo ndio ilikuwa ya Kwanza wa Wife kupanda ndege.Ikanipa maujiko kweli.Mtaani wakajua Bakhressa nimeenda kuoa.Mwisho wa Reli tena,siunajua tena .Mme kaja kwa ndege na karudi na mkewe kwa ndege.
Sasa hapo iliniwezesha kurudi ndani ya wiki moja tu na kuanza kazi kama kawaida kwa amani na furaha,na kumshukuru sana boss kwa kunipatia tickets za ndege kwenda na kurudi,lakini hapo ujue ni kwamba nafasi yangu ni muhim sana na ilikuwa ni msimu wa kazi.Sasa alijua kabisa kwamba lazima acheze na rasilimani mtu.Is very technical

Sasa kama wewe sehem inalipa unashindwa ku pick staff mwingine?yaani jinsi watu wanavyohaha kutafuta ajira kesho tu ukitangaza unawapata.
Na hii inaoneysha kwamba hata mfanyakazi wako alikuwa akiumwa basi unafunga biashara,
Kwa ufupi tangu nazaliwa ndio naona na kusikia biashara hiyo yako inafungwa mtu akienda likizo.

Sasa kwa maelezo yako hapo juu,tatizo ni wewe mwenyewe na sio muajiriwa wako.
 
Zanzibar spices; naona hujanielewa mi nadhani Luna tofauti Kubwa sana ya fursa na kulipa wewe umeongelea kua biashara yangu inalipa sio ivyo unavyofikiri wewe Mimi nimemaanisha kua biashara niliyofungua mtaani kwangu ni tegemeo kwao cha kusikitisha sijawahi kula matunda ya biashara yangu ingawa watu wanaingia na kutoka kwa mahitaji; elewa kua biashara sio Kubwa kiivyo ni biashara ndondogo tu nilichoambulia ni hasara tupu
 
Huwa najiuliza sana kwa nini wahindi wanafanikiwa sana kwenye biashara zao nakosa jibu, ingawa kuna ujanja janja na magumashi ya kodi kodi wafanyao ila hawa jamaa wapo serious sana na biashara zao, na wapo makini sana kwenye usimamizi, kinachotuangusha sisi wabongo wengi ni usimamizi hafifu, watu wanafanya biashara kwa kubahatisha bahatisha, kukata tamaa mapema, na mwisho kabisa ni watu tunaowaajiri haijalishi awe ndugu yako au rafiki ama mtu baki ni mwiba sana, na wana formula zao kabisa kwamba akipata chance ni kuiba tu.

Mkuu..khs wahindi nikweli wako Serious kwenye Biashara lkn kwenye mambo ya NDUMBA wako mstari wa mbele miaka ya 90"s nimefanyakaz kwao nawafahamu vzr sana
 
Malengo yangu 2014 yalikuwa ni kusimamisha biashara kadhaa ndogo ndogo. Biashara ambazo Inaweza kunipa faida ya Tsh 20000 hadi 50000 kwa siku.

Bahati mbaya hadi mwaka unaisha sijaweza kufanikiwa. Kwa kifupi mwaka huu umekula kwangu. Nimepoteza si chini ya 30m katika uwekezaji usio na tija. Kakatika kipindi chote nilichojaribu kusimamisha biashara ndogo ndogo nimejifunza yafuatayo;
1. Ni vigumu kupata watumishi waaminifu.Amini usiamini TZ kila mtu ni fisadi. Watu ni wezi kuliko unavyoweza kuamini. Kama haupo kusimamia mwenyewe shughuli za kila siku basi biashara ndogo ndogo huwezi kufanya.

2. Kodi ya pango ya frame ni unrealistic. Kodi ya frame nyingi ni kubwa kuliko unavyoweza kuzalisha. Mwisho wa siki unamfanyia biashara mwenye frame.

3. Uwezo wa kununua wa wa TZ walio wengi uko chini sana. Wengi wanapenda vitu vya bei rahisi bila kujali ubora. Ndo maana soko la vitu vya kichina vina shamiri. Wako wachache wanaojali ubora lakini ni wachache sana.

4. Ulozi umetawala katika biashara ndogondogo, kama siyi mwenzao utapigwa vita kila kona.

Naomba kuwasilisha.

Hongera sana mkuu, nakubaliana na yote ulioyataja except namba 4 tu,
Pili mwaka 2014 kiuchumi ulikuwa chini sana, nayo ni factor kubwa sana kwa mafanikio ya biashara,
Inaendelea kadri ntakapopata muda pole sana tuko wengi
 
Malengo yangu 2014 yalikuwa ni kusimamisha biashara kadhaa ndogo ndogo. Biashara ambazo Inaweza kunipa faida ya Tsh 20000 hadi 50000 kwa siku.

Bahati mbaya hadi mwaka unaisha sijaweza kufanikiwa. Kwa kifupi mwaka huu umekula kwangu. Nimepoteza si chini ya 30m katika uwekezaji usio na tija. Kakatika kipindi chote nilichojaribu kusimamisha biashara ndogo ndogo nimejifunza yafuatayo;
1. Ni vigumu kupata watumishi waaminifu.Amini usiamini TZ kila mtu ni fisadi. Watu ni wezi kuliko unavyoweza kuamini. Kama haupo kusimamia mwenyewe shughuli za kila siku basi biashara ndogo ndogo huwezi kufanya.

2. Kodi ya pango ya frame ni unrealistic. Kodi ya frame nyingi ni kubwa kuliko unavyoweza kuzalisha. Mwisho wa siki unamfanyia biashara mwenye frame.

3. Uwezo wa kununua wa wa TZ walio wengi uko chini sana. Wengi wanapenda vitu vya bei rahisi bila kujali ubora. Ndo maana soko la vitu vya kichina vina shamiri. Wako wachache wanaojali ubora lakini ni wachache sana.

4. Ulozi umetawala katika biashara ndogondogo, kama siyi mwenzao utapigwa vita kila kona.

Naomba kuwasilisha.

UKO SAHIHI SANA mkuu
 
Back
Top Bottom