Biashara ndogo ndogo zinachangamoto kubwa

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,900
4,436
Malengo yangu 2014 yalikuwa ni kusimamisha biashara kadhaa ndogo ndogo. Biashara ambazo Inaweza kunipa faida ya Tsh 20000 hadi 50000 kwa siku.

Bahati mbaya hadi mwaka unaisha sijaweza kufanikiwa. Kwa kifupi mwaka huu umekula kwangu. Nimepoteza si chini ya 30m katika uwekezaji usio na tija. Kakatika kipindi chote nilichojaribu kusimamisha biashara ndogo ndogo nimejifunza yafuatayo;
1. Ni vigumu kupata watumishi waaminifu.Amini usiamini TZ kila mtu ni fisadi. Watu ni wezi kuliko unavyoweza kuamini. Kama haupo kusimamia mwenyewe shughuli za kila siku basi biashara ndogo ndogo huwezi kufanya.

2. Kodi ya pango ya frame ni unrealistic. Kodi ya frame nyingi ni kubwa kuliko unavyoweza kuzalisha. Mwisho wa siki unamfanyia biashara mwenye frame.

3. Uwezo wa kununua wa wa TZ walio wengi uko chini sana. Wengi wanapenda vitu vya bei rahisi bila kujali ubora. Ndo maana soko la vitu vya kichina vina shamiri. Wako wachache wanaojali ubora lakini ni wachache sana.

4. Ulozi umetawala katika biashara ndogondogo, kama siyi mwenzao utapigwa vita kila kona.

Naomba kuwasilisha.
 
ulozi maana yake nini?

Uchawi, mtu kutumia uchawi kuvuta wateja kwenye biashara yake.

Tatizo la uchawi linachangiwa na kufanya biashara za kufanana na nyingi katika eneo moja wakati wateja hawaongezeki, hivyo badala ya baadhi ya wafanyabiashara kutumia mbinu za kibiashara mf kupunguza bei hata sh.tano, au kumwongezea mteja ili kumvuta, yy anatumia nguvu za giza.

Watu wamepanga foleni kumi wanauza vitumbua na maandazii, vitumbua vya bi fulani visipoisha wengine hawauzi!!!!
 
Nime kupata mkuu....hiyo ni changamoto nzito sana.
 
Kwa upande wangu biashara ndogondogo zinalipa sana.. location na target yako ni jambo la msingi.....

Ukiwapo mwenyewe na una muda wa kusimamia kikamilfu kweli inalipa. Lakini kwa sie ambao tuna kazi nyingine ambazo zinatubana ni changamoto kubwa. Hasa kutokana watu kuto kuwa waaminifu.
 
ulozi maana yake nini?

Binafsi siamini ulozi na sijawahi na wala sitegemea kwenda kwa waganga kutafuta nyota ya biashara.

Lakini mara kadhaa nimekutana na vitu vya ajabu nje ya frame yangu. Ingawa hadi kesho siamini kama vitu hivyo vimechangia kufanya nishindwe. Ila vipo.
 
Kwa kweli hayo mambo ypo ila ki ukweli si ya kujihusisha nayo huko ni kujitakia nuksi,amini katika Mungu utashinda tu.
 
Bila uchawi huwezi fanya biashara wewe zubaa tu shauri yako utakufa masikini. Hata Bill Gates anatumia ndumba
 
Huwa najiuliza sana kwa nini wahindi wanafanikiwa sana kwenye biashara zao nakosa jibu, ingawa kuna ujanja janja na magumashi ya kodi kodi wafanyao ila hawa jamaa wapo serious sana na biashara zao, na wapo makini sana kwenye usimamizi, kinachotuangusha sisi wabongo wengi ni usimamizi hafifu, watu wanafanya biashara kwa kubahatisha bahatisha, kukata tamaa mapema, na mwisho kabisa ni watu tunaowaajiri haijalishi awe ndugu yako au rafiki ama mtu baki ni mwiba sana, na wana formula zao kabisa kwamba akipata chance ni kuiba tu.
 
biashara ya usafirishaji mf. bodaboda,bajaj,teksi, hiace ndio hatari makonda na madereva wanaiba balaa
 
Achana na biashara za UTWANA na UBWANA.Tafuta mfanykazi mpe hata hisa 10%,au mwongeze marupurupu mfanye the part of buz
 
Huwa najiuliza sana kwa nini wahindi wanafanikiwa sana kwenye biashara zao nakosa jibu, ingawa kuna ujanja janja na magumashi ya kodi kodi wafanyao ila hawa jamaa wapo serious sana na biashara zao, na wapo makini sana kwenye usimamizi, kinachotuangusha sisi wabongo wengi ni usimamizi hafifu, watu wanafanya biashara kwa kubahatisha bahatisha, kukata tamaa mapema, na mwisho kabisa ni watu tunaowaajiri haijalishi awe ndugu yako au rafiki ama mtu baki ni mwiba sana, na wana formula zao kabisa kwamba akipata chance ni kuiba tu.
Biashara nyingi za wahindi ni za famila. Wanasimamia wenyewe. Yaani Baba, mama, watoto, wajukuu.

Kinachotuangusha sisi wengine ni kufanya biashara kwa remote. Yaani tuna shughuli zingine say umeajiriwa, Monday to friday uko kazini huku kwenye biashara umeacha mwingine kusimamia.

Ukipata bahati ya wasinamizi wazuri utafabikiwa. Lakini wengi wao watakuangusha tu.
 
Achana na biashara za UTWANA na UBWANA.Tafuta mfanykazi mpe hata hisa 10%,au mwongeze marupurupu mfanye the part of buz

Tatizo ni uaminifu tu, hata umlipe kiasi gani bado kuna gubu la tamaa, wangapi wanalipwa vizuri na bado wanaiba, hiyo hisa 10% atapata na bado ataiba. Mwisho wa siku tatizo vijana wanataka mafanikio ya haraka ndani ya muda mfupi.
 
Achana na biashara za UTWANA na UBWANA.Tafuta mfanykazi mpe hata hisa 10%,au mwongeze marupurupu mfanye the part of buz
Kuna ndugu yangu mmoja aliniambia ukimpa mchaga au mpemba kysimamia biashara yako hatakuangusha. Baada ya miaka michache atakuwa ameanzisha biashara yake na biashara yako iko pale pale. Lakini watu wengine basda ya mwaka atakuwa hana kitu na biashara yako imekufa.

Hivyo ukimpata 'Mchaga' au 'Mpemba' siyo kwa maana ya kabila la hasha bali mtu anayejitambua na mchapakazi hii idea yako itafanya kazi. Lakini walio wengi watakuangusha tu.
 
Binafsi siamini ulozi na sijawahi na wala sitegemea kwenda kwa waganga kutafuta nyota ya biashara. Lakini mara kadhaa nimekutana na vitu vya ajabu nje ya frame yangu. Ingawa hadi kesho siamini kama vitu hivyo vimechangia kufanya nishindwe. Ila vipo.

Nakuunga mkono hapa, uchawi au kwenda kwa mganga eti utengeneze pesa utaishia kuua albino, mtoto, kunywa visivyokunywa na kulala makaburini bila kuambulia chochote, zaidi sana sana huyo tapeli mganga ndio utasikia kaenda kununua flat tv au muziki..
Biashara ndogo ndogo faida zake ni ndogo, ila utafanikiwa kama ulivyoshauriwa hapo juu na jamaa, location na target ya customer wako, ofcourse itategemea pia promotion, price na customer services..MUHIMU hapa ni ni sales sales sales, kuuza sana stock yako..
Kinachonisikitisha ni pale napoenda dukani, nataka kitu naambiwa hakipo au kimekwisha na wala huyo muuzaji haandiki pembeni kuwa hivi vitu tununuwe baadae, kesho na siku zote zinazofuata bado hicho au hivyo vitu bado havijawa restocked, sasa hapo unakuwa unajiuliza je huyu anatania au anafanya biashara, inakuwa kama hio biashara ipo ipo tu uonekane kama nawe unachacharika, katika customer services hili linawaangisha wengi, maana utakuta dada anapaka rangi kucha, au anaongea na simu, au anapiga domo tu na mshikaji au kalala sakafuni, nakwambia hataamka wala kujisumbuwa kukusalimia na kukukarisbisha na kukuuliza unatahitaji nini..
Inabidi kuwa makini sana hapa, ama sivyo utakuwa unapoteza hela na muda wako tu kwa kweli..
 
Kuna ndugu yangu mmoja aliniambia ukimpa mchaga au mpemba kysimamia biashara yako hatakuangusha. Baada ya miaka michache atakuwa ameanzisha biashara yake na biashara yako iko pale pale. Lakini watu wengine basda ya mwaka atakuwa hana kitu na biashara yako imekufa.

Hivyo ukimpata 'Mchaga' au 'Mpemba' siyo kwa maana ya kabila la hasha bali mtu anayejitambua na mchapakazi hii idea yako itafanya kazi. Lakini walio wengi watakuangusha tu.

Nikweli mfano kuna jamaa mmoja ni mchaga amemwajiri kijana mchaga ni hizi biashara za tigopesa/mpesa/luku sijui max malipo na viuduma vingi vingi tu kwa jinsi huyo mfanyakazi anavyopiga kazi bosi wake kamkodishia makazi kwa hiyo analipiwa kodi na bosi wake, na yeye amefungua duka lake la mobile accessories, kwa jinsi alivyo mchapa kazi bosi wake alimwambia afungue biashara yoyote ila isifanane na ya bosi wake.
 
Kwa upande wangu biashara ndogondogo zinalipa sana.. location na target yako ni jambo la msingi.....

Nakubaliana na wewe,clear vote kwa hili.
Mleta mada inaonekana ulikuwa na matarajio makubwa sana bila kujipanga namna ya kukabiliana na changamoto.
Mke tu anachangamoto zaidi ya biashara na mtu unapambana na miaka inaenda na watoto haooo

Ningeomba nikujibu kama ulivyoweka

1. Ni vigumu kupata watumishi waaminifu.Amini usiamini TZ kila mtu ni fisadi. Watu ni wezi kuliko unavyoweza kuamini. Kama haupo kusimamia mwenyewe shughuli za kila siku basi biashara ndogo ndogo huwezi kufanya.
Usilaumu watu wote kuhusu suala la uaminifu.
Mungu humlipa kila mtu hapa hapa duniani na pia mbele ya safari.
Kwanza jipime wewe je nimuaminifu?
Na kama uliwahi kufanya tukio la kufanya kutokuaminika basi ujue mungu atakulipa kwa style kama hiyo.
Hii ni sawa na kwenye maandiko kwa sie waislam:-
Kwamba kama wewe umezini na mtu wa mtu,basi jua mungu atakulipa hapa hapa na kukuonyesha ubaya wa tukio hilo,na wewe utaziniwa mwanao,mkeo/mmeo,dada yako/kaka yako,wakikosa hao basi hata mama yako au baba yako.

Na ukiweka dhana ya kutoamini kila mtu basi jua ume limit wigo wako kimaisha.

Hii inategema na jinsi gani unaweza kukaa na staffs wako na kuwapa maelekezo na pia kufanya kama sehem ya familia,na sio ubwana na utwana,na pia malipo yaendani na kipato chako na sio kujiangalia wewe tu na familia yako.
Muajiri mzuri ni yule anaeona mfanyakazi wake anapiga hatua kwa kile anachomlipa na motisha nyingine.
Mfano ni mie,niliajiri Driver wa kuendesha Carry na ilikuwa pale Tabata na alikuwa muaminifu sana na kama ndugu,nilikaa nae muda wa mwaka na,lakini ilitokea nafasi ya ubalozini ya udereva na kwa jinsi nilivyoona kwamba ni mstaarabu sana kwa akipindi chote,basi ikabidi nimuagize aende kwa mtu na kwa bahati nzuri akafanikiwa.Na asante yake yeye pia alinitafutia driver of the same type na ndio anafanyakazi hadi sasa na sie tunaendelea kutembeleana kama family na kipindi cha likizo anaomba gari anapiga day worker.
Tatizo la waajiri wengi,suala la mafanikio kwa mfanyakazi wako unaona kama unaibiwa,hujui kuumwa,hujui msiba.
Ujue kwamba mafanikio ya unaemuajiri ndio yanampa tija ya kufanyakazi bila msongo mkubwa wa mawazo,na ndio maana baadhi ya makampuni ya kigeni yanatoa nyumba na usafiri na pesa ya dharura ili ufanye kazi yao kwa utulivu.
Sasa kwenye biashara unayosema,inategema udhaifu wako wa kukimbia changamoto upoje.Kuna mtu anaibiwa kama ......?mbona bado hao hao anawaongeza bonuses kibao,maana wanafikia malengo yake,(sina nia mbaya Mods)

2. Kodi ya pango ya frame ni unrealistic. Kodi ya frame nyingi ni kubwa kuliko unavyoweza kuzalisha. Mwisho wa siki unamfanyia biashara mwenye frame.

Ndio maana inasemwa kwamba kama unaweza chukua huwezi acha.

Kuna tofauti ya kufanya biashara Tandale kwenye kodi za elfu 20,000 - 50,000 na kufanya kazi Kariakoo kwenye kodi hadi milioni mbili.
Sasa utaamua biashara hiyo uipeleke huko au kule.
Na ukubwa wa kodi watu bado hawaachii Frames.Tambua kwamba aliejenga nyumba na yeye amewekeza mamilioni ya pesa na pia Nyumba na frames ni biashara kubwa na ya matajiri sana kwa nchi za ulaya.Sasa imeanza kuhamia kwetu ili tuchangamke.
Wewe jiulize katika frame hizo unazosema bei kubwa kuliko unavyozalisha,mbona wenzio wamekomaa na wapo uliowakuta wanaendelea.
Muhim ni kuijua biashara na kufanya kwa moyo wako bila kuiga kwa kuona fulani anafanya anapata sana wakati hujui changamoto anazokabiliana nazo.Kuna mtu anaweza kukuambia changamoo za biashara zake wewe mwenyewe ukakimbia.
Maana biashara unazofanya wewe wapo watu umewakuta wanafanya na wanaendelea na wengine wanafungua upya.Sasa jiulize wale wamewezaje kuvumilia kuliko wewe ulieshindwa.
Unapoweka profit marging ya faida ya 20,000 -50,000 kwa siku pia ujue kuweka loss ambayo baadhi ya wakati inaweza kula hadi mtaji mzima na kuanza katika negative zero.

Wale waliounguliwa Mabanda na mali zao Mjini,walipoteza mtaji mzima,lakini siku ya pili wamerejesha mabanda mapyaaa utafirikia hakuna tukio.
Hofu yangu kwako ni kwamba akili umeweka uchawi na kukariri uchawi kuliko kupanga plan nzuri ya biashara.

3. Uwezo wa kununua wa wa TZ walio wengi uko chini sana. Wengi wanapenda vitu vya bei rahisi bila kujali ubora. Ndo maana soko la vitu vya kichina vina shamiri. Wako wachache wanaojali ubora lakini ni wachache sana.

Hapa ndio nahisi kwamba ulivamia biashara kwa kuiga.

Hii hadi ulaya ipo hivyo,na ndio nchi zenye kipato kikubwa.
Huo ni mgawanyiko wa aina ya wateja,na ndio maana kuna migahawa kama Mc Donald nk ambayo kama unapesa za upatu huli.Na wakati huo huo ipo ya bei ya kawaida sana tu na watu wanapeta.
Pia tambua kwamba kuwa ghali sio kwamba ndio kuwa bora.
Watanzania ni wanunuaji wazuri sana tu kama umejipanga.Mfano mdogo kabla ya safisha jiji,kuna mtu unakuta anakibanda chenye ukubwa wa mita mbili,lakini anakuambia anaingiza elfu hamsini na zaidi kwa siku.
Sasa huyo ni mjanja anajua target zake,na pia anapambana na chamoto zake.
Mamalishe wale unaowaona,sie tuliojenga Chanika ndio tunawajua,unakuta mamalishe anashusha nyumba chanika kwa kuuza chakula tu,na mtaji wake hauzidi laki moja.Lakini anajua namna na nidhamu ya kupanga matumizi na changamoto zake.
Biashara ni akili na namna unavyojipanga na kupambana,hakuna maisha lele mama.
Maisha magum ni yale walioishi mitume na manabii wakati huo sio leo tumerahishiwa kila kitu halafu tunashindwa kupambana na changamoto.
Usiweke sehem mtaji kwa kukariri mafanikio makubwa na pesa kurudi kwa haraka kama unavyotaka.Siku zote ipange biashara kama unavyotaka wewe ila usitegemee returns zake zitakuja kama unavyotaka wewe.Ipe biashara Grace Period kulingana na nature yake.

4. Ulozi umetawala katika biashara ndogondogo, kama siyi mwenzao utapigwa vita kila kona.
Hii inaonyesha ulivyombali na nyumba za ibada,na hata ukienda basi unakuwa na nia nyingine na sio mapenzi ya dhati kwa mangu kama njia na ngao yako.
Fuata maandiko na ndani yake kuna njia,maana hata mungu anajua uchawi upo ila hautamduru yule anaemuanini na kufuata maagizo na njia zake,na hata kama akipitiwa na upepo wa uchawi basi atampa njia na kumponya kama upendo wake kwa mja wake alienyoshea na anaeonyesha mapenzi ya dhati kwake na sio mapenzi ya msimu.

Na ukiwa na tabia ya kuamini haya mambo ya kichawi wakati wewe unae Mungu aliehai na anakupa njia ya kumuomba na kupita ili matatizo yako yaishe kwa mamlaka alienayo,hapo unaweza kukwama.
Utakuwa kila kitu hata kile ambacho mungu ana kupa kama mtihani kukupima imani yako kwake basi wewe utasema umerogwa

Mungu ndio njia,kote huko tunakopita tunapelekwa na mambo ya kidunia tu.
 
Back
Top Bottom