Biashara mikoani zitakufa, Dar peke yake ndiyo itabaki ikifanya biashara

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,302
12,851
Mambo mawili yanaua biashara mikoani na kukuz biashara Dar.

1. Mitandao ya kijamii.
2. Urahisishaji wa kusafirisha bidhaa.

1. Mitandao ya kijamii imerahisisha sana mawasiliano ya muuzaji na mteja Imerahisisha sana namna ya kutangaza biashara. Mteja anaweza kuona biashara maduka mbalimbali na akafananisha bei kwenye mtandao tu. Anafanya window shopping akiwa katulia hapohapo alipo.

Sasa mara nyingi mtu anapotaka bidhaa ya pesa nyingi kama TV, music system nk, anafanya sana utafiti. Hapo akiingia mitandaoni atakuta maduka ya Dar yamejaa tele. Maduka mengi yanauza hizo bidhaa wakati mkoani unakuta duka moja tu.

Tena unakuta watu wa Dar wanaelewa teknolojia mpya vizuri tofauti na mkoani. Na kwa sababu maduka haya ni makubwa, yanakuwa yanauza bei poa. Mitandao imerahisisha sana window shopping. Mtu hata akitaka suti, viatu na vitu vingine kama hivyo anaingia mtandaoni na kuagiza.

2. Usafirishaji
Bei za usafirishaji na uaminifu vimekua sana. Mtu akinunua kitu Dar na kusafirisha bado bei inakuwa chini kuliko kununua kitu hichohicho mkoani. Na kawaida kinachukua siku moja au mbili max kufika. Tulipofikia inawezekana kuna maduka yana wateja wengi wa rejareja kutoka mikoani kuliko wa Dar hapohapo.

Tunakoenda maduka ya mikoani yatabaki kuuza vitu vidogovidogo, nyanya, vitunguu, simu jinga na vile ambavyo ni ngumu kusafirisha.

Nini kifanyike kuokoa biashara za mikoani zinazodorora kila siku?
 
Kikubwa hili ni janga la taifa hapo baadae na hatutoweza kukua kiuchumi km nchi sehemu ya mzunguko wa fedha ni moja.

Ndiomana mwendazake alijaribu kutengeneza miundombinu na sera yake ya viwanda lengo ilikuwa n kuepuka maswala km haya.

Hivyo kama uongozi ulio madarakani usipochukua uamuzi mgumu kunusuru hali hii ni ngumu kuweza kuweka mikakati km mtu binafsi.

Kwa kuwa unaweza agiza mzigo kutoka dar lkn miundombinu mibovu inakufanya gharama zinakuwa kubwa mpaka mzigo unakufikia.

Na wewe hutoweza kuuza kwa bei ambayo ipo lazima uuze bei itakayorudisha gharama zako soni changamoto ambayo ni fursa kwa serikali
 
Back
Top Bottom