Biashara kufanyika ndani ya Barabara yenye msongamano wa magari na Watu Gongolamboto, TANROADS na Manispaa ya Ilala mkoa wapi?

Biashara kufanyika ndani ya Barabara yenye msongamano wa magari na Watu Gongolamboto, TANROADS na Manispaa ya Ilala mkoa wapi?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
photo_2026-02-04_09-24-37.jpg
Baada ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi kukamilika maeneo ya Gongolamboto, wafanyabiashara ndogo yaani Machinga sasa wameamua kupanga biashara zao hadi katikati ya barabara, matokeo yake sasa kuna foleni kubwa nyakati za asubuhi na jioni.

Dalili ya kuongezeka kwa wafanyabiashara katika eneo hilo imekuwepo kabla hata ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi, hakuna hatua zilizochukuliwa, sasa barabara imekamilika, hakuna hatua zinazochukuliwa.

Wafanyabiashara wamefurika kuanzia Kituo Kipya kwenye eneo la kugeuzia magari, kwenda mpaka barabara ya kuingia Kampala International University. Unaweza kuwahi huko ulikotoka, lakini ukifika Gongolamboto unaweza kutumia hata saa nzima kupita kama una gari.

Kinachosaidia kwa sasa ni kwa sababu mabasi ya mwendokasi hayajaja, lakini kama yatakuja, maana magari ya kawaida hayataruhusiwa kupita kwenye njia zake.

Tunajua Gombolamboto hakuna soko kubwa la kuwachukua hao Wamachinga, lakini TANROADS wanapaswa kulinda eneo lao la barabara litumike kama lilivyokusudiwa.

Manispaa ya Ilala pia wanawajibu wa kuwapanga wafanyabiashara hao, kama wameshindwa kuwajengea soko. Haiwezekani tukaishi kama nchi haina Sheria.
photo_2026-02-04_09-24-36 (2).jpg

photo_2026-02-04_09-24-36.jpg
 
msilete ukuda kwa wapiga kura wetu

japo tutalitizama
 
Dah rangi nyeusi hizi. Same thing ipo Mbagala aisee. Foleni imekua maradufu.

Machinga, Bajaji na Bodaboda wanajiachia sana ova wako juu ya sheria.

Kimara inaenda kushuhudia ongezeko kubwa sana la machinga pembeni ya barabara. Wameanza jana nimeona meza kadhaa kituo kimojawapo.
 
Hiyo yote Tisa, kumi ni huku mbagala ...machinga wamejenga kabisa vibanda ndani ya barabara kuanzia zakheim Hadi rangi tatu na hakuna la kuwafanya, serikali wanalea UJINGA na mwisho wa siku wanashindwa kujitibu

Nchi ya kifala kama hivi imeandaa afcon hiii ni zaidi ya kituko
 
Back
Top Bottom