Biashara katika Siasa na ajira ya Serikali katika Siasa

Biashara katika Siasa na ajira ya Serikali katika Siasa

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,753
Reaction score
4,866
Nimesikiliza kilio cha waajiliwa wa serikali walioonesha niya ya kutaka kugombea nafasi ya Ubunge baada ya kujikuta wanakatiwa mshahara wa mwezi July. Serikali iko sahihi maana kuna mwongozo wa aina hiyo. Tatizo ni kwa nini serikali iliweka mwongozo wa kibaguzi aina hiyo?

Yaonekana serikali ilikuwa inajaribu kuzuia waajiliwa wake wasiingie ktk siasa, kwa uchoyo wa watu fulani au kwa kutojua umuhimu wa watumishi hawa. Ni kama vile Waingereza zile enzi za akina Nyerere, kwa kuwalazimisha akina Nyerere kuacha kazi, maana hawakupenda kutoa Uhuru wa Tanaganyika.

Mwongozo kama huu kwa miaka hii ni wa kizembe. Wengi wanajidai kutetea eti ni kukwepa conflicts of interest, Hapana! Mbona wafanyabiashara wanaingia ktk siasa na bado wanaendelea na biashara zao? Tena wanazitumia kufanikisha nafasi za kisiasa?

Kuna watu wanamiliki mabasi na wanayatumia kutoa huduma kwa wapiga kura kwa mtindo ambao unaashilia ushawishi wa kisiasa. Wengine wanakuwa Bungeni na kuwekwa kwenye kamati za viwanda na biashara wakati wanamiliki viwanda na biashara. Je, hiyo siyo conflicts of interest

Tusiweke uwigo kuzuiya waajiliwa wa serikali kuingia ktk siasa. Tuache uchoyo.
 
Mtumish wa serikali ukishajiingiza kwenye siasa.

Unaenda kuigawa jamii katika utoaji wako wa huduma.

Bila shaka Kuna watu utawabagua kwa itikadi za KISIASA Kama wanasiasa wengine.

Ni Bora uchague TU Mona, kusuka au kunyoa
 
Back
Top Bottom