Biashara hizi 15 zitakutoa 2021

Biashara hizi 15 zitakutoa 2021

Wakuu, ngoja nianze kutiririka bila kupoteza muda.

1 • Digital marketing agency.

There so much money to be made in this area.

Kwa ufupi ni business itakayofanya vizuri kwa miaka nyingi sana sana kwasababu siku zote wamiliki wa biashara wanatafuta watu waliobobea kuwasaidia kupata wateja wa bidhaa au huduma wanazouza.

Sasa kama wewe unauwezo wakuchanga karata zako vizuri na kuanzisha digital marketing agency utakuwa vizuri sana 2021.

2 • Kumiliki Online Store inayouza bidhaa ndani na nnje ya nchi.

Sababu hapa ni kuimarika kwa mifumo ya malipo ya kimtandao. Kwa mfano sasa hivi hata usipokuwa na bank account unaweza kutengeneza virtual bank account kwa kutumia SIM card yako ya Vodacom, Tigo au Airtel. Ukiwa na hii vurtual card utaweza kuweka pesa na kununua chochote unachotaka mtandaoni.

Sasa tunapoelekea watanzania nao watazoea haya. Pesa nyingi itamiminika hapa. I’m telling you.

3 • Tourism

Watanzania sisi nchi yetu imejaliwa tourists attractions nyingi. Kuanzia utamaduni wa watu wetu hadi mbuga zetu za wanyama, mito, bahari, misitu na maziwa.

Kwasababu corona inaisha hiyo maana yake mwakani tourism inaenda kusimama tena.

Muhimu tusifanye tourism kimazoea.

Wiki iliyopita nilienda camping trip kuona indigenous bribes lake eyasi. Nilikuwa na wageni wangu toka United States. Hii trip ilikuwa nzuri sanaaaaa. Wageni wali rate *5. Na nilichofanya ni kwanza kuifanya trip hii iwe memorable kwao. Kwamba naprovide good service zaidi na walivyotarajia.

Pesa ipo sana kwenye tourism tukizidi kuwa wabunifu. Kwahiyo ukiwa na pesa na unaelewa unachofanya unaweza wekeza hapa.

4 • Restaurant yakuuza healthy food kwenye mji mkubwa, Arusha, Dar, Mwanza, etc.

Wakuu, sasa hivi watu wangi wanapendelea healthy food. Binafsi mimi ni vegan for many many years. Maana yake situmii product yoyote inayotokana na mnyama.

Sasa nilichoona watu wengi wanahamia huku. Ukiweza kuwekeza ukafungua modern restaurant kwenye mji mkubwa kama hapa Arusha na unaandaa vyakula vitamu tena heathy? Trust me utapiga sana pesa hapa. Ukiwa Arusha mimi nitakuwa mteja wako nambari one.

5 • Real Estate

Kwa mfano hapa Arusha real estate (viwanja, nyumba za kunua/kupangisha) bei inakwenda juu kila mwezi. Hapa unaweza anza taratibu kama agent baadaye ukipata pesa zaidi unaanza na wewe kununua real estate.

6 • Affiliate Marketing

Covid 19 imechangia pakubwa kubadili tabia za watu wanaonunua mtandaoni.

Katika kipindi hiki cha covid 19 watu wengi wamekuwa tayari au niseme wamekuwa comfortable kununua online bila woga.

Sasa hapa kuna opportunity.

Na ndiyo hii affiliate marketing.

Kwa wasiofahamu affiliate marketing ni biashara ya kupromote bidhaa za wengine mtandaoni na wewe kulipwa commission kwa kila mtaja atakaye nunua kupitia wewe.

Kwa kawaida kabla hujaanza affiliate marketing business inabidi kwanza ufanye mawasiliano/application na mzalishaji wa bidhaa unayotaka kumsaidia ku-promote ili ukiuza ulipwe promotion. Sasa kwasababu hii bisiness utakuwa unafanyia online basi utapatiwa special link inayokutumblisha ni wewe ndiye umemleta mtaja kila mara mteja atakapo click hiyo link unayotumia kupromote bidhaa husika.

Kwa hii business model inawezekana sana tu Tz na kwa mwaka 2021 watu watakaokuwa serious na hii business watatengeneza pesa.

Lakini niseme hapa lazima ujipange.

Unahitaji uwe na review website ambayo affiliate marketer wa kawaida itamchukua miaka mingi kufanya unachofanya.

Hii si ku-copy na ku-paste links kwenye groups za Facebook na Whatsapp. Hizo ni mambo za watoto.

Affiliate Marketing ni big money industry. Na inafanyika kwa umakini wa hali ya juu.

7 • Online Business Consulting

Hapa napo kuna pesa.

Watu wengi sana sana wanatafuta namna watakavyosaidiwa kuanzisha au kukuza Online Business. Sasa ukiwa vizuri hapa pesa zote zitakuja kwako.

8 • Fixer

Wakuu, mwaka 2021 watu wengi watapitia misukosuko kama inavyokuwa miaka yote. Sasa hapa kama wewe ni mtu wakuweza kutatua changamoto za watu bila kujali ni zakibinafsi basi nakwambia utatengeneza sana pesa.

Mbinu hapa ni kuwa na connection na watu au familia zenye pesa mjini kwako. Itabidi ujiweke kuwa wewe ni mtu unayeweza kufanikisha lolote wanalohitaji.

Unajua watu wengi wenye pesa wapo na mambo mengi yakufanikishiwa. Kuanzia halali au haramu. Uchaguzi ni wako.

9 • Kilimo cha mbogamboga bila kutumia dawa zenye sumu.

Zipo high end hotels pia restaurants zinazohitaji mbogamboga zisizotiwa dawa zenye sumu.

Sasa hapa kama utakuwa vizuri ukafanya research ukaingia mkataba waku-supply mbogamboga kwenye hotels hizi nakwambia utatengeneza pesa nzuri sana bila kuwaza. Kama nilivyosema fanya research kwanza.

10 • Plambing services

Wakuu hii business yakutengeneza au kuweka sawa miundombinu ya maji au waliwato majumbani kwa watu ni Business nzuri sana.

Lakini inabidi uifanye kisasa na uwe na vifaa na vijana wanaofahamu kufanya hii kazi.

Kipindi hiki waTz wengi wanaishi kwenye nyumba au apartment zenye miundombinu hii sasa ikiharibika hawafahamu nani hasa atawatengenezea.

Mfano leo heater bafuni kwangu imegoma kufanya kazi imebidi nimpigie jamaa ana kampuni yake hapa Arusha ametuma kijana haraka amefanya kazi na nimelipa. Sasa kwa mji mkubwa kama Arusha na ukijiweka vizuri na kutangaza kampuni yako utakuwa vizuri sana.

11 • Online tutoring

Je, una Skills yoyote unayodhani unaweza kumfundisha mtu mwingine? Binafsi ninaweza kukusaidia jinsi yakufanikisha hili kwamaana ya kufahamu namna gani unaweza kuwa na Online classes na ukafundisha kwa kiwango cha juu kabisa ukitumia teknolojia.

Hii ni opportunity nzuri sana kwasababu mwaka 2021 watanzania wengi watakuwa na njaa ya maarifa kwasababu watu wanazidi kufahamu Ukiwa na rights skills zinazohitajika hasahasa mtandaoni basi unaweza kutengeneza pesa. Sasa wewe kama unafahamu let say designing, photography, coding, copy writing, cooking, kwanini usitumie hizi Skills kufundisha wengine na kutengeneza more money?

12 • Biashara ya vifaa vya ujenzi.

Miji mingi ya Tanzania inakuwa kwa haraka. Kwa uhakika kabisa takwimu zionaonyesha sekta ya ujenzi itaendele kufanya vizuri 2021. Sasa kama unamtaji wakutosha ukianzisha Store yakuuza vifaa vya ujenzi lazima utapiga pesa. Kama kawada fanya kwanza research kabla hujaweka pesa zako. Inabidi ufahamu kasi ya ujenzi katika mji wako na wapi uweke store hapo mjini.

13 • Kampuni ya ujenzi.

Kama wewe upo vizuri kwenye mambo ya ujenzi au unauwezo wakuwaleta pamoja mafundi ujenzi wenye weledi mzuri pia una vifaa basi utaweza kupata deals nyingi zakujenga nyumba za watu au project fulani za mashirika hapa Tz. Inategemea uwezo na mtaji ulio nao, hatahivyo.

14 • Kuaandaa Matamasha ya Burudani.

Wait,

Burudani? Really?

Yes, hii kitu ukifanya kwa ubunifu inakutoa 2021.

Mwezi wa 9 nilikutana na dada mmoja yeye anaandaa matamasha kubwa kwaajili ya kukutanisha watu wapate good time. Kwa huku kaskazini analenga kipindi cha December watu wanakuja mapumziko sasa yeye anatumia Hii opportunity kuandaa matamasha na niseme tu watu wana-respond vizuri sana.

Labda nikupe mfano unaofahamika na watu wengi. Matamasha ya burudani yanayoandaliwa na Clouds media group. Haya matamasha yanatengeneza pesa nyingi sana. Lakini wewe kwasababu unaanza huitaji kuandaa kwa ukubwa wa Clouds Media Group. Unaweza ukaanza na mkoani kwako. Hapa inabidi ufanye kazi kwa karibu na kampuni za vinjwaji kama vile makampuni ya vijwaji baridi au wazalishaji wa pombe.

Haya makampuni siku zote yanakaribisha wajasiriamali wanaoweza kufanya hizi mambo. Makampuni haya yanapata faida pia kwasababu katika makubaliano lazima wao ndiyo watakuwa wauzaji wa vinjwaji katika tamasha unaloandaa.

Sasa mtu wangu hapo unaona, kama upo na kichwa kizuri, unaweza ku-organize watu kufanikisha hili basi 2021 utakuwa vizuri.

15 • Sex Toys kwa wanawake 🧐

Wakuu hii business sijafahamu kama inaruhusiwa hapa Tanzania ama vipi.

Kitu nilichogundua wakina dada wengi sana sasa hivi wapo depressed.

Wengi wao hawapendi tena wanaume au wakiwa nao basi wanakuwa na mambo yao mengine yakuwasaidia kufika kilele cha mmlima Kilimanjaro.

Niliwahi kusikia kwenye idhaa ya kiswahili BBC, huko Tabora baadhi ya wanawake wanatumia ugoro kufika kileleni. Na walikuwa wanahojiwa wanasema wakiwa na wanaume wao hawajisikii kabisa kwahiyo bora watumie ugoro tu.

Nilivyosikia haya niliwaza mambo mengi sana. Sasa kwakuwa mimi ni mjasiriamali nikafanya uchunguzi nikatambua japo hawa waliohojiwa ni wachache tu, lakini hii ni issue kubwa. Si wanawake wa Tabora pekee. Wakina dada wengi tu wenye pesa mijini nao kuna namna yao wanatumia kwasababu hawataki tena wanaume.

Sasa mtu wangu ukiwa na Store inauza sex toys tegemea kupiga pesa nyingi sana. Na iwapo utaweza kuifanya hii Business kwa kuzingatia huduma nzuri na bidhaa bora basi pesa zitakuwa upande wako.

Ok, kwa leo niishie hapa.

Tuonane wakati mwingine

Tuwasiliane makingmoneyonlinetz@gmail.com

Cheers 🥂
Hiyo na. 15 mbaya, tumche mwenyezi Mungu. Mambo ya wazungu waachie wazungu ambao kwao hata kutembea naked ni sawa.
 
mkuu namba nane hapo umetaja fixer, nielezee kwa kinaganaga nipate mwanga nifanye hicho kitu.

pia naomba kujua hapo kwenye tourism naanzaje!?.. yaaan kuna costs za kuanza ?.

mimi ni mgeni katika ulimwengu wa ujasiriamali
Mkuu, kuwa fixer maana yake unawasaidia watu wenye pesa kufanikisha michongo yao. Kwa mfano hapa town Arusha kuna watu wengi sana kuanzia wageni toka nje au hata wazawa tu wenye pesa wanahitaji uwasaidie labda ku-solve matatizo yao ya kibinafsi kwa mfano kupata nyaraka fulani au labda masuala ya kimahusiano nk.

Binafsi mimi siyo fixer lakini nafahamu watu wengi kwenye miji mikubwa wanafanya hizi mambo. Kuwa fixer haimaanishi unajihusisha na mambo maovu...nop, ni vile tu watu wengi wenye pesa wanamatatizo mengi sana mazito na hawawezi kufanya wenyewe sasa wewe ukiweza kuwa karibu nao na unauwezo wakusolve hayo matatizo basi wewe tayari ni fixer. Ukitaka kupata deals nyingi za namna hii fahamiana na matajiri wanasiasa.
 
Hao marafiki wa ughaibuni nawapataje?
Mkuu njia rahisi yakupata marafiki inabidi kwanza uwe authentic, kwa maana ya kwamba kweli unataka kujenga urafiki.

Ukifanya mambo kwa hila watu watagundua na watakuepuka. Hasahasa wageni toka nnje. Binafsi nimetengeneza marakifi wa dhati kabisa kote duniani.

Njia nayotumia ni Couch Surfing (kuna uzi nimeandika kuhusu hii kitu), AirBnB (nipo na apartments ninapokea wageni hapa Arusha), Instagram lakini pia hapa Arusha kwenye events za kitalii au kufamiana mtaani tu. Sasa hapa ndiyo mambo yanaanza sasa. Ukiwa na marafiki toka nje na wewe ni smart unaweza kuuza idea na upo genuine basi mtu wangu soon utapiga deals nyingi.

Uaminifu + good personality ndiyo silaha ya kwanza kupata wageni toka nje. Wakati naanza haya mambo ya tourism nilikuwa kwanza kabisa napenda kufanya urafiki na watu wanaotoka nchi za ng'ambo. Nikajiunga Couch Surfing na nikaanza kupokea wageni. Japo wageni wengi wa Couch Surfing ni very cheap lakini mimi sikujali pesa kwasababu mimi ni mtu nayependa good time pia si mtu wa shida ndogo ndogo. Lakini ni kama vile nilikuwa najiwekea hazina. Hii kitu ilinijenga lakini pia ilinisaidia kuwa mvumilivu kwa marafiki zangu. Kwasababu ya uzoefu huu sasa hivi napokea wageni wenye pesa kupitia AirBnB lakini pia word of mouth. Kwamba unakuta mgeni toka US nilifanyanaye kazi sasa akirudi kwao anakuwa anawaambia marafiki wengine kwamba ukienda Tanzania na unataka kuandaliwa experience nzuri iwe kwenda Serengeti, Ngorongoro, Tarangine, nk basi mtafute Global Ciziten. Nmana hii tunazidi kujulikana lakini pia kupata kazi through connection.
 
Mkuu, mimi nina marafiki toka marekani na ulaya. Je ni namna gan naweza organize nao ishu ya utalii ili niweze kupokea wageni na kuwapeleka kwenye vivutio?

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Njia rahisi ni wewe mwenyewe kuonekana unapenda tourism. Na kweli uwe umeanza kufanya kitu kuhusu hili.

Je, umeshawahi kuorganize safari hata ya kwenda na marafiki au familia yako hapa Tanzania?

Kwasababu kama wewe nywenyewe hauna hata picha moja au hauna interest yoyote na mambo ya adventure hiyo itakuwia vigumu sana kuwashawishi. Tuwasiliane.
 
Vipi kama hauishi kwenye tourist centers unawezaje kufanya tourism?
Kwanza kabisa focus kutafuta marafiki genuine. Hapa inakuwa mwanzo mzuri wa wewe kutoa ideas za tourism. Kwa mfano upo Dodoma na una rafiki Sweden na yupo interested na african safari. Sasa hapa unaweza mweleza kuhusu tourists attraction zilizopo Arusha au Zanzibar bila yakufikiria aaaah mimi nakaa Dodoma kwahiyo sitaweza.

Kama akisema yes nataka nitembelee let say Tarangire sasa hapa ni jukumu lako tena kutafuta taarifa namna gani unafanikisha hili kuanzia kurent safari vehicle, kufahamu jinsi yakulipia park fee nk. Siku mgeni wako anakaribia kufika unakuwa tayari upo KIA unamsubiri.

Ukimaliza kazi unarudi zako Dodoma. Huu ni mwanzo, ukianza kupata kazi nginyi sasa hapa unaweza kuhamia kabisa. Mkuu mafanikio yanafuatwa si kuyasubiria. Kwayeyote atakayehitaji Master Class kwaajili ya hii mambo anitafute nitamsaidia bila shaka.
 
Ok, so unaweza ukawa unatangaza hizi atractions online.Hapa namaansha uwe na website na social media accounts
 
Hapo tourism ya ndani, capital inakuaje mkuu!?.
Capital unataka kununua nini?

Tourism ni business unayoweza kuanza hata bila senti tano.

Mtihani wako wa kwanza kabisa ni kupata watu walio tayari kutoa pesa uwapeleke safari. Na kufanikisha hili huitaji pesa yoyote.

Baadaye, hatahivyo, kama mambo yakienda vizuri basi uahitaji pesa labda yakunua safari vehicle, labda camping gear etc. Ila kwa sasa hivi you dont need capital my friend. Tuwasiliane kama unahitaji nikusaidie one on one.
 
Mkuu, kuwa fixer maana yake unawasaidia watu wenye pesa kufanikisha michongo yao. Kwa mfano hapa town Arusha kuna watu wengi sana kuanzia wageni toka nje au hata wazawa tu wenye pesa wanahitaji uwasaidie labda ku-solve matatizo yao ya kibinafsi kwa mfano kupata nyaraka fulani au labda masuala ya kimahusiano nk.

Binafsi mimi siyo fixer lakini nafahamu watu wengi kwenye miji mikubwa wanafanya hizi mambo. Kuwa fixer haimaanishi unajihusisha na mambo maovu...nop, ni vile tu watu wengi wenye pesa wanamatatizo mengi sana mazito na hawawezi kufanya wenyewe sasa wewe ukiweza kuwa karibu nao na unauwezo wakusolve hayo matatizo basi wewe tayari ni fixer. Ukitaka kupata deals nyingi za namna hii fahamiana na matajiri wanasiasa.
Unaweza vip kufahamiana na hao mabwanyenye?
 
naam mkuu nimekuPM.
 
hahaha...!!

hii nimeipenda sana, najiona hii naweza kuifanya.
 
Back
Top Bottom