Biashara hizi 15 zitakutoa 2021

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
767
1,655
Wakuu, ngoja nianze kutiririka bila kupoteza muda.

1 • Digital marketing agency.

There so much money to be made in this area.

Kwa ufupi ni business itakayofanya vizuri kwa miaka nyingi sana sana kwasababu siku zote wamiliki wa biashara wanatafuta watu waliobobea kuwasaidia kupata wateja wa bidhaa au huduma wanazouza.

Sasa kama wewe unauwezo wakuchanga karata zako vizuri na kuanzisha digital marketing agency utakuwa vizuri sana 2021.

2 • Kumiliki Online Store inayouza bidhaa ndani na nnje ya nchi.

Sababu hapa ni kuimarika kwa mifumo ya malipo ya kimtandao. Kwa mfano sasa hivi hata usipokuwa na bank account unaweza kutengeneza virtual bank account kwa kutumia SIM card yako ya Vodacom, Tigo au Airtel. Ukiwa na hii vurtual card utaweza kuweka pesa na kununua chochote unachotaka mtandaoni.

Sasa tunapoelekea watanzania nao watazoea haya. Pesa nyingi itamiminika hapa. I’m telling you.

3 • Tourism

Watanzania sisi nchi yetu imejaliwa tourists attractions nyingi. Kuanzia utamaduni wa watu wetu hadi mbuga zetu za wanyama, mito, bahari, misitu na maziwa.

Kwasababu corona inaisha hiyo maana yake mwakani tourism inaenda kusimama tena.

Muhimu tusifanye tourism kimazoea.

Wiki iliyopita nilienda camping trip kuona indigenous bribes lake eyasi. Nilikuwa na wageni wangu toka United States. Hii trip ilikuwa nzuri sanaaaaa. Wageni wali rate *5. Na nilichofanya ni kwanza kuifanya trip hii iwe memorable kwao. Kwamba naprovide good service zaidi na walivyotarajia.

Pesa ipo sana kwenye tourism tukizidi kuwa wabunifu. Kwahiyo ukiwa na pesa na unaelewa unachofanya unaweza wekeza hapa.

4 • Restaurant yakuuza healthy food kwenye mji mkubwa, Arusha, Dar, Mwanza, etc.

Wakuu, sasa hivi watu wangi wanapendelea healthy food. Binafsi mimi ni vegan for many many years. Maana yake situmii product yoyote inayotokana na mnyama.

Sasa nilichoona watu wengi wanahamia huku. Ukiweza kuwekeza ukafungua modern restaurant kwenye mji mkubwa kama hapa Arusha na unaandaa vyakula vitamu tena heathy? Trust me utapiga sana pesa hapa. Ukiwa Arusha mimi nitakuwa mteja wako nambari one.

5 • Real Estate

Kwa mfano hapa Arusha real estate (viwanja, nyumba za kunua/kupangisha) bei inakwenda juu kila mwezi. Hapa unaweza anza taratibu kama agent baadaye ukipata pesa zaidi unaanza na wewe kununua real estate.

6 • Affiliate Marketing

Covid 19 imechangia pakubwa kubadili tabia za watu wanaonunua mtandaoni.

Katika kipindi hiki cha covid 19 watu wengi wamekuwa tayari au niseme wamekuwa comfortable kununua online bila woga.

Sasa hapa kuna opportunity.

Na ndiyo hii affiliate marketing.

Kwa wasiofahamu affiliate marketing ni biashara ya kupromote bidhaa za wengine mtandaoni na wewe kulipwa commission kwa kila mtaja atakaye nunua kupitia wewe.

Kwa kawaida kabla hujaanza affiliate marketing business inabidi kwanza ufanye mawasiliano/application na mzalishaji wa bidhaa unayotaka kumsaidia ku-promote ili ukiuza ulipwe promotion. Sasa kwasababu hii bisiness utakuwa unafanyia online basi utapatiwa special link inayokutumblisha ni wewe ndiye umemleta mtaja kila mara mteja atakapo click hiyo link unayotumia kupromote bidhaa husika.

Kwa hii business model inawezekana sana tu Tz na kwa mwaka 2021 watu watakaokuwa serious na hii business watatengeneza pesa.

Lakini niseme hapa lazima ujipange.

Unahitaji uwe na review website ambayo affiliate marketer wa kawaida itamchukua miaka mingi kufanya unachofanya.

Hii si ku-copy na ku-paste links kwenye groups za Facebook na Whatsapp. Hizo ni mambo za watoto.

Affiliate Marketing ni big money industry. Na inafanyika kwa umakini wa hali ya juu.

7 • Online Business Consulting

Hapa napo kuna pesa.

Watu wengi sana sana wanatafuta namna watakavyosaidiwa kuanzisha au kukuza Online Business. Sasa ukiwa vizuri hapa pesa zote zitakuja kwako.

8 • Fixer

Wakuu, mwaka 2021 watu wengi watapitia misukosuko kama inavyokuwa miaka yote. Sasa hapa kama wewe ni mtu wakuweza kutatua changamoto za watu bila kujali ni zakibinafsi basi nakwambia utatengeneza sana pesa.

Mbinu hapa ni kuwa na connection na watu au familia zenye pesa mjini kwako. Itabidi ujiweke kuwa wewe ni mtu unayeweza kufanikisha lolote wanalohitaji.

Unajua watu wengi wenye pesa wapo na mambo mengi yakufanikishiwa. Kuanzia halali au haramu. Uchaguzi ni wako.

9 • Kilimo cha mbogamboga bila kutumia dawa zenye sumu.

Zipo high end hotels pia restaurants zinazohitaji mbogamboga zisizotiwa dawa zenye sumu.

Sasa hapa kama utakuwa vizuri ukafanya research ukaingia mkataba waku-supply mbogamboga kwenye hotels hizi nakwambia utatengeneza pesa nzuri sana bila kuwaza. Kama nilivyosema fanya research kwanza.

10 • Plambing services

Wakuu hii business yakutengeneza au kuweka sawa miundombinu ya maji au waliwato majumbani kwa watu ni Business nzuri sana.

Lakini inabidi uifanye kisasa na uwe na vifaa na vijana wanaofahamu kufanya hii kazi.

Kipindi hiki waTz wengi wanaishi kwenye nyumba au apartment zenye miundombinu hii sasa ikiharibika hawafahamu nani hasa atawatengenezea.

Mfano leo heater bafuni kwangu imegoma kufanya kazi imebidi nimpigie jamaa ana kampuni yake hapa Arusha ametuma kijana haraka amefanya kazi na nimelipa. Sasa kwa mji mkubwa kama Arusha na ukijiweka vizuri na kutangaza kampuni yako utakuwa vizuri sana.

11 • Online tutoring

Je, una Skills yoyote unayodhani unaweza kumfundisha mtu mwingine? Binafsi ninaweza kukusaidia jinsi yakufanikisha hili kwamaana ya kufahamu namna gani unaweza kuwa na Online classes na ukafundisha kwa kiwango cha juu kabisa ukitumia teknolojia.

Hii ni opportunity nzuri sana kwasababu mwaka 2021 watanzania wengi watakuwa na njaa ya maarifa kwasababu watu wanazidi kufahamu Ukiwa na rights skills zinazohitajika hasahasa mtandaoni basi unaweza kutengeneza pesa. Sasa wewe kama unafahamu let say designing, photography, coding, copy writing, cooking, kwanini usitumie hizi Skills kufundisha wengine na kutengeneza more money?

12 • Biashara ya vifaa vya ujenzi.

Miji mingi ya Tanzania inakuwa kwa haraka. Kwa uhakika kabisa takwimu zionaonyesha sekta ya ujenzi itaendele kufanya vizuri 2021. Sasa kama unamtaji wakutosha ukianzisha Store yakuuza vifaa vya ujenzi lazima utapiga pesa. Kama kawada fanya kwanza research kabla hujaweka pesa zako. Inabidi ufahamu kasi ya ujenzi katika mji wako na wapi uweke store hapo mjini.

13 • Kampuni ya ujenzi.

Kama wewe upo vizuri kwenye mambo ya ujenzi au unauwezo wakuwaleta pamoja mafundi ujenzi wenye weledi mzuri pia una vifaa basi utaweza kupata deals nyingi zakujenga nyumba za watu au project fulani za mashirika hapa Tz. Inategemea uwezo na mtaji ulio nao, hatahivyo.

14 • Kuaandaa Matamasha ya Burudani.

Wait,

Burudani? Really?

Yes, hii kitu ukifanya kwa ubunifu inakutoa 2021.

Mwezi wa 9 nilikutana na dada mmoja yeye anaandaa matamasha kubwa kwaajili ya kukutanisha watu wapate good time. Kwa huku kaskazini analenga kipindi cha December watu wanakuja mapumziko sasa yeye anatumia Hii opportunity kuandaa matamasha na niseme tu watu wana-respond vizuri sana.

Labda nikupe mfano unaofahamika na watu wengi. Matamasha ya burudani yanayoandaliwa na Clouds media group. Haya matamasha yanatengeneza pesa nyingi sana. Lakini wewe kwasababu unaanza huitaji kuandaa kwa ukubwa wa Clouds Media Group. Unaweza ukaanza na mkoani kwako. Hapa inabidi ufanye kazi kwa karibu na kampuni za vinjwaji kama vile makampuni ya vijwaji baridi au wazalishaji wa pombe.

Haya makampuni siku zote yanakaribisha wajasiriamali wanaoweza kufanya hizi mambo. Makampuni haya yanapata faida pia kwasababu katika makubaliano lazima wao ndiyo watakuwa wauzaji wa vinjwaji katika tamasha unaloandaa.

Sasa mtu wangu hapo unaona, kama upo na kichwa kizuri, unaweza ku-organize watu kufanikisha hili basi 2021 utakuwa vizuri.

Ok, kwa leo niishie hapa.

Tuonane wakati mwingine

Tuwasiliane makingmoneyonlinetz@gmail.com

Cheers 🥂
 
Mkuu hapo kwenye restaurant ndo nina mipango napo ..nataka nifungue ya kuuza breakfast tu kama ya aina hii. Ndio napambana hapa town kupata location kali ..kama unaweza nisaidia pia itakuwa vizuri sana ..je kwa hapa Arusha naweza kutengeneza pesa nzuri sana?
 
Attachments

  • 20201023_203039.jpg
    20201023_203039.jpg
    118.8 KB · Views: 34
Mkuu naomba kupata elimu kuhusu biashara ya utaliii
Njia rahisi ya kujifunza inabidi uanze kwa kufanya.

Tena unatakiwa uanze sasa hivi.

Swahi la kwanza lakujiuliza.

1 . Je, unataka kufanya utalii wa ndani au unataka kufanya tourism kwakupokea wageni toka nje.

Hili swali ni muhimu kwasababu ulishajibu sasa utafahamu utalii upi umechagua kufanya. Hapa A town niliona kuna jamaa yeye anafanya utalii wa ndani na ame-focus wateja wake ni wanafunzi wa vyou. Njia ya kuwapata? Anatumia WhatsApp group. Anapeleka clients wake Magoroto Tanga, Hot Spring Boma Ng'ombe Hai, Oldupai etc. Huu ni mwanzo mzuri sasa hasa kama faida ipo. Sasa wewe unaweza ukaiga huu mfano hapo mjini kwako. Au unaogopa? Unadhani ni kazi ngumu sana?

Binafsi nimeshafanya kitu kinachofanana na hiki. Ila mimi nilikuwa nalenga wanafunzi wa shule za sekondari kipindi cha holidays. And i was only 21. Naomba kuonana na mwalimu mkuu, nahakikisha mimeenda na picha kabisa na documents zote za sehemu ninazolenga kupeleka wanafunzi wa shule yake wakajifunze. Hii ni powerful kwasababu ukitumia mifano dhahiri rahisi watu kukuamini. Hapa nilikuwa mjanja nilihakikisha sehemu zote nazotaka kuwapeleka nipo na taarifa zake bila kusuasua. Trust me, nilikuwa natengeneza faida hadi kufikia Tsh260,000 kwa siku kila wiki. Niliacha hii project baada ya kupata opportunity Yali, mgango wa President Barack Obama wakusaidia vijana wajasiriamali, vijana wanaoendesha not for profit organizations, cbo's, political leaders etc. Mimi nilikuwa semi finalist mdogo kuliko wote. I believe. Lakini sikufanikiwa kwenda Washngton kuonana na President Barack Obama. Na hii ndiyo sababu kuu nilijiunga Yali. Namkubali Obama mbaya.

Ok turudi kwenye swali yako...

Iwapo utaamua kuchagua utali kwa maana ya kuwalenga tourists kutoka nje basi huna budi kujitahidi kwa bidii.

Njia rahisi hapa nikutafuta rafiki wa nje aliye na same interest. Utapiga hatua. Mwenyewe itakuwia vigumu kupata clients wakukulipa pesa. Binafsi natumia njia hii yakufanya partnership. Nipo na watu wafanya nao kazi na kwanamna hii inakuwa rahisi business kuonekana business kweli.

Kila la kheri. Ukiona unahitaji msaada zaidi nitafute.

Cheers
 
nilikuwa
Nina ndugu yangu yupo nje (denmark) amekuwa very interested na hii business lakini ameshindwa kupata mtu makini wa kuingia makubaliano nae kama partnership Ili waweze kuingiza pesa...

Kama hutojali naweza nikaongea nae then nikuunganishe nae Ili kupeana abc za hii biashara.
 
Mkuu namba nane hapo umetaja fixer, nielezee kwa kinaganaga nipate mwanga nifanye hicho kitu.

Pia naomba kujua hapo kwenye tourism naanzaje!?.. yaaan kuna costs za kuanza ?.

Mimi ni mgeni katika ulimwengu wa ujasiriamali
 
Mkuu hapo kwenye restaurant ndo nina mipango napo ..nataka nifungue ya kuuza breakfast tu kama ya aina hii. Ndio napambana hapa town kupata location kali ..kama unaweza nisaidia pia itakuwa vizuri sana ..je kwa hapa Arusha naweza kutengeneza pesa nzuri sana?
Mkuu, kwanza kabisa nikupe big ups. Nadhani inawezekana hii business model. Siwezi sema ndiyo guarantee utafanikiwa kwasababu kuna mambo mengi yanaweza enda mrama kwenye business. Nitumie message mkuu
 
Back
Top Bottom