Biashara haramu kwa miaka mitano mtu anastaafu sawa na Daktari bingwa

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,412
Habari za saa hizi wana jamvi, hongereni wana Dar es Salaam kwa mvua, sasa hamna kisingizio cha kutokupeana.

SIASA: Ukiacha biashara haramu ya madawa ya kulevya, biashara ya Siasa ndiyo inayolipa kuliko zote. Wakati kila uchao maghorofa na biashara mpya zikifunguliwa, siasa ni biashara mpya inayolipa na isiyolipiwa Kodi.

Mke wa Rais Mstafu na Mkurugenzi wa WAMA pamoja Mwalimu Mstaafu wa shule ya Msingi Oysterbay ambaye ni mbunge wa Bunge la JMT amependekeza yeye na wenzie wapewe mafao baada ya waume zao kustaafu maana maisha wanayoishi ni duni sana kulinganisha na waume zao walipokuwa madarakani.

Hii ni baada ya Yeye [huyo Bibi] kuchukua mafao ya ualimu, kula posho za WAMA, kula milioni 15 kwa mwezi za ubunge, Mumewe kupewa lita 70 za mafuta za gari, nyumba masaki, Oysterbay na Msoga ila sasa hivyo havitoshi inabidi waongezewe na mafao.

Pongezi kwa huyu mbunge na Tanganyika haitokusahau, hii inashajihisha wabunge wa Zanzibar wateuliwe nafasi za Bara ili

Mke wa Rais, Waziri mkuu, Katibu mkuu, Mawaziri, wabunge, wakurugenzi, Wakuu wa mikoa na wilaya, Ma RAS na DAS bado wakurugenzi wa Bodi mbalimbali na taasisi za serikali. Wenza wao nao wanakula pension.

Kama hii dhuluma ni kweli imepitishwa na hawa viongozi wetu ambao wote ni waumini wa Imani za dini, zinazojinadi kwamba zinapigania Haki sawa kwa watu wote, kuwaaminisha waumini habari za Mungu muweza wa yote, uwepo wa maisha baada ya kifo na hukumu ya pepo na moto, lakini bado hao viongozi wa kisiasa wanafanya Dhambi hii kisha viongozi wa Dini hawakemei kwa maneno wala kupinga kwa vitendo, basi maana yake wote hawaamini uwepo wala uwezo wa Mungu mkuu anaependa Haki, na hata habari za maisha baada ya kifo pamwe na hukumu za mema na mabaya kwao sio za kweli.

Kama viongozi wangekua wanaamini mafundisho ya dini zetu za majahazi, bila shaka dhuluma za wazi kwa wananchi wao masikini zisingefanyika, ingawa inawezekana pia wanatekeleza baadhi ya maagizo ya Imani hizo za wakoloni zinazohalalisha dhuluma kwa wanyonge kama ile mistari ya Biblia inqyosema kuwa "mwenye Tisa ataongezewa sita,nyingine huku yule mwenye moja atapokwa hata ile moja aliyonayo".

Sasa hata kama akili zetu zipo busy na Daby ya Kariakoo, lakini mara chache tujaribu kuziweka akili zetu kwenye mambo ya maana kwajili ya mustakabali wa maisha yetu, watoto wetu na hatma ya Amani na umoja wa taifa letu, kwa kuzingatia kuwa, Amani tuliyonayo ni matunda katika mti wa Haki, sasa tutavunaje matunda ya Amani huko mbele kama tutaendelea kuukata mti wa Haki unaozaa Amani kirahisi kama hivi?

Kwamba wabunge wetu wanatuaminisha kuwa hao wenza wa viongozi wetu matajiri ndio wanashida sana za kimaisha kuliko watumishi wengine au wananchi wengi wa kipato cha chini kiasi cha kuwapatia pesa hizo ambazo wenza wao wanapata zaidi wakiwa kazini na hata baada ya kustaafu? Haki iko Wapi?

Heri mimi sio muumini wa Dini za wakoloni, naamini Mungu wangu aliyejuu Mungu JUA
🌞
na watoto wangu nimewmbia kwamba, siku nikifa nichomwe Moto, na msiba wangu usihusishe Dini yoyote ya wakoloni, huku watu wote wakikaribishwa kuongelea maswala ya UPENDO tu ambayo ndio dini ya kweli.

MY TAKE : Mwenezi wetu mpya wa chama aandae Maandamano makubwa kumpokea mbunge shujaa aliyependekeza hii sheria na hatimaye kupitishwa.
 
Keki yenyewe ya taifa ndogo hata tukisema tugawane hatutardhika acha wao wale kwa niaba yetu. Sisi hatuna njaa kiviiile. Wao wana uhitaji zaidi.
Sisi tunaanza kupokea khanga na kofia na wao tunawaongezea mafao.
 
kiukweli siasa ya bongo inalipa, na hawaoni haya kutunga sheria za kujipatia maokoto
 
Inatia hasira sana,,, na ina huzunisha sana.

Mwalimu wa shule ya msingi aliyefundisha miaka 30 kwa mshahara wa 490K tena kwa madeni kibao...

W
Hawa wauaji wakaamua kumpa KIKOKOTOO, KWA KWELI HII NCHI SIASA NDIO KAZI BORA KULIKO ZOTE....
 
Habari za saa hizi wana jamvi, hongereni wana Dar es Salaam kwa mvua, sasa hamna kisingizio cha kutokupeana.

SIASA: Ukiacha biashara haramu ya madawa ya kulevya, biashara ya Siasa ndiyo inayolipa kuliko zote. Wakati kila uchao maghorofa na biashara mpya zikifunguliwa, siasa imekuwa biashara mpya inayolipa na isiyolipiwa Kodi.

Mke wa Rais Mstafu na Mkurugenzi wa WAMA pamoja Mwalimu Mstaafu wa shule ya Msingi Oysterbay ambaye ni mbunge wa Bunge la JMT amependekeza yeye na wenzie wapewe mafao baada ya waume zao kustaafu maana maisha wanayoishi ni duni sana kulinganisha na waume zao walipokuwa madarakani.

Hii ni baada ya Yeye [huyo Bibi] kuchukua mafao ya ualimu, kula posho za WAMA, kula milioni 15 kwa mwezi za ubunge, Mumewe kupewa lita 70 za mafuta za gari, nyumba masaki, Oysterbay na Msoga ila sasa hivyo havitoshi inabidi waongezewe na mafao.

Pongezi kwa huyu mbunge na Tanganyika haitokusahau, hii inashajihisha wabunge wa Zanzibar wateuliwe nafasi za Bara ili

Mke wa Rais, Waziri mkuu, Katibu mkuu, Mawaziri, wabunge, wakurugenzi, Wakuu wa mikoa na wilaya, Ma RAS na DAS bado wakurugenzi wa Bodi mbalimbali na taasisi za serikali. Wenza wao nao wanakula pension.

Kama hii dhuluma ni kweli imepitishwa na hawa viongozi wetu ambao wote ni waumini wa Imani za dini, zinazojinadi kwamba zinapigania Haki sawa kwa watu wote, kuwaaminisha waumini habari za Mungu muweza wa yote, uwepo wa maisha baada ya kifo na hukumu ya pepo na moto, lakini bado hao viongozi wa kisiasa wanafanya Dhambi hii kisha viongozi wa Dini hawakemei kwa maneno wala kupinga kwa vitendo, basi maana yake wote hawaamini uwepo wala uwezo wa Mungu mkuu anaependa Haki, na hata habari za maisha baada ya kifo pamwe na hukumu za mema na mabaya kwao sio za kweli.

Kama viongozi wangekua wanaamini mafundisho ya dini zetu za majahazi, bila shaka dhuluma za wazi kwa wananchi wao masikini zisingefanyika, ingawa inawezekana pia wanatekeleza baadhi ya maagizo ya Imani hizo za wakoloni zinazohalalisha dhuluma kwa wanyonge kama ile mistari ya Biblia inqyosema kuwa "mwenye Tisa ataongezewa sita,nyingine huku yule mwenye moja atapokwa hata ile moja aliyonayo".

Sasa hata kama akili zetu zipo busy na Daby ya Kariakoo, lakini mara chache tujaribu kuziweka akili zetu kwenye mambo ya maana kwajili ya mustakabali wa maisha yetu, watoto wetu na hatma ya Amani na umoja wa taifa letu, kwa kuzingatia kuwa, Amani tuliyonayo ni matunda katika mti wa Haki, sasa tutavunaje matunda ya Amani huko mbele kama tutaendelea kuukata mti wa Haki unaozaa Amani kirahisi kama hivi?

Kwamba wabunge wetu wanatuaminisha kuwa hao wenza wa viongozi wetu matajiri ndio wanashida sana za kimaisha kuliko watumishi wengine au wananchi wengi wa kipato cha chini kiasi cha kuwapatia pesa hizo ambazo wenza wao wanapata zaidi wakiwa kazini na hata baada ya kustaafu? Haki iko Wapi?

Heri mimi sio muumini wa Dini za wakoloni, naamini Mungu wangu aliyejuu Mungu JUA
" data-src="/proxy.php?image=https%3A%2F%2Fstatic.xx.fbcdn.net%2Fimages%2Femoji.php%2Fv9%2Ft5f%2F1%2F16%2F1f31e.png&hash=ecba5b268897e1d40553617d97fb06b6" data-lb-sidebar-href="" data-lb-caption-extra-html="" data-single-image="1"> <img src=" title="" width="" height="" />
na watoto wangu nimewmbia kwamba, siku nikifa nichomwe Moto, na msiba wangu usihusishe Dini yoyote ya wakoloni, huku watu wote wakikaribishwa kuongelea maswala ya UPENDO tu ambayo ndio dini ya kweli.

MY TAKE : Mwenezi wetu mpya wa chama aandae Maandamano makubwa kumpokea mbunge shujaa aliyependekeza hii sheria na hatimaye kupitishwa.
Hili bunge lipewe waarabu wa DP world
 
Nchi hii wabunge wamejipa umuhimu mkubwa sana, lkn ukweli bila wao nchi inaweza kwenda mbele bila shida yoyote.

Tuna wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, watendaji kata, na mabalozi hawa wote wanaweza kupiga kazi nchi ikasonga mbele.

Walimu na madaktari ni muhimu sana kuliko hata hao wabunge lkn maisha yao hayalingani kabisa.

Ifike wakati tuwaambie ukweli hawa wabunge waache kudeka, hii nchi ni yetu wote.
 
Keki yenyewe ya taifa ndogo hata tukisema tugawane hatutardhika acha wao wale kwa niaba yetu. Sisi hatuna njaa kiviiile. Wao wana uhitaji zaidi.
Sisi na nani wewe nyumbuu??!!
 
Back
Top Bottom