Biashara gani kwa mtaji wa sh Mil 20 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara gani kwa mtaji wa sh Mil 20

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mbimbinho, Jan 28, 2011.

 1. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Habari zenu wadau.
  Ndani ya wiki moja rafiki yangu anatarajia kupata mkopo wa Mil 20. Sasa ameniomba ushauri wa biashara gani anaweza fanya na akawa na uhakika wa kuingiza kuanzia sh 100,000 na zaidi kwa siku?
  Msaada wa mawazo ndugu zangu, maana mi mwenyewe sijui chochote kuhusu biashara na kwanza still student.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  biashara zipo nyingi sana kwa mil 20....

  tatizo sio aina ya biashara,tatizo aina ya mtu mwenyewe,biashara sio sawa na kuajiriwa...
  biashara unatakiwa wewe uwe wa kwanza ofisini na wa mwisho kutoka,na sometimes unaenda lala na kuamka na matatizo ya biashara yako

  wakati uliowaajiri wao wanasubiri mshahara tu mwisho wa mwezi hata kama faida hakuna....

  je huyo mwenzio anao uwezo wa kufanya bishara,?mentally?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli!
  Kipi kinatangulia, kutafuta na kuchukua mkopo bila kujua utafanyia nini au kutafuta cha kufanya, kufanya feasibility study au business plan kukipigia budget kisha kuomba mkopo?

  Ubaya wa kutafuta ushauri ili utumie fedha ya kukopa ni kwamba unaweza kupata idea nzuri mno lakini utekelezaji wake ukawa kazi. Hii inatokana na ukweli kwamba ni vema kufanya kitu unachokipenda na kukiweza. Mtu anaweza kukushauri fanya biashara ya kufuga kuku wakati maishani hujawahi kujaribu na wala hujui ufugaji huu unafanyika vipi. Utaingiza 20 m kununua vifaranga kisha wapitiwe na kideri wafe wote! Mkopo utarudisha vipi?
   
 4. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kama anajua kuziba pancha ya magari na kuuza matairi afanye!!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Halafu watu wanatakiwa kukopa ili kuendeleza biashara na sio kuanzisha biashara.....
   
 6. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,863
  Likes Received: 2,790
  Trophy Points: 280
  Na hiyo benki inayotoa fedha bila kuona business plan ni benki gani hiyo? Na kama alikuwa na business plan ya kuombea fedha halafu anataka kubadili ghafla huyo atapoteza fedha shauri yake! Mimi nilifikri jamaa angeanza kwanza kuwa na "viable business idea" halafu akatengeneza business plan ndo aende benki kukopa fedha! Kama haya hajayafanya mwambie aache kukimbilia fedha ya mkopo itamtokea puani!!
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Labda sio benki,kuna watu wanaitwa shark loaner ......
   
 8. babalao

  babalao Forum Spammer

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu atakuwa amekopa benki au SACCOS kwa guarantee ya mwajiri nimeona mifano hii kwa wafanyakazi wengi wakishakopa ndiyo wanatafuta business idea tena kwa kuomba ushauri kwa kila mtu, hii ni mbaya kweli kazi ipo kuwapatia watu hawa elimu ya ujasiriamali sitashangaa akianzisha business akakwama na kufulia.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hawa ndio wabaya kuliko hata benki.Unaenda kwa sharkloaner kama una kitu cha chapchap kinachohitaji hela ukifanye haraka nakurudisha upesi.Sharkloaners ni sharks kwelikweli hawana huruma.
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Biashara nzuri ni kuwarudishia ela yote wenye mkopo na kurudi kwanza kutafuta b'ness ya kufanya,ndo akakope sasa. Mkuu bila uongo,bora ueleze openly maana hamna anayeweza kukushauri bila kujua unaweza nini. Mi kwa mil20 naweza kuingia dili za viwanja na nkawa tajiri,naweza kuimport gari tatu na nkala ova 6mil profit in 2months nk,ila kama hujui la kufanya ujui!
   
 11. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Asanteni wandugu., ishu yenyewe ni hivi. Jamaa ndio kamaliza chuo this Month, so anampango wakati anahangaikia ajira nyumbani basi atafute kitu cha kufanya maana inafahamika kuwa Nchini kwetu kazi ni shughuli sana kuipata, hivo akaazima hela kwa rafiki ake kiasi cha Dola 15000. So yeye hana ujuzi na biashara yeyote, maana kitaaluma ni kwamba msela kamaliza Architecture.
   
 12. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  mkuu.... ninashauri afanye company registration kwanza itakayokuwa na diversity of objectives of which the company will do...including undertaking professional jobs in architeucture (his own field) or consultants works.. and including construction works....apate TIN, business license and bank a/c...halafu aanze kufanya review courses kwa ajili ya registration za Architect and Quantity surveyor Registration board... from there atakuwa ni mtu mwenye kampuni halali na saa yeyote anaweza kufanya kazi yeyote au bishara yeyote...hii ni kwa kuanzia na haitamcost zaidi ya 1.3 M ...... hapo ndipo anaweza kuanza kuendeleza a/c yake kwa shughuli mbali mbali na baadae akawa na a/c nzuri akapata mkopo mkubwa zaidi bank kwa ajili hata ya kununua mitambo ya ujenzi
   
 13. P

  Paul S.S Verified User

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu anaweza kutafuta mahali pazuri ambapo hamna dry cleaner akaanzisha baada ya kufanya study ya biashara yenyewe
   
 14. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu huyo rafiki yako anachukuaje mkopo bila kujua anaenda kuufanyia nini? Na je yeye anajua biashara gani? Nivizuri aombe ushauri kwa biashara anayo dhania itamlipa hicho kiasi anachotaka bcoz tayari atakua na interest ya kuifanya kwavile ni kazi aliobuni mwenyewe. I'm very sure lazima kuna shughuli aliodhania kufanya ndio maana akapatwa na msukumo wa kutaka kupotea hicho kiasi.
   
 15. B

  Bobby JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Habari yako mkuu Gsana. Sorry unaweza kutujuza zaidi hapa? Niko kwenye deal za magari pia kwa kiasi fulani. Ninahamu ya kujua, may be kwa hizo 20m ni brands gani za magari ambazo ungeagiza na ziko fast sokoni? natanguliza shukrani sana.
   
 16. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unaweza kuagiza gari 3 kwa mara moja au katika vipindi tofauti?
   
 17. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa hapa ni kutokuwa na mipango kuhusu biashara. Ilitakiwa afikirie biashara ya kufanya na mambo muhimu yote ndiyo achukue mkopo.
   
 18. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  anaweza fungua duka la hardware,na liwe mahali ambapo kuna shughuli za ujenzi wa mara kwa mara.
  pia supermarket inalipa.
  NINA UZOEFU NAVYO. kweli hutajuta na hakikisha unafatilia kwa karibu.
   
 19. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kwa mtaji wa Tsh.1,000,000/= (milioni moja tu) unaweza kuibuka bilionea kwa muda mfupi ili mradi una malengo thabiti ya muda mrefu na muda mfupi. Malengo haya yakiambatana na bidii, nina uhakika hata kama hiyo milioni moja utakuwa umekopa unaweza kuirudisha ndani ya mwezi moja na utabakia na faida ya milioni nyingine moja. Kwa maelezo zaidi na johnsonlugenge@yahoo.com nae atakupa njia ya kufanya.
   
 20. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  we utakuwa tapeli, kwanini mnataka muende chemba wakati ye kauliza hadharani? jibu swal bana
   
Loading...