Bia zimepanda bei

Bia zimepanda bei

minuz

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2014
Posts
624
Reaction score
216
Wanajamvi,

Bia zimepanda na bei jana nimeuziwa castle lager 2500 nilikua na ten tu ivyo niliishia bia 4 stim hakuna apo fegi sijavuta na mpira haujaisha costa rica wamekomaa balaa asa kutokana na huu ukata naludi nyumbani kuanzia leo ni mwendo wa konyagi tu mibia bei mbaya stim hakuna hela zenyewe za ku ungaunga bia sio dili wala nini wito kwa tanzania konyagi kazeni buti wateja tunaongezeka.
=============================================

TBL yaonyesha sononeko lake kuhusu kuongezewa kodi kinyemela.

Kupitia gazeti la Mwananchi lililochapishwa leo tar 24, Kampuni ya uzalishaji bia ya Tanzania Breweries Limited kupitia ofisi yake ya mkurugenzi mtendaji imetoa tangazo rasmi la kwa umma juu ya kitendo cha serikali kuendelea kuongeza kodi inayotozwa kwenye bidhaa za bia ambazo pia huzalishwa na kampuni hiyo.

Katika tangazo hilo, kampuni ya TBL imeelezea kuwa uamuzi wake wa kupandisha bei kwa mara ya kwanza mnamo July Mosi mwaka 2014.Ulitokana na bajeti ya Wizara ya fedha iliyosomwa Juni 12 mwaka huu iliyokuwa na ongezeko la kodi la asilimia kumi.

Tangazo hilo linaeleza kuwa, Baada ya TBL kufanya ongezeko la bei, serikali iliamua kupandisha kodi ghafla kufikia asilimia 20 kutoka asilimia kumi ya awali jambo linalo ilazimu TBL kupanga bei upya kulingana na ongezeko hilo la kodi. Kwa mantiki hiyo serikali imeongeza asilimia kumi nyingine 10% kinyemela tofauti na ile iliyopangwa kisheria na iliyosomwa kwenye bajeti ya serikali kupitia Waziri wa fedha

Kupitia tangazo hilo TBL imeilalamikia serikali kwa kuendelea kuikandamiza kampuni hiyo licha ya mchango wake mkubwa katika kodi ya serikali na maendeleo ya jamii

Tangazo hilo limeelezea mchango wa zaidi ya shilingi Billioni 600 ambao imechangia kwenye serikali kupitia makato ya kodi, kisha kuonesha uwekezaji wa dola millioni 500 za kimarekani uliolenga kupanua uzalishaji wa bia hapa nchini hususan katika mikoa ya Dar, Arusha na Mwanza.

Katika kuonesha umuhimu wa kampuni hiyo katika uchumi wa Taifa, TBL inaelezea fursa kubwa ya ajira iliyotoa kwa vijana wa kitanzania na kuonesha kuwa kitendo cha serikali kuendelea kupandisha kodi kiholela kinaweza kupunguza uzalishaji hivyo kusababisha kundi kubwa la vijana kupoteza ajira zao.

Pia kampuni imelalamikia gharama za ziada zinazoikumba kampuni hiyo zinaathiri sana shughuli zao kama hali isiyotabirika ya upatikanaji wa maji na umeme unaokatika mara kwa mara

Mwisho TBL inatoa malalamiko ya wazi juu ya mazingira magumu ya uwekezaji ambayo wamekuwa wakiyavumilia na kutaja shida kubwa wanayoipata kutokana na kutokuwa na nishati ya uhakika wala maji.

Pamoja na malalamiko yote TBL inamaliza kwa kuandika, "Kwa kuzingatia ufafanuzi huo, Tanzania Breweries Limited Imelazimika kuongeza bei ya bidhaa zake kutokana na ongezeko hilo.

 
hapo safi kabisa dakika chache tu akili inakaa vizuri
9k=

au kisichana chao kinatosha
2Q==
 
Wana jamvi bia zimepanda bei jana nimeuziwa castle lager 2500 nilikua na ten tu ivyo niliishia bia 4 stim hakuna apo fegi sijavuta na mpira haujaisha costa rica wamekomaa balaa asa kutokana na huu ukata naludi nyumbani kuanzia leo ni mwendo wa konyagi tu mibia bei mbaya stim hakuna hela zenyewe za ku ungaunga bia sio dili wala nini wito kwa tanzania konyagi kazeni buti wateja tunaongezeka

the spirit of nation
 
Mbona tutakoma,itabidi sasa hivi niwe naanzia Polisi Mess halafu ndio najichanganya kwenye viwanja vya kawaida.
 
Hahahaha lakin castle lager hazijapandishwa bei ni ileile 2.

Nakwambia jana nimeuziwa 2500 na nimelalamika ile mbaya lakini nilichemsha meneja wa bar akanipa ushauri nibadilishe bia ndio nikaona bora ya konyaji tu tabu yote ya nini bora kuyumba tu
 
Sasa kama hao wanaopanga hiyo bajeti wanapiga vita unywaji unategemea nini. Udini nao unachangia upuuzi mwingi tu Tz.Wengine wanafanya kukomoa tu, wala sio kwamba wamekosa vyanzo vya mapato
 
hahaaa,kiroba jogoo na banana wameongezewa kodi lakini hawajapandisha bei ya kinywaji...why?expecting tha drop outs of ''beeeeer''....!
 
Sasa kama hao wanaopanga hiyo bajeti wanapiga vita unywaji unategemea nini. Udini nao unachangia upuuzi mwingi tu Tz.Wengine wanafanya kukomoa tu, wala sio kwamba wamekosa vyanzo vya mapato
Hakuna udini na wala hukomolewi ,tunafanya hivyo kwa kuwa tunajua nyie ni walevi die hard hata ikiuzwa kwa dhahabu mtanunua tu!
 
mia mbili tu,,wanawasumbua wahudumu bure kusaka change
 
ina bidi tutafute style nyingine ya kutupa stim maana ma biaaa ishakuwa shida ktk bei
 
Mbona hiyo bei ndogo,wenzio hunywa bia kwa sh.4000

Hao ni mafisadi kwa sisi watz wa mshahara tarehe 40 kununua bia 4000 ni zambi kwanza ata stim yenyewe inakatika nikiifikilia tu iyo buku 4 moyo unadunda
 
Karibu katka Spirit Of Our Nation "konyagi"
 
Back
Top Bottom