Bi. Khadija MKE wa Mtume Muhammad ndio Sampuli ya Mke Bora ambaye unaweza kufanya naye Maisha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
Bi. KHADIJA MKE WA MTUME MUHAMMAD NDIO SAMPULI YA MKE BORA AMBAYE UNAWEZA KUFANYA NAYE MAISHA.

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani.

Ukisikia msemo usemao Nyuma ya kila mwanaume mwenye Mafanikio kuna Mwanamke, elewa kuwa Mwanamke anayetajwa hapo sio Mwanamke Kupe Nyonyaji, mbinafsi na goigoi au mdoli ambao kazi kukugeuza msukule.
Hapa tunazungumzia Wanawake WA maana, wasio wabinafsi, hapa tunazungumzia kina Bi. Khadija aliyemsapoti Mtume Muhammad na mwenye mchango mkubwa kwenye Dini kubwa na kongwe ya Uislam.

Hapa tunazungumzia Wanawake sampuli ya kina Sarah Mkewe Ibrahim, tunazungumzia Abigail Mkewe Daudi, tunazungumzia kina Maria Magdalena Rafiki wa Yesu aliyekuwa akimsapoti Yesu. Tunazungumzia Sipora Mkewe Nabii Musa. Hao ndio Wanawake ambao Kiuwiano wapo mmoja Kati ya Mia moja.

Vijana, nendeni Kwa matajiri watawapa Siri Hii. Usione matajiri Wana wake zao, ukasema mbona kale kamwanamke ni kabovu lakini jamaa anakang'ang'ania, nakupa Siri tuu, Mwanamke lazima awe Supportive, Msaidizi, ambaye sio Nyonyaji, yaani asiwe anawaza tuu kuhudumiwa n kujitanguliza mbelembele kisa ubinafsi wake.

Ukipata Mwanamke anayejitanguliza Mbele n mbinafsi umekwisha wewe.

Taikon nayasema haya Kutokana na vijana na wanaume wengi kupoteza muelekeo wa kimaisha.
Vijana wengi wamejikuta wakihenyeka,wakiteseka, wakipigwa kanyaga twende na malipo Yao huwa ni lawama na majuto.

Ndugu zangu, Mtume Muhammad (SWA) moja ya Watu mashuhuri zaidi Duniani WA muda wote hakuwa mjinga kuwa na Mwanamke Bora Bi. Khadija.
Role ya Bi. Khadija Kwa Muhammad ni kubwa na isiyosahaulika, Huwezi utajua uislam na MUHAMMAD pasipo kumtaja Bi. khadija. Never ever.

Sio kwamba MUHAMMAD hakuwa na Wake wengine, walikuwepo lakini Daraja la Bi. Khadija ni kubwa na lajuu zaidi kuliko hao wengine.

Huwezi mtaja Yesu na Ukristo pasipo kumtaja Maria Magdalena, hilo haliwezekaniki. Magdalena ndiye aliyekuwa bega Kwa bega na Yesu mpaka mwisho. Sio kwamba hakuna Wanawake wengine. Wapo. Nachelea kusema kama Yesu angeoa Basi angemuoa Magdalena.

Sababu kubwa ni kuwa ni nadra Sana Kupata Mwanamke mwenye Roho ya ukarimu na kupenda kama walivyo kina Bi. Khadija, Magdalena, Sipora, Sarah na majike mengine ya shoka.

ASIJE akakudanganya yeyote na mitazamo ya kijinga, ukipata MKE Umepata kitu Bora Sana. Lakini hapa tunazungumzia Mwanamke asiye mbinafsi, mwenye Upendo na ukarimu.

Sio unajitutumua kuhudumia limwanamke ambalo siku ukifukuzwa kazi linakukimbia, sio unahudumia Mwanamke ambaye siku ukifilisika linachanja mbuga na kukuacha.
Vijana, kitu pekee ambacho kitakujulisha kuwa Mwanamke uliyenaye ni WA Aina gani ni kuangalia ushiriki wake wa kiuchumi kwenye Maisha yako.

Ogopa Mwanamke wa chake ni chake, chako chawote. Hiyo ni mdudu Mbaya, kupe Nyonyaji. Ogopa Mwanamke ambaye linajitanguliza kimbelembele na kutaka lenyewe ndio ulitumikie.
Sisi Watibeli naam Aina ya kina Mtume Muhammad SWA, kina Yesu, kina Daudi, kina Ibrahim, na Musa na watu wengine wenye mitazamo kama yetu hatukubali ku-date na Makupe Nyonyaji. Na kamwe hatutaweza kuwa Misukule ya Watu wengine.
Na hatutaki Watu wawe Misukule yetu.

Vijana, hakuna Jambo zuri kwako kama kuishi na Mwanamke mwenye Roho ya ukarimu, upendo na kutoa kama ulivyo wewe.

Ogopa Mwanamke ambaye akitoa kipesa chake anakunja USO, ogopa Mwanamke ambaye akitoa kitu kidogo analalamika, hiyo ni fisadi, hasidi, kupe Nyonyaji, hakupendi. Na wanaume wa aina yetu naam Sisi Watibeli tunafukuza mara moja. Ni akheri uishi pekeako kuliko kuishi na Mwanamke mpigaji, yaani unaoa Mwanamke na kumuita Mkeo ambaye ni adui yako. Na wengi wanateseka Kwa sababu Hii.

Sisi Watibeli, tunasema ndoa ni nzuri ikiwa hakuna Utapeli iwe Utapeli Kwa Mwanamke au Mwanaume.

Hoja ya kuhudumia MKE wako ni hoja iliyodhahiri. Lakini kamwe usihudumie jitu tapeli, Nyonyaji, binafsi. Jitu ambalo sio MKE lakini lilikulaghai na kujifanya MKE.

Mhudumie Mwanamke wako ikiwa unajua kabisa hata siku ukiwa apeche Alolo atakuhudumia. Mwanamke ambaye mnasaidiana Maisha. Huyo ndio Mwanamke anayestahili kuitwa jina MKE.

Lakini ukishaona Mwanamke anazile pigo za kulalamika kuwa ametoa Pesa yake sijui anajitanguliza mbelembele huku hakujali wewe. Huyo piga Chini mara moja. Hakunaga familia ya maana iliyowahi kujengwa hivyo.

Mwanamke mbinafsi anajiwaza mwenyewe na watoto wake. Lakini Mwanamke mwenye Upendo, nazungumzia kina Bi. Khadija anamjali Kwanza mumewe ndipo wengine wafuate.
Sio ajabu siku ukizeeka Mkeo akakukimbia na akaenda Kwa Watoto wako na kukugombanisha na watoto wako ili uhenyeke na wengi WA Wazee wetu tumewaaona na ushahidi upo.

Ndugu zangu, najua kuna wenye Akili nzito hawatanielewa nazungumzia nini.

Kamwe, abadani usikubali kuishi na MTU mbinafsi ndani ya nyumba, usikubali kuweka Roho na Maisha yako rehani Kwa Mwanamke tapeli. Maisha yako ni yathamani kubwa.

Hivyo ndivyo utakavyofurahia Maisha MTU wangu. Hivyo ndivyo utakavyojivunia familia yako, yaani Mkeo na watoto.
Lakini ukijikoroga utakuwa kituko na kichekesho Dunia ingalipo.

Ogopa kuishi na Nyoka ndani ya nyumba. Unapoambiwa uishi na Mwanamke Kwa Akili hiyo ndio maana yake.
Wasije wakakuzidi Akili Kwa kukusifia ujingaujinga, ATI wewe ni Mwanaume Bhana, nihudumie bhana, jinyime kwaajili yangu bhana! Wakati lenyewe halifanyi chochote. Huko ni kuzidiwa Akili na wanawake. Pumbavu Kabisa!

Tumieni Akili za kiume na sio hisia za kiume. Huruma na kasumba za kijinga zimewaua wengi na kuwatesa wazee wenu.

Msije sema Taikon sikusema, Mimi nimemaliza.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hiyo mbegu ya wanawake aina ya khadija ilisha isha hapa Tz zilio bakia ni mbegu za wajasiliamali wa ndoa.

Wapo kibao
Sema uwiano wa Wanawake Maskini na matapeli ndio changamoto.

Ninajua matajiri na watu wenye vipato vikubwa hapa Tanzania ambao wake zao wamechangia pakubwa.

Lakini Maskini wengi wakiume ukichunguza kiini cha yote ni ku-date na Wanawake Kupe Nyonyaji. Lazima upasue matairi
 
Sasa hao wanawake wa shoka tutawapata je kwa kutumia criteria ipi? Wengi umasikini umesha wabadili tabia, wengine ndugu zao wanabadili tabia na muelekeo, wengine hawana dini waamunifu kwao ni mwiko.......kwahiyo tufanya je kuwapata hao?
 
Tathmilia pia zimechangia sana kuwafanya wanawake wawe feki na hatari sana kwa afya ya akili ya mwanaume.
 
Sasa hao wanawake wa shoka tutawapata je kwa kutumia criteria ipi? Wengi umasikini umesha wabadili tabia, wengine ndugu zao wanabadili tabia na muelekeo, wengine hawana dini waamunifu kwao ni mwiko.......kwahiyo tufanya je kuwapata hao?

Ipo Njia moja tuu.
Kumuomba Mungu Kwa sababu yeye ndiye anayewaleta.

Suleiman BINGWA wa Wanawake aliwahi kusema;

Mithali 19:14​

Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara/mwema hutoka kwa BWANA.

Mbele kidogo akataja Sifa za MKE anayetoka Kwa Bwana. Ambazo ni hizi hapa;
Mithali 31:
10Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.
12Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.
13Hutafuta sufu na kitani;
Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
14Afanana na merikebu za biashara;
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;
Na wajakazi wake sehemu zao.
16Huangalia shamba, akalinunua;
Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;
Hutia mikono yake nguvu.
18Huona kama bidhaa yake ina faida;
Taa yake haizimiki usiku.
19Hutia mikono yake katika kusokota;
Na mikono yake huishika pia.
20Huwakunjulia maskini mikono yake;
Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;
Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22Hujifanyia mazulia ya urembo;
Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni;
Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24Hufanya nguo za kitani na kuziuza;
Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;
Anaucheka wakati ujao.
26Hufumbua kinywa chake kwa hekima,
Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;
Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri;
Mumewe naye humsifu, na kusema,
29Binti za watu wengi wamefanya mema,
Lakini wewe umewapita wote.
 
Mwanamke mcha Mungu na mme hana mda wa kuangalia tamthilia
Tathmilia ni mpango wa shetani kubomoa familia kwa sababu anajua saikolojia ya mwanamke Ina copy ikionacho na kupaste kwenye ndoa kifuatacho ni msuguano, msuguano ukianza tu riziki unafunga kwenye ndoa hapo kila mmoja utafuta pa kupumulia mwingine bar mwingine kwa Ben 10 kifuatacho talaka,ili watoto wakose dira awapeleke kwenye ushoga,uteja,ukibaka,ulevi nk yote chanzo ni tamthilia thus tamthilia zote Dunia zinafanana bila kujali lugha kwa sababu zipo kwenye mission moja.
 
Mkuu pombe ni kinywaji cha mwanzo zaid duniani ukitoa maji ,kipo ata mbele ya maziwa , labda ulevi ila sio wa pombe.
 
Bi Khadija ni Mke bora kabisa ndie mke wa kwanza wa mtume alieanza nae maisha akiwa kijana wa miaka 25 na aliishi nae kwa miaka 25 kama sikosei ndio akaja kuoa wake wengine kwa lengo la kuwafundisha dini.

Na Bi. Khadija hakuwa na Noma licha ya kuwa na uchumi mkubwa. Pia alijua MUHAMMAD bado ni Mwanaume mdogo ilhali yeye umri umesogea
 
Bi. KHADIJA MKE WA MTUME MUHAMMAD NDIO SAMPULI YA MKE BORA AMBAYE UNAWEZA KUFANYA NAYE MAISHA.

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani.

Ukisikia msemo usemao Nyuma ya kila mwanaume mwenye Mafanikio kuna Mwanamke, elewa kuwa Mwanamke anayetajwa hapo sio Mwanamke Kupe Nyonyaji, mbinafsi na goigoi au mdoli ambao kazi kukugeuza msukule.
Hapa tunazungumzia Wanawake WA maana, wasio wabinafsi, hapa tunazungumzia kina Bi. Khadija aliyemsapoti Mtume Muhammad na mwenye mchango mkubwa kwenye Dini kubwa na kongwe ya Uislam.

Hapa tunazungumzia Wanawake sampuli ya kina Sarah Mkewe Ibrahim, tunazungumzia Abigail Mkewe Daudi, tunazungumzia kina Maria Magdalena Rafiki wa Yesu aliyekuwa akimsapoti Yesu. Tunazungumzia Sipora Mkewe Nabii Musa. Hao ndio Wanawake ambao Kiuwiano wapo mmoja Kati ya Mia moja.

Vijana, nendeni Kwa matajiri watawapa Siri Hii. Usione matajiri Wana wake zao, ukasema mbona kale kamwanamke ni kabovu lakini jamaa anakang'ang'ania, nakupa Siri tuu, Mwanamke lazima awe Supportive, Msaidizi, ambaye sio Nyonyaji, yaani asiwe anawaza tuu kuhudumiwa n kujitanguliza mbelembele kisa ubinafsi wake.

Ukipata Mwanamke anayejitanguliza Mbele n mbinafsi umekwisha wewe.

Taikon nayasema haya Kutokana na vijana na wanaume wengi kupoteza muelekeo wa kimaisha.
Vijana wengi wamejikuta wakihenyeka,wakiteseka, wakipigwa kanyaga twende na malipo Yao huwa ni lawama na majuto.

Ndugu zangu, Mtume Muhammad (SWA) moja ya Watu mashuhuri zaidi Duniani WA muda wote hakuwa mjinga kuwa na Mwanamke Bora Bi. Khadija.
Role ya Bi. Khadija Kwa Muhammad ni kubwa na isiyosahaulika, Huwezi utajua uislam na MUHAMMAD pasipo kumtaja Bi. khadija. Never ever.

Sio kwamba MUHAMMAD hakuwa na Wake wengine, walikuwepo lakini Daraja la Bi. Khadija ni kubwa na lajuu zaidi kuliko hao wengine.

Huwezi mtaja Yesu na Ukristo pasipo kumtaja Maria Magdalena, hilo haliwezekaniki. Magdalena ndiye aliyekuwa bega Kwa bega na Yesu mpaka mwisho. Sio kwamba hakuna Wanawake wengine. Wapo. Nachelea kusema kama Yesu angeoa Basi angemuoa Magdalena.

Sababu kubwa ni kuwa ni nadra Sana Kupata Mwanamke mwenye Roho ya ukarimu na kupenda kama walivyo kina Bi. Khadija, Magdalena, Sipora, Sarah na majike mengine ya shoka.

ASIJE akakudanganya yeyote na mitazamo ya kijinga, ukipata MKE Umepata kitu Bora Sana. Lakini hapa tunazungumzia Mwanamke asiye mbinafsi, mwenye Upendo na ukarimu.

Sio unajitutumua kuhudumia limwanamke ambalo siku ukifukuzwa kazi linakukimbia, sio unahudumia Mwanamke ambaye siku ukifilisika linachanja mbuga na kukuacha.
Vijana, kitu pekee ambacho kitakujulisha kuwa Mwanamke uliyenaye ni WA Aina gani ni kuangalia ushiriki wake wa kiuchumi kwenye Maisha yako.

Ogopa Mwanamke wa chake ni chake, chako chawote. Hiyo ni mdudu Mbaya, kupe Nyonyaji. Ogopa Mwanamke ambaye linajitanguliza kimbelembele na kutaka lenyewe ndio ulitumikie.
Sisi Watibeli naam Aina ya kina Mtume Muhammad SWA, kina Yesu, kina Daudi, kina Ibrahim, na Musa na watu wengine wenye mitazamo kama yetu hatukubali ku-date na Makupe Nyonyaji. Na kamwe hatutaweza kuwa Misukule ya Watu wengine.
Na hatutaki Watu wawe Misukule yetu.

Vijana, hakuna Jambo zuri kwako kama kuishi na Mwanamke mwenye Roho ya ukarimu, upendo na kutoa kama ulivyo wewe.

Ogopa Mwanamke ambaye akitoa kipesa chake anakunja USO, ogopa Mwanamke ambaye akitoa kitu kidogo analalamika, hiyo ni fisadi, hasidi, kupe Nyonyaji, hakupendi. Na wanaume wa aina yetu naam Sisi Watibeli tunafukuza mara moja. Ni akheri uishi pekeako kuliko kuishi na Mwanamke mpigaji, yaani unaoa Mwanamke na kumuita Mkeo ambaye ni adui yako. Na wengi wanateseka Kwa sababu Hii.

Sisi Watibeli, tunasema ndoa ni nzuri ikiwa hakuna Utapeli iwe Utapeli Kwa Mwanamke au Mwanaume.

Hoja ya kuhudumia MKE wako ni hoja iliyodhahiri. Lakini kamwe usihudumie jitu tapeli, Nyonyaji, binafsi. Jitu ambalo sio MKE lakini lilikulaghai na kujifanya MKE.

Mhudumie Mwanamke wako ikiwa unajua kabisa hata siku ukiwa apeche Alolo atakuhudumia. Mwanamke ambaye mnasaidiana Maisha. Huyo ndio Mwanamke anayestahili kuitwa jina MKE.

Lakini ukishaona Mwanamke anazile pigo za kulalamika kuwa ametoa Pesa yake sijui anajitanguliza mbelembele huku hakujali wewe. Huyo piga Chini mara moja. Hakunaga familia ya maana iliyowahi kujengwa hivyo.

Mwanamke mbinafsi anajiwaza mwenyewe na watoto wake. Lakini Mwanamke mwenye Upendo, nazungumzia kina Bi. Khadija anamjali Kwanza mumewe ndipo wengine wafuate.
Sio ajabu siku ukizeeka Mkeo akakukimbia na akaenda Kwa Watoto wako na kukugombanisha na watoto wako ili uhenyeke na wengi WA Wazee wetu tumewaaona na ushahidi upo.

Ndugu zangu, najua kuna wenye Akili nzito hawatanielewa nazungumzia nini.

Kamwe, abadani usikubali kuishi na MTU mbinafsi ndani ya nyumba, usikubali kuweka Roho na Maisha yako rehani Kwa Mwanamke tapeli. Maisha yako ni yathamani kubwa.

Hivyo ndivyo utakavyofurahia Maisha MTU wangu. Hivyo ndivyo utakavyojivunia familia yako, yaani Mkeo na watoto.
Lakini ukijikoroga utakuwa kituko na kichekesho Dunia ingalipo.

Ogopa kuishi na Nyoka ndani ya nyumba. Unapoambiwa uishi na Mwanamke Kwa Akili hiyo ndio maana yake.
Wasije wakakuzidi Akili Kwa kukusifia ujingaujinga, ATI wewe ni Mwanaume Bhana, nihudumie bhana, jinyime kwaajili yangu bhana! Wakati lenyewe halifanyi chochote. Huko ni kuzidiwa Akili na wanawake. Pumbavu Kabisa!

Tumieni Akili za kiume na sio hisia za kiume. Huruma na kasumba za kijinga zimewaua wengi na kuwatesa wazee wenu.

Msije sema Taikon sikusema, Mimi nimemaliza.

Acha nipumzike SASA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kuna WANAWAKE halafu kuna hawa wengine wenye jinsia za wanawake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom