Bi harusi atoroshwa, Kitchen Party Oktoba 31

Bi harusi atoroshwa, Kitchen Party Oktoba 31

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
attachment.php


KAZI sana! Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa nyumbani kwake siku chache kabla ya ndoa.

Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.



attachment.php

Bi harusi mtarajiwa, Saida Said (18) aliyetoroshwa siku chache kabla ya ndoa.

Akizungumza na Uwazi juzi, mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina lake lichapishwe gazetini alisema mama huyo amekuwa akihaha kwa binti yake kotoroshwa na mwanaume huyo tangu Septemba 25, mwaka huu ambapo kila akimpigia simu hapatikana hewani.


Jeshi la polisi bado liko ndani ya msako mkali ili kuhakikisha binti huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa kwa mwanaume huyo.


attachment.php

Muonekano wa karibu zaidi wa binti Saida Said.

"Mpaka sasa mama wa bi harusi hajatoa taarifa kwa bwana harusi wala ndugu zake, amekuwa akimtafuta kimyakimya huku akimuomba Mungu binti yake apatikane kwa vile mahari alishalipwa, sasa anaogopa ikifika siku ya ndoa itakuwa aibu kubwa," alisema ndugu huyo.

Ndugu huyo alisema Saida alitarajiwa kufanyiwa ‘kitchen part' Oktoba 31, mwaka huu na kufuatia na ndoa Novemba 6 huku ikidaiwa kuwa, upande wa bwana harusi michango inaendelea kama kawaida.

Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu; BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.

Source:Global Publishers
 

Attachments

  • IMG_1174.JPG
    IMG_1174.JPG
    43.1 KB · Views: 2,792
  • IMG_1178.JPG
    IMG_1178.JPG
    52.4 KB · Views: 2,789
  • biharusi.jpg
    biharusi.jpg
    61.4 KB · Views: 2,811
Duuh.. Mash'allah mtoto mlimbwende huyu..
Kwanza ametoroshwa au ameondoka kwa ridhaa yake mwenyewe..? Tayari ana miaka 18 na kisheria ni mtu mzima.. Nitashangaa kama atakamatwa huyo aliemchukua kama ikithibitika binti aliondoka kwa ridhaa yake mwenyewe..
Vile vile inawezekana huko alikotaka kuolewa hakukuwa chaguo lake..
Wawataarifu hao waliotaka kuoa na warudishe mahari..
 
hhahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa uwiiiiiiii ametoroshwa jamani haya ni majanga shab njoo huku umemtorosha mtoto wa watu
 
hahahaahaaaaaaaaaaaaa shemeji wee umenena maana mtoto mwenyewe ana miaka 18 ndo katoroshwa si kaona wazee wanamletea mizengwe ndo maana ametoroshwa na shaby
Duuh.. Mash'allah mtoto mlimbwende huyu..
Kwanza ametoroshwa au ameondoka kwa ridhaa yake mwenyewe..? Tayari ana miaka 18 na kisheria ni mtu mzima.. Nitashangaa kama atakamatwa huyo aliemchukua kama ikithibitika binti aliondoka kwa ridhaa yake mwenyewe..
Vile vile inawezekana huko alikotaka kuolewa hakukuwa chaguo lake..
Wawataarifu hao waliotaka kuoa na warudishe mahari..
 
wazazi wengine sijui wakoje! binti 18 badala wampeleke shule wanataka aolewe!!! hatari sana. watoto wadogo kama hawa ndio wanaendaga kuliwa tigo huko kwa waume zao maana ni rahisi sana kudanganyika bado wadogo.
 
hata mi ningemtorosha kwa kweli... mtoto anajicho kama dondola!!! hiyo rangi sasaaaaaa
 
hahahaahaaaaaaaaaaaaa shemeji wee umenena maana mtoto mwenyewe ana miaka 18 ndo katoroshwa si kaona wazee wanamletea mizengwe ndo maana ametoroshwa na shaby

Ha ha ha shem.. Inawezekana shaby hana kisu kirefu ndo maana wazazi wamepokea mahari toka kwa shefa mwingine.. Ila binti ana mahaba ya dhati kwa shaby.. Chezea mahaba wewe..
Mahaba nipige shoti..
 
Pia.....mama Saida naye anaweza kjikuta kwenye kosa la kuozesha mtoto... uswazi kazi
 
Duuh.. Mash'allah mtoto mlimbwende huyu..
Kwanza ametoroshwa au ameondoka kwa ridhaa yake mwenyewe..? Tayari ana miaka 18 na kisheria ni mtu mzima.. Nitashangaa kama atakamatwa huyo aliemchukua kama ikithibitika binti aliondoka kwa ridhaa yake mwenyewe..
Vile vile inawezekana huko alikotaka kuolewa hakukuwa chaguo lake..
Wawataarifu hao waliotaka kuoa na warudishe mahari..

uko sahihi halafu maeneo hayo wapemba kibao
na wapemba ndo zao kulazimishana ndoa
 
Nimempenda kadada karembo bora hata kangetorokea kwenye miss tz kangekuwa kamiss tz
 
chombo kweli! jaman shebby yaani umeshindwa kuvumilia ujue mwenzio kesha tolewa mahari na michango kwa mume mwinzio inaendelea. jaribu kuvaa viatu vya mkweo utajua ana hali gani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom