Military Genius
JF-Expert Member
- Mar 3, 2019
- 760
- 1,445
Hadi mwaka 2001 kulikua na idadi ya wakazi 1,200 lakini baadaye walihama wote Kutokana na mauzauza yanayoendelea huko. Kila ikifika jioni hakuna mtu yeyote kuingia katika kijiji hicho.
Serikali imeweka makatazo mengi kwa watalii na wananchi wa kawaida kuwa hawaruhusiwi kutembelea maeneo hayo ikifika jioni, hata wachache waliotaka kushuhudia kunanini na kwenda usiku hawakuwahi kurejea.
Watalii kadhaa hutoa shuhuda kuwa waingiapo tuu ndani ya kijiji hicho hata nyakati za mchana hupoteza utulivu, huhisi kama wako na watu wengine wanaowafuata bila wao kuwaona.
Usichokifahamu ni kuwa hata hao watalii wanaopata nafasi kwenda kutalii huko ni raia wa India pekee, serikali ilipiga marufuku kwa watalii wa nje ya India kufika huko kutokana na wengi wao kuwahi kwenda na kutorejea tena.
Haijulikani bado sababu ya hayo yote ni nini, lakini inaaminika kuwa hali hizi zilianza miaka mingi nyuma wakati ngome mbili za watawala tofauti zilipojengwa kijijini hapo, na mmoja Guru Baru Nath alionyesha kuzidiwa, akaacha laana.