Bhangarh: Kijiji cha ajabu nchini India

Military Genius

JF-Expert Member
Mar 3, 2019
536
1,000
IMG-20200808-WA0001.jpg
Kinaitwa kijiji cha Bhangarh kinachopatikana nje ya mji wa Rajgarh, Alwar nchinj India, kijiji hiki kipo tangu mwaka 1573 lakini hadi sasa kinatajwa kuwa ni moja ya maeneo hatari zaidi kuyatembelea nchini humo.

Hadi mwaka 2001 kulikua na idadi ya wakazi 1,200 lakini baadaye walihama wote Kutokana na mauzauza yanayoendelea huko. Kila ikifika jioni hakuna mtu yeyote kuingia katika kijiji hicho.

Serikali imeweka makatazo mengi kwa watalii na wananchi wa kawaida kuwa hawaruhusiwi kutembelea maeneo hayo ikifika jioni, hata wachache waliotaka kushuhudia kunanini na kwenda usiku hawakuwahi kurejea.

Watalii kadhaa hutoa shuhuda kuwa waingiapo tuu ndani ya kijiji hicho hata nyakati za mchana hupoteza utulivu, huhisi kama wako na watu wengine wanaowafuata bila wao kuwaona.

Usichokifahamu ni kuwa hata hao watalii wanaopata nafasi kwenda kutalii huko ni raia wa India pekee, serikali ilipiga marufuku kwa watalii wa nje ya India kufika huko kutokana na wengi wao kuwahi kwenda na kutorejea tena.

Haijulikani bado sababu ya hayo yote ni nini, lakini inaaminika kuwa hali hizi zilianza miaka mingi nyuma wakati ngome mbili za watawala tofauti zilipojengwa kijijini hapo, na mmoja Guru Baru Nath alionyesha kuzidiwa, akaacha laana.

IMG-20200808-WA0001.jpg
 
Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,159
2,000
Hawa jamaa utalii wao mkubwa ni wa majengo, wanajua kusifia na kuyakweza mitandaoni lakini ukifika hakuna chochote!

Mie nilikuwa na hamu na Lotus temple, ukiiona mitandaoni inavyosifiwa mpaka unaogopa!

Kufika pale ni jengo la kawaida sana, halina ishu yoyote ya maana! Ila wajinga wanatengeneza hela balaa kupitia utalii wa majengo! Sijui Tanzania tunakwama wapi kujenga majengi ya kitalii tunaishia kutangaza tembo na simba tuu kila mwaka!
 
.tunashindwa kujiongeza kabisa mkuuu
 
mtu chake

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
20,794
2,000
Hawa jamaa utalii wao mkubwa ni wa majengo, wanajua kusifia na kuyakweza mitandaoni lakini ukifika hakuna chochote!

Mie nilikuwa na hamu na Lotus temple, ukiiona mitandaoni inavyosifiwa mpaka unaogopa!

Kufika pale ni jengo la kawaida sana, halina ishu yoyote ya maana! Ila wajinga wanatengeneza hela balaa kupitia utalii wa majengo! Sijui Tanzania tunakwama wapi kujenga majengi ya kitalii tunaishia kutangaza tembo na simba tuu kila mwaka!
Hahahaha km hiki tulichokisoma hapa ,majengo ambayo yana mauza uza mbn bongo mengi tu , tunaweza kujibrand ila uvivu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
16,958
2,000
Hakuna chochote ni Uongo mtupu, hiyo laana ya huyo mtawala iwapate watu wa nchi zingine tu badala ya haohao wahindi waliomuudhi?

Na binadamu wa sikuhizi walivyo curious hasa wazungu wangeshafika siku nyingi sana humo mpaka katikati ya hilo jengo
 
Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
14,032

mkuu,kwa sisi wafuatiliaji wa Historia tunaamini katika laana,kuna dogo aliitwa king tutnkanam alikuwa mtawala wa misri toka akiwa mdogo kabisa,na alikufa akiwa kijana
kwenye kaburi lake kumeandikwa “laana impate yeyote atakayemsumbuwa pharaoh katika usingizi wake” ,watu waliobomoa hilo kaburi na kuiba mali zake walikufa vifo vya ajabu sana mara tuu baada ya kutoka hapo.fuatilia historia ya Misri laana is real
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,282
2,000
mkuu,kwa sisi wafuatiliaji wa Historia tunaamini katika rahana,kuna dogo aliitwa king tutnkanam alikuwa mtawala wa misri toka akiwa mdogo kabisa,na alikufa akiwa kijana
kwenye kaburi lake kumeandikwa “rahana impate yeyote atakayemsumbuwa pharaoh katika usingizi wake” ,watu waliobomoa hilo kaburi na kuiba mali zake walikufa vifo vya ajabu sana mara tuu baada ya kutoka hapo.fuatilia historia ya Misri rahana is real
Laana..

Rahana ndo nini sasa?
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
16,958
2,000
mkuu,kwa sisi wafuatiliaji wa Historia tunaamini katika laana,kuna dogo aliitwa king tutnkanam alikuwa mtawala wa misri toka akiwa mdogo kabisa,na alikufa akiwa kijana
kwenye kaburi lake kumeandikwa “laana impate yeyote atakayemsumbuwa pharaoh katika usingizi wake” ,watu waliobomoa hilo kaburi na kuiba mali zake walikufa vifo vya ajabu sana mara tuu baada ya kutoka hapo.fuatilia historia ya Misri laana is real
Hiyo ni historia, inaweza kuwa ya kweli au ya uongo.

Sio kila historia ni ya kweli hata kama watu wanaiamini, hiyo ni sawa na habari ya kihistoria ya kumgrade Cleopatra kuwa alikuwa ni Mwanamke mzuri na hatatokea mwanamke mzuri kama yeye hitimisho la dunia.

Naamini katika Karma, unapomfanyia mtu au watu jambo baya basi ipo siku nawewe utatendwa tu.
 
Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
14,032
2,000
Hiyo ni historia, inaweza kuwa ya kweli au ya uongo.

Sio kila historia ni ya kweli hata kama watu wanaiamini, hiyo ni sawa na habari ya kihistoria ya kumgrade Cleopatra kuwa alikuwa ni Mwanamke mzuri na hatatokea mwanamke mzuri kama yeye hitimisho la dunia.

Naamini katika Karma, unapomfanyia mtu au watu jambo baya basi ipo siku nawewe utatendwa tu.
mkuu ni Historia ya kweli,watu waliokutwa na laana hiyo walishuhudiwa kweli na picha zao zipo ni miaka ya 30-50 hapo.unaweza hata kuingia google ujisomee au kama unataka kuthibitisha mwenyewe jaribu kuchukua hizo mali za dhahabu mfano viti,sahani na vikombe vya farao alafu kinatachokutokea utathibitisha nachosema
 
nashukuru
 
Military Genius

JF-Expert Member
Mar 3, 2019
536
1,000
Hiyo ni historia, inaweza kuwa ya kweli au ya uongo.

Sio kila historia ni ya kweli hata kama watu wanaiamini, hiyo ni sawa na habari ya kihistoria ya kumgrade Cleopatra kuwa alikuwa ni Mwanamke mzuri na hatatokea mwanamke mzuri kama yeye hitimisho la dunia.

Naamini katika Karma, unapomfanyia mtu au watu jambo baya basi ipo siku nawewe utatendwa tu.
.samahani unaweza ukapita na google kidogo
 
Kamongo

JF-Expert Member
Mar 20, 2009
933
1,000
Hawa jamaa utalii wao mkubwa ni wa majengo, wanajua kusifia na kuyakweza mitandaoni lakini ukifika hakuna chochote!

Mie nilikuwa na hamu na Lotus temple, ukiiona mitandaoni inavyosifiwa mpaka unaogopa!

Kufika pale ni jengo la kawaida sana, halina ishu yoyote ya maana! Ila wajinga wanatengeneza hela balaa kupitia utalii wa majengo! Sijui Tanzania tunakwama wapi kujenga majengi ya kitalii tunaishia kutangaza tembo na simba tuu kila mwaka!
Posta palikuwa na majengo mengi ya zamani lakini yote yamevunjwa,mfano salamander,Magoti ect
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
2,145
2,000
Hawa jamaa utalii wao mkubwa ni wa majengo, wanajua kusifia na kuyakweza mitandaoni lakini ukifika hakuna chochote!

Mie nilikuwa na hamu na Lotus temple, ukiiona mitandaoni inavyosifiwa mpaka unaogopa!

Kufika pale ni jengo la kawaida sana, halina ishu yoyote ya maana! Ila wajinga wanatengeneza hela balaa kupitia utalii wa majengo! Sijui Tanzania tunakwama wapi kujenga majengi ya kitalii tunaishia kutangaza tembo na simba tuu kila mwaka!
Mkuu Lakini Hayo Ni Majengo Ya Zamani ambayo hata Sisi tunayo Bagamoyo,Zanzibar,Kilwa,Dodoma Kondoa,Pangani na kwengineko....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom