Mimi kama mimi kilimo kinaniwezesha kuishi maisha ya wastani na kupeleka watoto wangu shule, hapa nilipo nina akiba ya kutosha bank kutokana na kilimo. Ila ninataka wakulima wengi wakwamuliwe, tatizo naona ni wao kuwezeshwa kwa kupewa mikopo na mambo ya masoko, kwani kilimo hakipewi kipaombele na watunga sera. Mimi sipo kwenye kilimo cha kusubiri mvua kwani nilishapata mtaji toka kwenye ajira niliyoamua kuiacha. Lakini ningependa nifanye kilimo kikubwa cha kuuza kimataifa hapo ndio ninapokwama pindi ninapotaka mtaji mkubwa wa kuendana na wazo langu. Sasa wewe ndugu yangu nikukuambia bila pesa huwezi kufanya lolote la maana, wewe unasema sio kila kitu kinahitaji hela!! Ili taifa liweze kusonga mbele inahitajika mipango mizuri na itafanikishwa kwa hela, hao unaowaona wakibishana hapa hawatokaa waondoke hata kama maendeleo yapatikane kwani ni sawa na kusema maendeleo yakipatikana basi Simba na Yanga zitaondoka.
Halafu kwenye mada yako, hawa wanaobishana hapa ambao ni cdm na ccm wengi wao wako mijini na wanaulewa wa mambo. Wana nafuu ya kimaisha kwa mantiki ya kuweza kulipa kodi ya nyumba na kumudu gharama fulani za mahitaji ya lazima. Hao ambao hawabishani na wengi wao wako kijijini hali zao ndio choka mbaya. Kwa hiyo siyo kweli kwamba maendeleo ya nchi hii yanakwamisha kwa haya malumbano ya cdm na ccm. Kama una wazo lenye tija la kuweza kuifanya nchi iendelee lilete lifanyiwe kazi na wala haliwezi kuondoa ushabiki uliopo.