Beyond Ufipa, Lumumba Political Discourses

Beyond Ufipa, Lumumba Political Discourses

nani kakudanganya pesa zinaleta maendeleo?.....mipango madhubuti, uthubutu, elimu, kujituma ndio chachu ya maendeleo......hata kabla ya pesa hazijagunduliwa watu walikuwa na maendeleo
Well said brother!
 
Hongera kwa ujumbe huu ndg Azizi Mussa. Wa Ufipa sidhani km wanaweza kukuelewa. Maana wao wanadhani chama kutetea mafisadi pengine hela zile watakuja kugawiwa bure na rais aliyetokana na mafisadi.
Kumbe sera hii ya awamu ya tano ya kauli mbiu ya hapa kazi inaweza kuleta matokeo chanya + huko tuendako km nchi lkn siyo km chama. Tanzania Mpya yaweza kuja.
 
Mkuu, shida yako ni kwamba unataka kutulazimisha sisi Watanzania wapiga porojo, wambea, wapenda udaku, tusiopenda kujisomea...tufikiri kwa kina na nje ya boksi. Hilo haliwezekani kwa sababu mfumo wetu wa elimu, kijamii na hata kitamaduni haujatuandaa kuwa watu wa kuhoji na kufikiri mambo kwa undani. Kama nilivyoona hapo juu we jiandae kutukanwa tu!

Weka mada nyepesi nyepesi tujadili hapa ohoooo ‍♂️‍♂️‍♂️‍♂️‍♂️‍♂️‍♂️‍♂️‍♂️
Umejibu vizuri, kinachotusumbua sisi ni "footprint" ya maisha yetu tangu tukiwa watoto.
 
Usitake kupotosha nilichosema, halafu uchawi na mwafrika ni jambo la kawaida sana.
Hahahahha, uko sahihi sana na ndicho tulichosema hapa. Tanzania ina vitu vya kututosheleza sote; Roho mbaya ndio huleta sumu ndani yetu

Uchawi ni tabia ya kutopenda kuona wengine wakifanikiwa na kufurahia anapowaona wakipata tabu ijapokuwa katika desturi hiyo mhusika hanufaiki chochote. Yaani yeye furaha yake ni akiona wengine wanakwama na hili kaligusia bwana Trump kwenye hotuba yake ya kuudhi kuhusu Afrika.

Tofauti tu ni kwamba kuna wachawi wenye vifaa na wale wasio na vifaa.
 
Hata humu jf huwezi ukachangia kitu cha maana sababu ya CCM? Mzee Lowasa alivyo kuwa CCM alikuwa ni zaidi ya Shetani alivyokuja kwenu amekuwa zaidi ya malaika? Nyalandu akiwa CCM alikuwa fisadi amekuja kwenu amekuwa mtu mwema? Mtulya akiwa kwenu alikuwa mtu ameenda CCM amekuwa zaidi ya Shetani! Hii ni aibu kwa nchi na kwa Afrika kuwa na watu wenye akili kama zako na wenzako. Any way sio kwamba hamjui! Tatizo Unafiki! ipo siku matunda ya mnachokipanda yatapatikana kwani halimtokei mtu isipokua lile alilootesha kwa mikono yake.

Labda nikuulize swali moja dogo tu. Ndani ya chama chenu, ni kitu gani hasa mnachofanya ili kuhakikisha kuwa viongozi wa chama chenu wanakuwa upgraded na kuwa bora zaidi ya wengine? au mtu akishakuja kwenu tu tayari malaika? Upuuzi mkubwa. Sory! unafiki mkubwa.

hapa mkuu umejionyesha ni mwana Lumumba,its ok mkuu kuwa mwana CCM sio dhambi
 
hapa mkuu umejionyesha ni mwana Lumumba,its ok mkuu kuwa mwana CCM sio dhambi
Kwani kuwa Ccm shida nini sasa?Au hoja hapo ni nini? Yaani ni sawa na kusema Mimi nitakuwa ni mwanaume ! Yeah kweli ni mwanaume, kwa hiyo?

Haujui kuwa Ccm ndio chama kinachounda serikali, kwa hiyo hata wewe maisha yako ni ya ki Ccm Ccm pia?
 
nani kakudanganya pesa zinaleta maendeleo?.....mipango madhubuti, uthubutu, elimu, kujituma ndio chachu ya maendeleo......hata kabla ya pesa hazijagunduliwa watu walikuwa na maendeleo

Hivi mnaongea nini nyie, ukiwa na hela ukakosa maendeleo basi wewe utakuwa umezitapanya tna utakuwa ni bonge la kenge. Hiyo mipango madhubuti, uthubutu, nk vinafanyika kwa kuwezeshwa na pesa. Hata wenye mawazo mazuri sana, hukopa pesa ili kufanikisha mawazo yao, au hufadhiliwa pesa ili waweze kufanikisha na kutekeleza mawazo yao. Mimi hapa nilipo nipe pesa, wewe baki na mipango yako madhubuti, uthubutu na elimu, kisha tupe mwaka mmoja njoo uone mimi na mwenye hizo sifa ulizotaja nani atakuwa na maendeleo. Pigeni hadithi zenu za kuongopeana hapa na Azizi, kama huna pesa your nothing in this world my friend. Ukiwa na pesa utapata kila kitu dunia hii labda ushindwe tu kununua furaha na kuzuia kifo, lakini sio maendeleo.
 
Mkuu tindo

Mtu awapo usingizini, walioko pembeni wanamuona tu kalala pale ila yeye mwenyewe kwa wakati ule anakuwa hana consciousness ya kuwepo pale alipo hadi atakapozinduka usingizini.

Kadhalika, anaweza awe anaota ndoto ambayo humfanya aamini bila wasiwasi kuwa katika ndoto hiyo yuko katika mazingira halisia.

Mazingira ambayo anakuwa nayo mtu akiwa ndotoni, hawawezi kuyaexperience waliomzunguka, na muhusika hawezi pia kuexperience mazingira ya nje hadi atakapo ibuka usingizini ndio kwa haraka hurudi kwenye physical world na kubaini alikuwa ndotoni

Sasa hebu fikiri ni nini kitatokea kama kwa sababu yoyote mtu alielala atashindwa kuamka na akaunganisha?

Ukinielewa hapa, hautapata shida kuelewa mada nyingine.
 
Hivi mnaongea nini nyie, ukiwa na hela ukakosa maendeleo basi wewe utakuwa umezitapanya tna utakuwa ni bonge la kenge. Hiyo mipango madhubuti, uthubutu, nk vinafanyika kwa kuwezeshwa na pesa. Hata wenye mawazo mazuri sana, hukopa pesa ili kufanikisha mawazo yao, au hufadhiliwa pesa ili waweze kufanikisha na kutekeleza mawazo yao. Mimi hapa nilipo nipe pesa, wewe baki na mipango yako madhubuti, uthubutu na elimu, kisha tupe mwaka mmoja njoo uone mimi na mwenye hizo sifa ulizotaja nani atakuwa na maendeleo. Pigeni hadithi zenu za kuongopeana hapa na Azizi, kama huna pesa your nothing in this world my friend. Ukiwa na pesa utapata kila kitu dunia hii labda ushindwe tu kununua furaha na kuzuia kifo, lakini sio maendeleo.
pesa sio msingi wa maendeleo .....unadhani kwa nini kuna nchi masikini na nchi tajiri?......kwani nchi masikini hawatumii pesa?.....maendeleo yanaletwa na maarifa,ujuzi, uthubutu,kufanya kazi kwa bidii n.k....matajiri, watu wenye maendeleo sio kwamba walianza biashara na pesa nyingi hakuna kitu kama hicho bali ubunifu, maarifa, kujituma ndio kumewafikisha hapo walipo...maarifa ,elimu, ndio kila kitu....kuna watu ni madalali hawana huo mtaji wa pesa nni matajiri kuliko wewe mwenye mtaji wa mamilioni ya pesa.....usidhani ukiw na mapesaa mengi ndio utapata maendeleo si kweli kama huna maarifa,sio mbunifu, huna elimu hizo pesa zitaisha tu utabaki omba omba
 
Pitia post yangu vizuri nimesema ukiwa na pesa ukakosa maendeleo basi utakuwa umezitapanya na utakuwa ni bonge la kenge. Unaweza usiwe na maarifa, ujuzi nk, lakini ukatumia pesa zako kuwalipa wenye maarifa na ujuzi kufikia maendeleo yako. Hapa nchini kwetu kuna watu wana maarifa, ujuzi nk lakini wanazidiwa maendeleo na wenye pesa hata kama wamezipata kifisadi. Hii reli ya SGR haijengwi na wenye maarifa wala wenye ujuzi wa hapa nchini kwetu, bali tunatumia pesa ili kupata hiyo treni. Hao wenye ujuzi, maarifa, uthubutu, wafanyakazi nk wote hakuna mwenye uwezo wa kujenga hiyo reli. Narudia tena, pesa ni kila kitu kasoro kununua furaha na kuzuia kifo tu. Huna pesa huwezi kupata maendeleo, kwani hata mawazo mazuri yanafanyika kwa wepesi kama una hela. Hebu kuwa na wazo zuri bila kuwa na pesa kama hujafa na hilo wazo lako ndani. Ila kama una hela hata kama umelala kitandani utatekeleza maendeleo yako.

Wewe mwenyewe ulikuwa ccm, Lowassa alivyohamia cdm ukamfuata kwa ajili ya hela zake. Lowassa huyo huyo alipokuwa ccm viongozi wa cdm walimwita fisadi ile mbaya. Lakini alipopenyeza rupia tu, Lowassa akageuka malaika na kelele zote zikaisha. Angeenda basi na huo ujuzi, maarifa, sijui na uchapa kazi kama kuna mtu angemnyenyekea. Zungumza chochote wewe na huyo Azizi wako lakini pesa acha kabisa dogo.
 
kuongelea maendeleo bila kuongelea siasa ni kiongelea kuoga bila maji. hata nikiongelea kufanya shughuli zangu siwez ruka kiunz bila kutaja wanasiasa maana ndio huamua biashara iweje nchini.

utafanyaje biashara bila kujua kodi . utafunguaje kiwanda bila kujua sera za nchi. utaendeshaje dini bila kujua kuwaombea tu na si kuwaambia dhambi zao wakuu wako. kimsing kujitoa kwenye siasa ni kuupuza jua kuliita mwezi wakati linakuunguza
 
Hakuna mtu atakayeibuka kutoka angani akatutoa hapa tulipo, ni sisi wenyewe tuonene tunasonga vipi mbele na tusipoanza sasa tutaanza lini? Changamoto za nchi hii hatuna wa kumlaumu zaidi yetu sisi wenyewe.

Tujitahidini kufikiri nje ya box, tusiwe tunakimbia spidi kubwa lakini wakati huo huo tumejifungia ndani. Ni muhimu kuona ni kwa vipi tunaweza kuboresha siasa zetu ili kila mara tuweze kuwa na viongozi bora zaidi lakini pia tuwe na wanachama na wananchi wanaoweza kusaidia mawazo yenye maana ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo
 
Back
Top Bottom