Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Kwanini Tusiamue kufanya itikadi ya Trump kuwa "Wrong" Kwa kujiongeza na kufikiri zaidi ya kujibizana wewe wa lumumba wewe! wewe wa ufipa!!
Ndugu watanzania wenzangu, tunatakiwa tufahamu kuwa dunia haitusubiri na muda tulio nao duniani ni mfupi mno. Sasa tukiamua kujifungia kwenye kaduara kadogo mno ka kufikiri wakati wenzetu wanatanua wigo wa kufikiri na kufanya maamuzi yenye impact za ajabu duniani na kuyatekeleza kwa kasi ndani na nje ya nchi zao ili kutimiza dhima ya maisha yao; huo utakuwa ni mzigo wetu wenyewe kama watanzania. Tutakuwa tumeamua kuwa mfano wa sisimizi aliyeingia kwenye kifuu chenye maji akadhani anaogelea kwenye bahari, kumbe yuko kwenye dunia ya peke yake!.
Dunia ni pana sana na ina vitu vingi sana ila kwa bahati mbaya Watanzania wengi (si wote) tunafikiri Dunia ni Ufipa na Lumumba, Chadema na CCM, kisha tushamaliza kila kitu, kinachofuata udaku wa kiongozi gani kamjibu nani au nani kamjibu kiongozi gani.
Ni lazima sasa Watanzania tuelewe kuwa ili kuweza kupata mabadiliko na maendeleo tunayoyataka na nchi yetu iwe bora kuliko hapo kabla, ni lazima sisi wenyewe kwanza kubadilika kwanza, na hayo yote huanzia kwenye fikra zetu.
Ndugu watanzania wenzangu; tusipoamua kubadilika hakuna kitakachobadilika juu yetu. Hiyo ni kanuni ya kimaumbile. Tusichoke kujifunza na tunayojifunza tuyafanyie kazi.Tusione aibu kubadilika kwani ndio njia pekee itakayotuwezesha kwenda mbele kwa kasi. Si nchi,si vyama vya siasa au kitu chochote kitakachokuwa bora ikiwa hatutabadilisha fikra zetu .
Tunasema eti karne ya 15, Afrika na Ulaya zilikuwa na maendeleo yanayokaribia kulingana lakini hatutafakari kwa kina kwamba kwa nini tupo hivi leo, tunafanya nini na wengine wanafanya nini na kwa nini. Tunapenda sana simple things, decisions & conclusions kwenye mambo nyeti.Tunasema Waafrika hatupendani kisha tunaishia hapo. Tunasema ukosefu wa ajira kwa vijana nchini ni bomu linalosubiri kulipuka kisha tunaishia hapo.Tunasema uzalendo umepotea Tanzania lakini hatupigi hatua mbele kujiuliza kwa nini na tufanye nini. Tunasema watanzania hatupendi kusoma vitabu halafu tunaishia hapo.Tunasema watanzania hatupendi kujadili mada za maana na kutoa hoja zenye manufaa kwetu na kwa watanzania wenzetu kisha tunaishia hapo then tunasubiria tukio la siku! n.k.
Kama mtu hajui aendako hawezi kupotea. Popote alipo au atakapokuwa itakuwa ni sawa. Kama mtu hajui au hana uhakika wa nini atakacho, chochote apatacho ni sawa.Kokote atakapoanzia, kokote atakapopita na atakapoishia ni sawa tu. Upepo ukiende kushoto, ataenda ukirudi kulia atarudi na ukiisha atatulia alipo.
Ni lazima wanadamu tuishi maisha yenye dhima "live with purpose" Tujue kwa nini tunaishi? tunataka nini? na tujiwekee misingi ya kufikia kile anachokitaka. Watanzania wengi hili bado hatujalielewa na athari yake ni kwamba tukiamka asubuhi tunaangalia nini kinatokea; tuanaenda nacho hadi jioni, tukiamka siku ya pili tunaangalia tena nini kinatokea tunaenda nacho na cha jana yake tushakisahau hivyo hivyo hadi kila mmoja wetu muda wake wa kuondoka duniani unafika, anaondoka naye anasahaulika.
Sasa kwa kuishi maisha ya namna hiyo, tusitegemee kupata matokeo ya maana sana wala kuwa na mchango mkubwa kwenye kuibadili nchi hii na hali ya maisha ya watu wake kwani katika mazingira hayo; chochote kitokeacho kwetu ni sawa kwa kuwa hatuna muelekeo maalum.
Mathalan, kuna mambo ambayo watanzania kila tukiamka asubuhi tunayalalamikia lakini hatuchukui hatua yoyote ya maana, au hatua tunazochukua ni zile zile na matokeo yanakuwa yale yale lakini wala hatugutuki; tunaendelea vile vile tu! tukiamini ipo siku mambo yatabadilika tu bila kujua kuwa kufanya hivyo ni kinyume kabisa na kanuni za kimaumbile ambapo ili binadamu afanikiwe ni lazima a- comply na kanuni hizo za kimaumbile.
Pamoja na maneno yakuudhi aliyotuambia Mzee Trumph; tunayo mambo ya kujifunza kutoka kwake hasa alipoeleza baadhi ya mambo yaliyoifanya Amerika na Ulaya Kuendelea na baadhi ya matatizo aliyotueleza kuwa watu weusi tunayo ikiwemo tabia ya kupenda kutafuta zilipo ndizi mbivu badala ya kuivisha za kwetu.
Kama Watanzania tukiamua kubadilika na kuachana na ushabiki huu usiotusaidia na tukajiongeza kidogo; kila kitu kinachotuhusu kitabadilika na kama tukiendelea kuwa kama tulivyo hakuna kitakachobadilika.