DIDAS TUMAINI
JF-Expert Member
- Nov 11, 2014
- 232
- 650
Kitabu cha Guiness cha Rekodi za Dunia ambacho huchapishwa kila mwaka kikibeba rekodi za mafanikio ya juu kabisa ya binadamu katika nyanja mbalimbali na maajabu ya asili(Guinness World Book of Records) kimemtangaza Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye kuwa ndie mtu aliyeweka rekodi Duniani ya kukamatwa mara nyingi zaidi na Polisi.
Jumatatu tarehe 20 Januari 2020 alifikisha jumla ya kukamatwa mara 50 ambapo alishikiliwa katika kituo cha Polisi Nalufenya kabla ya kuhutubia wakereketwa wa chama chake katika uwanja wa Bugembe.
Wakati wakijiandaa ghafla vitu havikwenda kama ilivyotegemewa na kujikuta yeye na timu yake wakiingia katika tafrani na Polisi wa vituo vya Jinja, Bugembe na Kakira. Mambo yalizidi kuwa si mambo baada ya Wanajeshi kutoka Barracks za Gadaffi walipofika eneo hilo hadi mabomu ya machozi kutumika.
Kwa mwaka 2016 pekee alikamatwa mara 15 kipindi cha uchaguzi.
Cha kushangaza, Rais huyo mstaafu wa chama cha Forum Democratic Change hajawahi kupewa hukumu hata mara moja ya makosa anayotuhumiwa na kukamatwa nayo.