Bernard Membe ahojiwa na Kamati ndogo ya maadili CCM. Asema kafurahishwa kwakuwa amepata nafasi ya kutoa maoni na kujieleza yote waliyotaka kuyajua

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Nimeshawasili eneo la tukio. Matayarisho yasiyo na dalili ya dalili ya ahirisho yamefanyika na kukamilika. Hapa Dodoma, wahusika wameshafika. Wamejipanga na kupangika.

Makada waandamizi wa chama wanapishana na makabrasha yasiyo na bashasha kuhusu suala la akina Membe, Makamba na Kinana hapa White House Dodoma. Wanawahi kuweka mambo sawa.

Wanakamati Ndogo ya Maadili ya CCM walishafika hapa Ukumbini mapema sana. Kwasasa, wanajipiga msasa wa kisasa wakisubiri kuanza kwa jambo lililotukutanisha hapa (ataanza Membe) hapo saa tatu asubuhi hii. Membe ameshafika.

Membe, Makamba na Kinana wamejipanga kuusema ukweli ambao hausemwi ndani ya CCM kwa sasa. Wanapata fursa yenye ruhusa kama kipusa kuutuma ujumbe muhimu wa kichama kwa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM itakayopelekewa mapendekezo.

Kamati hii Ndogo ya Maadili ya CCM itawasikiliza wahusika na baadaye kuwasilisha ripoti yenye mapendekezo kwa NEC. NEC ndiyo inayoweza kutoa uamuzi, kwa mujibu wa Katiba ya CCM na Kanuni zake, kwa wahusika. Leo ndiyo mwisho wa kusubiri kwao!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa White House, Dodoma)
Wanakamati


Membe awasili ofisi za CCM kuhojiwa

membe+pc.jpg

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe leo asubuhi Alhamisi Februari 6, 2020 amewasili katika ofisi za makao makuu ya CCM mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma za kimaadili zinazomkabili.

Membe amewasili katika ofisi hizo maarufu ‘White House’ akiwa katika gari aina ya Range Rover jeusi.

Baada ya kuwasili katika ofisi hizo, Membe aliyevaa suruali nyeusi na shati lenye michirizi mieusi na kijani, alisalimiana na watu mbalimbali aliowakuta nje, kisha kuingia ndani ya jengo hilo lililopo katikati ya Jiji la Dodoma.

Ujio wa Membe katika jengo la White House jijini Dodoma leo Februari 6,2020, utakuwa umefungua milango kwa vigogo watatu wanaotakiwa kuhojiwa na Kamati ndogo ya maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara.

Ulinzi katika viunga vya ‘White House’ umeimarishwa katika ofisi hizo ambapo kwa mara kwa kwanza Kampuni ya ulinzi ya Suma JKT ndiyo wanaolinda wakati siku za nyuma wamekuwa wakilinda raia wa kawaida huku waandishi wakizuiliwa kuingia getini.

Mahojiano yaendelea

Hadi saa 7:20 mchana leo Alhamisi Februari 6, 2020 Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe alikuwa katika ofisi za makao makuu ya CCM mjini Dodoma alikofika leo saa 3 asubuhi kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma za kimaadili zinazomkabili.

Mh. Membe azungumza mara baada ya mahojiano ya masaa 5

Membe2+pic.jpg

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema amekuwa mtu wa furaha baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dodoma leo Alhamisi Februari 6.

Membe amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoka katika mahojiano hayo yaliyochukua saa tatu.

“Tulikuwa na mkutano wa masaa matatu ya mijadala mizuri, mikubwa, ya kitaifa inayohusu Chama chetu Cha Mapinduzi na nchi yetu, na nimekuwa mtu wa furaha kubwa ajabu kwa sababu nimepata nafasi nzuri ya kufafanua mambo kadhaa ambayo chama changu ilitaka kuyajua.

“Nimepata nafasi ya kutoa mawazo ya yale mambo ambayo niliombwa kutoa, kwa hiyo sasa hivi mimi na mke wangu tunakwenda kula chakula kizuri sana kwenye hoteli moja ambayo haijulikani baada ya hapo nitaanza safari ya kurudi Dar es Salaam, lakini niwaambie safari hii ya kuja Dodoma, ilikuwa ni ya masaa makubwa sana kwa chama na kwa taifa…” amesema Membe.

Pia soma: Bernard Membe aitwa kwenye Kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti wa Nidhamu CCM
 
VUTA-NKUVUTE,

Nilimsikia Polepole akiomba chama kiwaruhusu vijana wawashe moto wa kuusema ukweli wa wazee fulani tunaodhani wanaheshima saana kwenye chama na nchini.

Sie tungependa waendelee tu kuwafichia siri zao - ili tuendelee kuwaheshimu.
Washauri wazee wenzako wasije wakatufikisha huko.
 
Yeye polepole ana heshima gani? Au huyo Jiwe ana heshima gani?
VUTA-NKUVUTE,

Nilimsikia Polepole akiomba chama kiwaruhusu vijana wawashe moto wa kuusema ukweli wa wazee fulani tunaodhani wanaheshima saana kwenye chama na nchini.

Sie tungependa waendelee tu kuwafichia siri zao - ili tuendelee kuwaheshimu.
Washauri wazee wenzako wasije wakatufikisha huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom