Benki ya Dunia imetoa ripoti ambayo imekuwa na sura kuu mbili ikiibebesha sifa Tanzania kiuchumi

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Hivi karibuni Benki ya Dunia imetoa ripoti ambayo imekuwa na sura kuu mbili ikiibebesha sifa Tanzania kiuchumi

Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani alikuta hali ya uchumi ikiwa katika misukosuko mingi ikiwamo janga la ugonjwa wa Covid-19, mahsusi ripoti ikieleza angalizo kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara. Ripoti hiyo imefanunua kwamba wakati nchi za jirani na Tanzania barani Africa, Uchumi wake ukishuka kwa wastani wa asilimia 2 za pato lao la taifa, hali ilikua kinyume na Tanzania ikishuhudiwa uchumi wake unapanda kwa wastani wa asilimia mbili.

Ongezeko hilo litatokana na kiongozi wa nchi (Rais Samia Suluhu Hassan) kufanya juhudi kupandisha uchumi wa nchi hadi mwishoni mwa mwaka 2021 penye misukosuko uchumi wa Tanzania uliongezeka kufikia wastani wa asilimia 4.3 na mwaka 2022 uchumi ulipanda hadi asilimia 4.8 lakini pia makadilio ya mwaka huu uchumi wa Tanzania utapanda na kufikia asilimia 5.3.

Benki ya Dunia inasifu hatua za Serikali ya awamu ya sita katika ufanisi kwenye uchumi, biashara na huduma mahsusi ikitaja maboresho shughuri za utalii, kufunguliwa mipaka ya biashara na mafanikio kwenye chanjo ya uviko-19.

Mbinu alizotumia Rais Samia Suluhu kukuza uchumi ni mara baada ya kuingia madarakani alifanya ziara za kibiashara zinazofungua tija na milango ya kibishara kitaifa katika nchi jirani na mataifa mengine.
 
Back
Top Bottom