Laface77
JF-Expert Member
- Jul 9, 2008
- 2,117
- 2,845
Jana nimesoma memo ya Benki Kuu ya Rwanda wakipiga marufuku utapeli wa kimtandao unaokwenda kwa jina la D9 Club kwa sababu wameeleza ni Pyramid Scheme/Ponzi Scheme ambapo wale waliotangulia huwa wananufaika kwa gharama ya wale watakaoingia kwa kuchelewa.
Kwa kweli naipongeza sana Benki Kuu ya Rwanda kwa hatua hii ya kulinda interests za wananchi wa Rwanda ili watu wengine wasinufaike kwa gharama za watu wengine. Tena wameenda mbali kwa kutaja hata jina la muanzilishi wa hiyo scheme nchini Rwanda pamoja na nchi ambazo huo mtandao umeenea sana ikiwepo Tanzania.
Sasa concern yangu ni kwa Benki Kuu ya Tanzania ambayo mpaka sasa iko kimya kuhusu utapeli huu. Hii hii benki kuu yetu iko kwa ajili ya kusimamia tu sekta ya mabenki na kuyapiga faini pale yanapoenenda kinyume na taratibu za uendeshaji wa mabenki au hata kulinda maslahi ya kifedha ya wanachi wa Tanzania. Ina maana mpaka leo hawajajua kuna utapeli wa aina hii unaendelea mpaka kanchi kadogo kama Rwanda kametuzidi katika hili? Nimeona baadhi ya Benki kama Tanzania Postal Bank na Equity bank zimetoa memo ya kuwaonya wafanyakazi wake wasije kushiriki katika scheme hii kwani ni utapeli na kinyume na maadili. Ifike mahali Benk Kuu ya Tanzania mfanye zaidi ya ku-regulate mabenki, muwalinde wanachi wa Tanzania ambao wengi wao hawana taarifa.
Angalia jinsi wananchi wengi wa Tanzania walivyopoteza fedha na mali zao wakati Benki Kuu ya Tanzania wakiwa kimya tuu. Kuna watu walipoteza hata nyumba zao kwa kuweka dhamana ili wapate fedha za kwenda kupand mbegu DECI. No wonder mkulu jana amewashangaa na kusema pale Benki Kuu kuna PhD 17 lakini hawalioni hili.