Benki gani ni bora?

sasa nyinyi mnahangaika ni nn shida? Mm naona kibubu, au kama pesa zako zinzweza kujaa chumba, chimba nyumba weka. Maana hapo hakuna mlolongo wowote wala makaratasi, huko kote lazima upange foleni na magumashi kibao.

Natamani kukuunga mkono, lakini kila nikifikiria mafuriko kama yale ya December 2011! Mmmh........sipati picha!
Laba kama huishi kuleeeee!!
 
Ndugu zangu i wish kama wote mngekuwa na Akaunti Commercial Bank Of Africa (CBA) muone utofauti. hiyo stress free Banking unayosikia ni ya ukweli kinoma. nawakubali sana hawa jamaa. wamejipanga.
 
Ndugu zangu i wish kama wote mngekuwa na Akaunti Commercial Bank Of Africa (CBA) muone utofauti. hiyo stress free Banking unayosikia ni ya ukweli kinoma. nawakubali sana hawa jamaa. wamejipanga.

Hizo ni benki za mijini huku kwetu hazipo...huku ni NMB, Posta, NBC, CRDB, Barclays na Vicoba.
 
nbc
1. Kwanza ina mtandao mkubwa wa atm kuliko zote- tembelea miji yote mikubwa na midogo utathibitisha
2. Ina mtandao mkubwa wa matawi nchi nzima- sio benki hizi za dar, mwanza na arusha tu achana nazo
3. Ina debit master card (atm card) inayoingia atm yoyote duniani iliyo na mastercard
4. Mastercard yake inatumika kufanya malipo kwenya maduka, supermarkets n.k
5. Ni global bank ina link na benki kubwa za sauz na uk- so international transaction ni kama kutoa fedha mfuko wa kulia na kuziweka mfuko wa kushoto
6. Baadae nitakutajia faida nyingine nyingi za kubenki na nbc

Kwa vigezo hivi mara mia aende CRDB. Tembo Visa yao waweza kununua kitu dukani hata ukiwa nje ya nchi mabali na kuchukua pesa kwenye ATM amabzo zina limit kwa siku. NBC huduma hovyo kabisa.
 
NMB - Benki ya Makabwera

Mkuu hii si benki ya makabwela tena. Nimefika kwenye tawi langu nikakutana na bango mlangoni linaloorodhesha "Bank charges" mpya za kufilisi mtu. Huduma bado ziko chini ya kiwango kwa sana na hawana Visa wala master card kwa hiyo ukivuka nchi tu hakikisha unazo za kutosha mfukoni mwako.
 
nbc
1. Kwanza ina mtandao mkubwa wa atm kuliko zote- tembelea miji yote mikubwa na midogo utathibitisha
2. Ina mtandao mkubwa wa matawi nchi nzima
Si sahihi sana. Ni miji midogo michache yenye nbc, si yote. Na si kweli kuwa ina matawi nchi nzima, llabda kwako kama nchi inaishia ngazi ya mkoa.
Suala la mtandao mkubwa si kigezo cha mwanzisha mada kama hicho kigezo angekiweka, basi nmb inaongoza!
 
Ndugu zangu i wish kama wote mngekuwa na Akaunti Commercial Bank Of Africa (CBA) muone utofauti. hiyo stress free Banking unayosikia ni ya ukweli kinoma. nawakubali sana hawa jamaa. wamejipanga.

Wamepanga kivipi? vipi riba kwenye mikopo? wana lipi ambalo benki zingine hazina?
 
Hahahaaa........wenzio wlaishatoka na hakuna kujizika wala kaburi

So mwizi akifanikiwa kimaisha nawe uanenda unaiba ili ufanikiwe kama yeye..................Hapa tunalenga kusaidiana katika shughuli halali na sio ujanja ujanja wa vijiweni na utapeli...................hao unaosema wametoka iko siku itatokea tu hitilafu kwa kuwa hawa wewe na mimi tulichonacho.........hatua ya kwanza ya mafanikio!
 
Wamepanga kivipi? vipi riba kwenye mikopo? wana lipi ambalo benki zingine hazina?

Ndio wito wangu tangu nianze kuchaia maada hii.................tupeni details msisisfie tu wakati hamjaelezea chochote cha zada walichonacho
 
benki bora au bora benki? mwisho wa siku wengi wetu tunaishia kubenki na benki ambayo aidha uliwahi kuwa na marafiki, ndugu au jamaa humo, ndo benki pekee iliyopo maeneo ulipo, mwajiri wako kakushurutisha uende huko kwa vile na yeye ndo yuko huko. kwa maana nyingine unajikuta kama dini uliyomo...umekuta wazazi wako huko na wewe ukabaki huko huko!
 
i hope swali halitageuka kuwa uwanja wa mabenkist kufagilia benki zao...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom