Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,169
- 3,360
hivi msimamo wa mkapa kuhusu gesi ya mtwara ukoje? m just curious!?
kwake gesi ni yataifa lakini mtwara lazima wanufaike
Pamoja na uchafu wake, namkumbuka Mkapa kwa uwezo wake wa kusimama na kukemea kitu kama mwanamume. Hawa wengine wanaokemea mambo huku wanakenua meno wananikera sana.
watu wengine sijui mtajitambua lini? yaani hata kujua ngedere na tumbiri ni mtu na mpwa wake hamjui? ndo maana wenzako kule wanamsikitikia yule jambazi!Asiye kuwa na kosa aanze kumtupia jiwe,mi nikifanya tathimini huyu jamaa namkubali sana na rafiki zangu wakenya wana sema Ben angekuja baada ya Nyerere tungekuwa mbali sana.Jamani fedha yetu inavyoporomoka thamani kila kukicha kuna aja ya kumkumbuka.Hili weza kuweka mlinganisho wa uchumi ukifanya kazi unaishi vizuri na mshahara wako hali kadhalika ukifanya biashara unaishi vizuri na biashara yako.
huwezi kuwa mnafiki halafu ukawa na ndimi moja!Pamoja na mapungufu yake ila namkumbuka kwa kuwa mtu wa NDIMI moja, akisema ni mwisho na sio kukimbia matatizo kwa kutafuta safari
Akumbukwe kwa nini naye huyo? Kuna tofauti gani ya maisha baina ya utawala wake na ule wa Mwinyi na Kikwete? Rumba bado ni kali tu na Tanzania hatujawahi kuwa na ahueni ya maisha hata siku moja. Na hapo wala sijagusia mambo mengine .
Isingekuwa Mkapa leo hii mngekuwa mnagombea ving'amuzi? wakati Mkapa anaingia madarakani maduka mangapi yalikuwa yanauza tv? kulikuwa na yadi ngapi za magari? hebu acheni kufuru jamani usile ugali wa mtu halafu ukainuka kumchoma mkuki mgongoni nchi ilikwisha na kubakia matobomatobo na pale hazina haukuwepo ht mshahara wa watumishi wa mwezi mmoja. Achaneni na Mkapa kabisa ongeleeni hao walioingia na kuanza kubugia mapochopocho aliyopika Mkapa na mjue wazi tungeendelea na Mkapa leo hii tungekuwa mbali sana tusingerudi nyuma mtapiga kelele hata mpishi kuonja mboga kama ina chumvi ama laa mtasema katafuna chakula cha wageni.
Economically the guy was ok you can't compare with the present one is believing on loans to from up country this is strange presider
Baada ya vyombo vya
habari vilivyokuwa vimenunuliwa na genge la mtandao kumsakama sana kwa
habari nyingi za kumponda. Mkapa aliwahi sema maneno machache sana kuwa
Watanzania tutamkumbuka.
Kwa kweli hali ya nchi iliyopo saizi hakika jamaa tutamkumbuka tu,
tutake tusitake. Nchi kila kitu kinaenda hovyo, na wanaonufaika ni
wachache waliokuwa vinara wa hilo genge. Hakika sipati picha itakapofika
2014 hali itakuwaje. Saizi hela haina thamani kabisa, naamini soon BOT
itaprint note zingine za elfu 20 na elfu 50. Ki ukweli buku 10 haina
thamani tena. Ukishachenji imeisha.
Nchi huwa haiongozwi kwa blabla bali inahitaji commitment ya hali ya juu
sana.
Kila la kheri.....