Benjamin Mkapa on BBC HardTalk (Video)

Benjamin Mkapa on BBC HardTalk (Video)

I like it, Mh. Mkapa alivyomweka sawa kwa hoja mwandishi mzungu mpaka akalainika na ku-conduct a proper interview. Ni ndoto zangu hali hii ya kujenga hoja ikaeleweka kama Mh. Mkapa ingekuwa inapatikana ktk serikali zote za kiafrika maanake aliyepo sasa hivi Afrika ni Mh. Robert Mugabe pekee anayeweza kujenga hoja.

na nyerere aliweza
 
Kwa sasa kuna mtu mmoja yupo hapo KENYA mana ndie rais ambae naamin kwa AFRICA anaweza kujieleza katika public kuliko yoyote yule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka ana uwezo lakini akautumia kulisaliti taifa! Mkapa ni rais aliyekosa uzalendo kuliko wote. Kumbuka wajibu rais ini kuifanyia kazi nchi yake, kila alichofanya chema alitimiza wajibu wake, hakutakiwa kufanya uovu. Niyachukiayo kwa Ben Mkapa:

1. Alimhadaa Nyerere kwamba yeye ni Mr. Clean, mzee wa watu akazunguka nchi nzima kumnadi, kumbe anaamsha aliyelala! Awamu yake ya pili akafanya kufuru ya ufisadi.
2. Ni rais aliyekuwa akithamini watu wa nje kuliko watu wake. Alidiriki kuwatamkia wananchi wake nmaneno ya kejeli mara wanapokuwa na malalamiko kwenye utawala wake e.g ""Acheni wivu wa kike"-wakati akifungua mgodi wa Tulawaka.
3. Mkandamizaji wa demokrasia kwa kutumia vyombo vya dola. mfano. mauaji ya Zanzibar, alidiriki hata kuwapongeza polisi walio ua waandamanaji! Pia alilikandamiza bunge pindi kunapokuwa na hot issues, anaitisha kikao cha wabunge wa CCM na kuwatisha ili kuzima issue.

Wandugu, tunao wajibu wa kulifanyia taifa mazuri si na mabaya pia. Mkapa was too arrogant to be a president....my opinion......kwani hata 1995 nilikuwa najua hilo nasikuthubutu kumuunga mkono...kimsingi arrogance yake niliwahi kuishudia laivu akiwa waziri wa sayansi teknologia naelimu ya juu. Hakuwa na muda wa kuongea na wanafunzi, regardless ya shida yenu.Mkiandamana ni mkongóto tu. Pure mmakonde!
Ninacho jua hakuna mwanadamu aliye mkamilifu lakini ukweli nikwamba ukiondoa Mwalimu Nyerere mkapa ni raisi anayefuata kwa hotuba zenye mvuto na za kujenga hoja. Ni katika kipindi chake ambapo hali ya uchumi ilimarika hata tukaaza kulipa madeni ambayo yalikuwa hayalipiki. Ndipo uimarishaji wa shule za msingi na ukarabati wake ulifanyika, ni katika kipindichake ambapo barabara nyingi ziliaza kujengwa. Kwa watu wa mikoa ya kusini tatizo la kutengwa na sehemu nyingine ya nchi liliisha maana daraja kubwa kwenye mto rufiji(Mkapa bridge) lili jengwa. Tuseme nini kuhusu uwanja wa Taifa na ukumbi wa kisasa wa Bunge? Vipi kuhusu mfumko wa bei ambapo kwa muda wote wa miaka 10 hakukuwa na mabadiliko makubwa ya bei Karibu bidhaa nyingi zilibaki katika bei ileile. Yako mengi Mazuri aliyofanya japo kuwa wengi tunayaona makosa tu. Lakini pia kutokana na unyenyekevu wake alizuia kuwa yeye tusimwite " mtukufu" jina lililokuwa limezoeleka kwa rais aliye mtangulia. Pia hakutaka Picha yake kuwekwa kwenye sarafu ama noti za fedha za Tanzania. Wengine wa naweza ongeza mengine mfano hutuba zake za kutumia misemo ya wanafalsafa mbalimbali n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mmpambe vipi lkn historia ikishaandikwa imeandikwa. Yeye ndiye rais wa kwanza nchini kufanya biashara "Clandestinely" akitokea ikulu kwa kujimilikia mgodi wa Kiwira pamoja na mkewe..!!

Yeye ndiye alikuwa kinara ktk utawala uliogubikwa na ufisadi kama wa Epa, Meremeta, Radar, Uuzaji mashirika ya umma na Nyumba za serikali kwa wapambe wake na hatutamsahau kwa kufanya Tanzania izalishe wakimbizi wa kwanza baada ya mauaji ya Zanzibar ya 2001. Ana "Legacy" mbovu sana huyu bwana.
 
Nina mashaka na wewe kuwa hujui kiingereza Kama bwana wenu mwenyekiti
*LISSU ATAABIKA SANA, AISHIA KUAIBIKA LONDON, ABANWA VIKALI NA KUTOA MAPOVU*

_NA Mwamba wa Kaskazini_

Leo ndio msemo kuwa Kiingereza sio maarifa umethibitika.

Tundu Lissu ana uwezo wa kutosha tu kuongea Kiingereza lakini asubuhi ya kuamkia leo kukosa maarifa kujawa na umbea, uongo na uzushi na uzandiki dhidi ya nchi yake kumemtokea puani akifanya mahojiano na Kipindi cha Hard Talk cha BBC.

Sikiliza haya.

*1.Aonesha Chuki Binafsi Kwa Magufuli*

Kosa la kwanza ni kutojadili hoja bali mtu.Kila alipoulizwa aliishia kutaja jina la Magufuli hata asipohusika.

Mtangazaji mzungu akabaki anashangaa na kumbana kwa maswali zaidi akaishia kutoa macho maskini.

*2.Lissu Hakutegema*

Hakika hata mimi sikutegema kama yule mzungu angefanya utafiti kiasi kile na kuyajua mengi ya Tanzania kiasi cha Lissu mwanzoni tu kubabaika na kuanza kuzusha uongo.

*3. Jaribio la kumdanganya Mzungu lakwama*

Baada ya kuzoea kuandika viwaraka vyake na kuwapa akina Martin Malera wa Tanzania Daima au Ibrahim Yamola wa Mwananchi leo Tundu Lissu kakutana na mwanahabari wa level nyingine.

Akajikuta anakosa ushahidi...anaambiwa unalalamika kila siku Serikali imekushambulia, unaushahidi gani anasema niliona gari inanifuatafuata, mzungu akambana kwani gari ziko ngapi na mtu yeyote si anaweza kukufuatilia kwani umeshafanya kazi ngapi za kukuweka katika risk ikiwemo kuwa wakili, Lissu akajikuta anakiri kuwa ni kweli hana ushahidi wa moja kwa moja bali ushahidi wa mazingira.

Asante sana mzungu, huyu Bwana leo baada ya mbwembwe nyingi sasa kakiri hana ushahidi zaidi ya mazingira tu ambayo pia yanaweza kuonesha chama chake kinahusika au hata dereva wake.

*4.Akosa maarifa kwenye madini*

Maskini hapa ndio jamaa alitoa mimacho tu baada ya mzungu kumbana kuwa yeye alipigania sana masuala ya nchi kufaidika na madini haoni kuwa JPM anachukua hatua nzuri?

Kwa hakika na mimi hapa nilipoteza Kiingereza changuSikumbuki hata Lissu alikuwa anajibu nini, aliishia maskini kutaabika na kuruka ruka huku na kule.Mzungu akaona isiwe shida, akahamisha mada!

Kwa kifupi hapa Lissu alijikuta anatamani kumpinga Magufuli, lakini pia akawaza anampinga kwa lipi?Kurekebisha mikataba ili nchi ifaidike? Akabaki anataja taja tu majina mara uwanja wa ndege Chato wakati nchi nzima vjwanja zaidi ya 15 vinajengwa

*5.Mtangazaji aamua kutaja mwenyewe mazuri ya Tanzania.*

Baada ya kuona Lissu hana analolikubali katika nchi yake mzungu wa watu akaamua kutaja mwenyewe mageuzi makubwa yanayoendelea Tanzania.

Akataja mapambano dhidi ya rushwa, akataja kuongezeka kwa mapato akataja kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya kijamii na miundombinu.

Usiniulize wakati wote huu mzungu anashusha nondo Lissu alikuwa kwenye hali ganiKumbuka mwenyewe kisa cha chura aliyebanwa na mlango

*6. Atoa mfano wa kitoto, wamuumbua*

Akieleza kwa nini wapinzani wenzake wamekuwa wakirejea CCM kuunga mkono juhudi za JPM Lissu aliishia kirusha matuhuma ambayo hadi mtangazaji akamuonya aache kuropoka bil ushahidi.

Lakini yotrme hii ni kwamba alishachanganyikiwa. Sasa sikia hii: akapewa mfano wa Masha aliyetoka CCM na kwenda upinzani (ingawa badae alirudi CCM) kama naye alihongwa huko upinzani? Usiniulize Lissu alikuwa katika hali gani hapa tena

*7.Akata fahamu, aunga mkono ushoga*

Akiwa hoi bin taaban na kisaikolojia akionekana mtu anayetamani mahojiano yaishe tu, Lissu akaulizwa ukiwa kiongozi wa upinzani na siku ukiingia Ikulu utafuta sheria zinazoelezwa kuwa kandamizi zinazoufanya ushoga kuwa kosa la jinai?

Maskini, mwisho wa zama ukatimia, baba la watu likajikanyagaaaa mwishowe likaingia kingi eti litafuta sheria zote zinazozuia ushoga nchini.Maweeeee

Rasmi Lissu kaunga mkono ushoga. Hakika ametaabika sana.

Kwa nini utaabike lakini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Nimeinyaka video ya mahojiano (mwaka 2001) kati ya Mhe. Mkapa na kile kipindi cha BBC HardTalk.

Kweli hii ilikuwa "HardTalk" kwani jamaa walimbana acha.

Waweza kuitazama kupitia link hii:

Compare to Lissu"s interview
 
Huu upuuzi wako hata ukijadiliana na mkeo atakuona fala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom