Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

CCM mmezidi sasa,mambo ya nchi kuzungumzia makanisani haileti maana hata kidogo!NYERERE AKIWA NA JAMBO LA NCHI, ALIKUA ANAITISHA PRESS CONFERENCE MSASANI
 
Wakati mwingine huwa napatatwa na wasiwasi wa uwezo wetu wa kufikiri, ben kwa kikwete? Sikatai jk kama mtu mwingine anamapungufu lakini siyo ya ben, wakati wa ben majambazi yalifanya tz shamba la bibi,haukuwekeza hata sent kwenye umeme balaa lote jk akalirithi angalia anavyopambana nalo,ndio kipindi watendaji wa serikakini walipojeuka miungu watu na tulipohoji akatwambia tuna wivu wa kike, mpasuko wa kidini ulichipua zaidi sasa hvi ni matokeo tu,mmesahau pareto aliyounda kwa ajili ya kutoa msamaha kwa wafungwa,waislam wakaja juu wajumbe hamsini wote wakristo, akauwa waislam mwembe chai pengo akampongeza bora kuua kumi nchi ibaki na amani, na mengine mengi tu.......... Mkapa ndiye raisi kilaza kuliko wote tz

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Sasa yeye kamuua nyerere na jk anawatesa wakina ulimboka lipi la kushangaza
 
mkapa na jk woote kwa kizanaki tunasema amanji ga nyanja!!!!!!!
 
huyu jamaa alikuwa mtemi aisee daaah akheri huyu kuliko dhaifu .......nakubaliana na mdau hapo juu alichochemka huyu jamaa ni kumuachia kikwete nchi .......hapa alichemka sana
 
Huyu mkapa yeye ndiye alie panda mbegu hata wazanibar aliwauwa asijisafishe ccm inamlinda asiende theheg
 
He is the one who starts to pull our nation buck,majanga yote yaliyoshamiri kwa sasa chanzo ni uongozi wake,asije jifanya kuhepa kivuli chake,yeye ndiye source kwa kuanzisha tabia ya kudharau WATANZANIA na kuziba masikio kutopokea ushauri.NA MBAYA ZAIDI MIKONO YAKE IMEJAA DAMU YA WAZANZIBAR.Sasa aona Taifa lazama anataka ruka kimanga.

ni kweli ila aliyempokea ameshindwa kuonyesha tofauti zaidi ya kuweka mbolea kwenye mapungufu ya ben, na kuanzisha mapungufu mengine makubwa.
 
Wakati nyerere amemwachia mwinyi, mzee ruksa akafungulia yote watu wakasema huyu ni bora,lakini mwishoni wakamchoka, wakati anatoka akasema mtanikumbuka, alichukua Ben watu wakamyea na kusema bora ya mwinyi kuliko huyu,waislamu wakasema ni adui wa dini yao. Sasa yamemkuta kikwete, akijenga barabara tunaambia ilianzishwa na Ben, akiboronga tunaambia mbovu. Mimi naona wenye matatizo ni sisi watanzania.Hakuna kiongozi hata mmoja aliekubalika kwa wananchi wote.
 
Hata kama Mkapa alikuwa fisadi na kuanzisha AnBen Company akiwa Ikulu lakini hakuruhusu madudu tunayoyaona sasa ya udhaifu wa kiongozi na kulikuza ombwe la uongozi Tanzania. Alichukua hatua mara moja. Rekodi ya serikali ya Mkapa kiutendaji iko mbali sana ukilinganisha na hii ya Kikwete. Thibitisheni. kwa kutoa mfano wa sekta moja tu iliyostawi katika miaka 8 ya utawala (ambao hauwezi) wa Kikwete.

Acha kujisahaulisha hivi wakati wa mkapa yaliotokea umeyasahau kahesabu makuburi ya walio kufa pemba na wengine kuwa wakimbizi jk na udhaifu wake lakini bado haijafika hali ile
 
Mhhhh! Nawe wasema? Ni bora ndugu kugombana, wakipatana maisha yanaendelea. Je Madini yetu tutayapata tena, baada ya hiyo miaka 999 kuisha?. Kaka wewe nyamaza tu. ACHA KATIBA IENDELEE KUKULINDA.
 
Hata kama Mkapa alikuwa fisadi na kuanzisha AnBen Company akiwa Ikulu lakini hakuruhusu madudu tunayoyaona sasa ya udhaifu wa kiongozi na kulikuza ombwe la uongozi Tanzania. Alichukua hatua mara moja. Rekodi ya serikali ya Mkapa kiutendaji iko mbali sana ukilinganisha na hii ya Kikwete. Thibitisheni. kwa kutoa mfano wa sekta moja tu iliyostawi katika miaka 8 ya utawala (ambao hauwezi) wa Kikwete.

Sekta ya udini imestawishwa vema tangu mwaka 2005 na sasa mavuno yameanza polepole.
 
Wa kuiweka sawa Tanzania ni magufuli peke yake.Ni mchapakazi,mbabe na sio mwizi. Huyu ndio nyerere,mwinyi,ben na kikwete combined.
 
Ahsante sana Mkuu TIMING. Jamaa ni mnafiki sana huyu anataka kujitakasa mbele ya jamii ya Watanzania wakati madudu yake ya ufisadi aliyoyafanya akiwa Ikulu hadi leo anayaficha. Yuko tayari kuongelea chochote kile with exception ya ufisadi wake mkubwa wa mabilioni ya pesa alioufanya akiwa Ikulu.

yawezekana kabisa baadhi ya mbegu za kibaguzi na social injustice alizipanda au hata kuzimwagilia yeye, hasa ufisadi

ni rais wa ajabu anayefungua co. ltd akiwa ikulu na kutumia anuani ya ikulu

He cant escape responsibilities for what we are now as a nation
 
Last edited by a moderator:
amaah!
tuwekeni vigezo vya kuwapima hawa viongozi ili tujue yupi ni afadhali.
pia tuzingatie mahitaji ya taifa kwa nyakati
 
Mzee Mkapa alisimamia vizuri uchumi lakini aliuza nyumba zetu na baadhi ya Mashirika yetu ya Umma ambayo hayakuwa na umuhimu mkubwa wa kuyauza.
Mh Kikwete anasimamia ukuaji Demokrasia. Tunapayuka tupendavyo hata kama anatupuuza. Anakuwa mzito wa kuchukua hatua za haraka za kutatua migogoro ya kijamii inayoliandama Taifa. Kila mmoja atakumbukwa kwa aliyoyafanya na aliyoyapuuzia pia.
 
alichofanikiwa ni kuvinyima vyombo vya habari uhuru wa kuripoti maovu ya serikali yake hivyo kwa baadhi ya watu kutoyatambua kirahisi.
 
Mzee Mkapa alisimamia vizuri uchumi lakini aliuza nyumba zetu na baadhi ya Mashirika yetu ya Umma ambayo hayakuwa na umuhimu mkubwa wa kuyauza.
Mh Kikwete anasimamia ukuaji Demokrasia. Tunapayuka tupendavyo hata kama anatupuuza. Anakuwa mzito wa kuchukua hatua za haraka za kutatua migogoro ya kijamii inayoliandama Taifa. Kila mmoja atakumbukwa kwa aliyoyafanya na aliyoyapuuzia pia.
 
Haya ni kama mambo ya kila Mzee wa zamani kudai kuwa Enzi za kusoma kwake alikuwa akishika nafasi ya kwanza. Wa mwisho alikuwa nani?
 
Back
Top Bottom