Bendera ya China kupelekwa mlima Kilimanjaro

Bendera ya China kupelekwa mlima Kilimanjaro

Queen Esther

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
2,206
Reaction score
1,464
Wana JF naamini hamjambo!

Kwasababu JF ni kisima cha maarifa, na ni jukwaa la great thinkers naomba mnisaidie jambo moja.

leo katika matangazo radio clouds wamesema kesho bendera ya China inapandishwa mlima Kilimanjaro? Jambo hili limenistua nikawa na maswali mengi baadhi ni Kama yafuatayo:-

- Je inapandishwa huko kufanya nini? For every reaction there is equal and opposite reaction. Sasa malengo hasa ni nini?
- Baba wa Taifa kupitia baba yetu Marehemu Nyirenda alipandisha bendera ya TZ kwa ajili ya UMOJA, AMANI, UTULIVU nk
- Kwenye ulimwengu wa Roho hili jambo lina maana yake. Basi mpango wowote muovu Mungu aubatilishe, TZ ni ya watanzania.
- Na Kama mpango ni mzuri na utakuwa na faida kwa watanzania basi na usimame.
- Kama kuna viashiria vyovyote vya ushirikina basi basi Mungu avibatilishe. miungu ya kigeni hatuitaki TZ.

Kama nimekosea basi nisamehe na panapohitaji marekebisho au mchango basi UZALENDO wako utumike.

Queen Esther
 
Hii ndo serikali ya ccm.. Wameshauuza tayari. Hivi term hii nani kakamatwa na unga kule.
 
safi

hii ni katika.kutekeleza masharit ya mikataba 29 aliyosaini mh rais jk na yule wa china
 
Inapandishwa hili kuwaangaza Tembo popote alipo hapa nchini. Pia wanakwenda kuangalia kama huko mlimani kuna chochote cha kuiba.
 
Yapaswa utambue kuwa tanzania ni jimbo mojawapo la nchi ya china,ndiyo maana wachina wamejazana hapa na kufanya watakalo biashara za umachinga kkoo ni za kwao,maliasili zote za kwao,biashara za ma bus kama NEW FORCE ni ya kwao,gereji ni za kwao serikali ipo mfukoni mwao.CCM inawalinda kwa nguvu zote
 
Wana JF naamini hamjambo!

Kwasababu JF ni kisima cha maarifa, na ni jukwaa la great thinkers naomba mnisaidie jambo moja.

leo katika matangazo radio clouds wamesema kesho bendera ya China inapandishwa mlima Kilimanjaro? Jambo hili limenistua nikawa na maswali mengi baadhi ni Kama yafuatayo:-

- Je inapandishwa huko kufanya nini? For every reaction there is equal and opposite reaction. Sasa malengo hasa ni nini?
- Baba wa Taifa kupitia baba yetu Marehemu Nyirenda alipandisha bendera ya TZ kwa ajili ya UMOJA, AMANI, UTULIVU nk
- Kwenye ulimwengu wa Roho hili jambo lina maana yake. Basi mpango wowote muovu Mungu aubatilishe, TZ ni ya watanzania.
- Na Kama mpango ni mzuri na utakuwa na faida kwa watanzania basi na usimame.
- Kama kuna viashiria vyovyote vya ushirikina basi basi Mungu avibatilishe. miungu ya kigeni hatuitaki TZ.

Kama nimekosea basi nisamehe na panapohitaji marekebisho au mchango basi UZALENDO wako utumike.

Queen Esther

Bendera iliyopandishwa pale ilikua ku-symbolize pride na value zetu kama taifa.

Leo China wanapandisha pale kwa reason zipi zenye ushawishi kwa maslahi ya nchi na bara la Afrika?

Kwa kuzingatia malengo ya kupandisha bendera yetu siku ya uhuru,now our sovereignity as a state is at stake !
 
Nashindwa cha kuchangia kwa kuwa sijajua lengo la upandishwaji huo wa bendera...
 
Kwani watalii huwa wanatoka jasho wakipanda kule..sidhani kama wanahitaji leso ya kufutia jasho hawa watu wa magharibi kule pick
 
Wachina washatuona ma.fa.la sana. Wanafanya chochote kama wapo kwao. 2015 .... na familia yake wakaombe hifadhi China na wasirudi milele.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Waaaaaaat?? Bendera ya china mlimani! Tumekwisha,nchi imeuzwa hii!! Wadau mnakumbuka yule baloz wa china aliepiga kampen na kinana? Sasa wachina wameshatuchungulia vya kutosha...au gesi waliopewa haikutosha?
 
Hadi mlima umebinafsiswa! Ni siku tu utaskia watz wote wamebnafsiswa! Chezea Mzaramo we!
 
utakuwa ni wendawazimu kuwaruhusu wachina wapandishe bendera yao mlima wetu uliotukuka.
atakaerhusu inabidi akapimwe akili kama ziko sawa.
baba wa taifa alikuwa na maana kubwa kusema bendera yetu ipelekwe pale wakati wa uhuru
hiki ni kituko cha mwaka
kwa wali marangu geti hadi horombo mkiwaona hawa na bendera yao watimueni mbali ichomeni moto kabisa
 
Bendera ya China ipepee Mlima Kilimanjaro?!?!? Wanajukwaa mlio na taarifa kamili juu ya hili tafadhali elezeni.
 
msiogope,watanzania wote, hakuna chochote kitakachofanikiwa,pale mlimani wachina na mapepo yao watakiona cha mtemakuni mlima wote watu wa mungu walisha mkabizi [mungu wa mbingu na nchi] msiogope hakuna mungu mgeni atakaye simama mbele ya [mungu wa mbingu na nchi]
 
Back
Top Bottom