Magazine Fire
JF-Expert Member
- Dec 28, 2011
- 1,364
- 1,475
kama hili ni kweli na watanzania tunalifumbia macho basi kinachofuata wachina wataweka bendela yao magogoni. haya yote yanawezekana tu kwenye nnchi ya mamburura na si vinginevyo.
Bendera ya nchi nyingine hupepea kwenye ofisi ya Ubalozi tu na si vinginevo!
Kwa maana hiyo Bendera ya Tanzania huko China inatakiwa kupepea kwenye ofisi ya Ubalozi wa Tanzania na siyo kwenye Mlima Everest(The highest mountain in the World).
Likewise Bendera ya China hapa Tanzania inatakiwa ionekane ikipepea kwenye Ofisi za Balozi wa China nchini Tanzania tu! Kinyume cha utaratibu huu wa Kibalozi ni sawa na kutangaza KOLONI la nchi yenye bendera kama haiko kwenye ofisi za Ubalozi!!
Kwa kitendo cha China kupeleka Bendera kwenye Mlima Kilimanjaro ni sawa na China kutangaza kuwa Tanzania ni Koloni la Wachina. Huo ni ukweli na ndiyo maana yake. Ndugu Watanzania tumesikia mengi sana kuhusu Wachina ndani ya Tanzania kuanzia bidhaa feki, biashara za Madawa ya Kulevya,Biashara ya Pembe za Ndovu na Faru na zote zikiwahusisha Wachina!!!!!
Kama Watanzania tuna akili timamu basi kwa umoja wetu na mshikamano wetu lazima tupinge kitendo hiki kwa nguvu zetu zote. Naomba Viongozi wa Upinzani hasa CHADEMA kuandaa maandamano ya nchi nzima kukataa hii aina ya Ukoloni mpya wa Kichina!
Tumechoka.................!!!!