Benard Saanane jisafishe haraka; atoa maelezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benard Saanane jisafishe haraka; atoa maelezo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taifa_Kwanza, May 30, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rafiki Bernard Saanane

  Nimejawa na masikitiko makubwa sana baada ya kupata habari za kuenguliwa kwako
  kwenye kinyang'anyiro cha Uenyekiti wa BAVICHA kwa sababu za kukiuka maadili ya uchaguzi.

  Kitu pekee kinachonipa faraja ni kwamba kama binaadamu, Mwenye Mungu ameishaweka
  msimamo wake juu ya makosa yote tuyafanyayo, kwamba Tukitubu na kuomba msamaha
  atatusamehe hata tukiwa tumechafuka na kuwa wekundu kama damu.Nafarijika sababu
  natambua kwamba unanafasi ya kutubu na kusamehewa, Ni mategemeo yangu kwamba
  utaitumia fursa hii adhimu.

  Naleta maombi haya kwako, kwamba zaidi ya kuomba msamaha kwa Mwenye Mungu, uje
  pia hapa jamvini na kuomba msamaha, sio kujitetea - sababu sisi hatuna mamlaka ya kuku
  samehe wala kufanya maamuzi yoyote juu ya maswahibu yaliyokukuta,lakini kwa nafasi
  uliyokuwa nayo katika mioyo ya watu wengi hapa jamvini, kutokana na misimamo, itikadi,
  ufahamu, uelewa, uungwana na machungu uliyotuaminisha kuwa nayo juu ya mstakabali
  wa nchi yetu umetuacha vinywa wazi kwamba hata wewe ulikuwa radhi kukiuka taratibu
  za uchaguzi ndani ya chama chako ili upate ushindi.

  Nasikia ulifikia hatua ya kusema unaweza kujitoa, sina hakika kama ni kujitoa kwenye
  chama au kwenye uchaguzi, kama ni kweli ulitoa kauli na ya namna hii basi inaonyesha
  kwamba utoto bado unakusumbua.

  Nisikuchoshe kwa maneno mengi sana, lakini nakukumbusha wajibu wako wa kurudi hapa
  jamvini na kutuomba msamaha sababu wakati unatangaza nia, uliweka hapa maelezo yako
  ya kina, yenye kuvutia na kutia moyo juu ya uwezo wako wa kuwa kiongozi.

  Naomba utambua kwamba nakuandia wewe sababu ni wewe pekee ndiye uliyetabulika
  hapa kama mgombea huko BAVICHA, wengine sikuwaona, hao watawajibika katika
  communities ambazo waliziamisha kuwa ni tunu kwa taifa letu.

  Jitie nguvu kama Mwanamme uombe msamaha, maisha yaendelee.
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Dikteta Saanane kaondolewa kabla ya kuingia kwenye kura.tumekaa tukafurahi,AENDE AKAGOMBEE UENYEKITI WA VIJANA WA ODM KENYA.AKAMSAIDIE KIPENZI CHAKE RAILA ODINGA.HECHE KUWA MAKINI NA HUYU ATAKUPINDUA.Hakikisha mnamdhibiti kweli kweli ​
   
 3. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtihani mgumu huo uliompa,jamvi lenyewe analiona kama kituo cha polisi, na hayupo peke yake. yupo mwingine alikuwa "mbele sana" kumbe alikuwa anatafuta ngazi ya kupandia.wote wamepigwa chini na wamelikimbia jamvi.njaa kali mwanangu si mchezo.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Don't be a cheap politician! Ben sometimes remaining silence is gold and talking is Silver!!
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  It is not the end of the world .... we still need to eat and prosper .....!
   
 6. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani ameongopa? hawakujinadi hapa jamvini kuwa ni watu weupe kama malaika,sasa kama wamegundulika kuwa na "Damu" kwa nini wasioge. ni Topic muafaka kabisa unataka tu kupindisha mada.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kumbe siasa na wanasiasa wanafanana sana na haijalishi chama watokacho

  Hebu angalia CHADEMA youths wanavyo-emulate wenzao wa CCM, halafu mnategemea tuone ninyi ni bora... Member anajiita nuclear one kashindwa hata kuficha upumbavu wake... yaonyesha hata wa mama ake na babake hawei kuuficha kwani yeye ni kama kawa la kufunikia lunch, limechapishwa maandhishi in bold, very colourfull

  poor thang!!

  HUU NI UPUMBAVU MKUU, YA CHAMA MALIZIENI HUKOHUKO!!!!

  Ben, Heche na wote mliokua pale, funikeni ujinga wa upinzani, fanyeni kazi mtangulizeni Mungu.... mkifanya hayo, wapumbavu kama Nuclear1 watakimbilia kwa dovutwa!!
   
 8. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Acheni kumsumbua huyu kijana uchaguzi umeshapita, hakuna malumbano. Aliyekuwa anatafutwa kesha patikana, tumpe ushirikianao aliyeshinda. Ben usikubali kurubuniwa na kuropoka ovyo endelea kujenga chama kwa nguvu zote usikate tamaa. Watu wanataka uropoke wakunukuu kesho na kesho kutwa ushindwe kufanya kitu kingine. Achana nao heshimu yaliyotokea mpe ushirikiano aliyeshinda, nafasi za uongozi hazijakwisha Chadema.

  Tena nikupongeze kwa hatua uliyofikia ni nzuri sana umma wawatanzania unakuangalia uwe mvumilivu. Hata yule mbaya wako unaedhani kakukasirisha jaribu kumvuta awe rafiki yako, usikubali kuonyesha hisia fulani za malalamiko komaa ndugu yangu. Lingine uwe makini na marafiki inawezekana haohao marafiki zako ndio wamekuchomea au wamekushawishi na wewe ukaingia kwenye mtego lakini wewe hujui. Wao walikuwa wanajua unavunja sheria ili usiingie kwenye ulingo sasa na wewe hukuhamaki kuwa sheria ni msumeno.
   
 9. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,754
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Huyu Bernard 2 O'CLOCK ndio nani???
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  nami namshauri Ben sanaane aachane na malumbano yasiyo kichwa yanayotaka kuibuliwa hapa. ni kweli nafasi za uongozi hazijaisha cdm pia kuijenga cdm c lazima uwe mwenyekiti bavicha. so kubaliana na matokeo, mpe support aliyeshinda pigeni kazi mpaka vjjni ndani kabisa watu waijue cdm na sera zenu. 2015 inakuwa kama kumsukuma mlevi
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Wewe ni pandikizi unadhani kwa kutoa maneno hayo utamtrap Ben,kwani yeye alivyoingia kwenye uchaguzi unadhani hakutumia five senses zake anajua aliingia kwenye uchanguzi kuna kushinda na kushindwa,Chadema ni Imara hata vijana wake ni jasiri na wako imara uchaguzi umeisha wote waliogombea watakaa chini kuangalia jinsi watakavyowatumikia watanzania na Kuikomboa nchi hii kutoka kwa wakoloni mambo leo CCM ,toa upupu wako hapa umetuma katika kila thread maneno yako ya kijinga,pandikizi weee
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi vitoto vijinga kama nuclear1 vinatia kinyaa
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Degree za India hizi! What a waste?
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  May 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Taifa_Kwanza na WanaJF kwa ujumla,

  Kwanza kabisa naomba Moderators Msihamishe hii thread au kuunganisha na Nyingine.

  Nashukuru sana kwa sababu nimeona Jf kuna waungwana, wachambuzi wa mambo na watu wasiosukumwa na ushabiki. Pia katika mchakato huu wa Uchaguzi, nimeshuhudia mambo mengi ambayo hata ninyi mngeyashuhudia nahisi hata fikra na mitazamo yenu ingebadilika.

  Hii thread nimeona nichangie kwa sababu ina hamu na imeonyesha jitihada za kutafuta ukweeli lakini hata hivyo ni lazima nizingatie Umoja wa Chama chetu kwanza. Maadui wetu wa kwanza ni CCM na sera zake mbovu. Nataka kujiepusha na harakati zote za kukigawa chama chetu, nazingatia Maslahi ya taifa letu na tumaini la watanzania wanaotegemea CHADEMA kama tunu kwao katika kulikomboa taifa letu.

  Siku zote mimi ni muumini mzuri wa kanuni. Kama chama kimeona nimekiuka kanuni, basi ni lazima niwajibishwe. Tujiulize au naomba kuulizwa katika muktadha wa kidemokrasia, je Saanane umekiuka kanuni za uchaguzi?

  Mazingira ya kuvunja kanuni: Niliunganisha nguvu na wagombea wenzangu wawili. Kanuni tata iliyovunjwa ni ile ya kukataza kampeni kabla ya muda.

  Tulijadili namna au uwezekano wa kuunganisha hoja zetu ili tumpigie kampeni mgombea huyo ashinde. Wakati huo huo mimi nikiwa tayari kujitoa lakini nimsaidie mgombea mwingine.

  Lengo langu si madaraka, mimi si mroho wa madaraka. Ninaipenda Bavicha na ninakipenda chama changu. Katika kuunganisha kwetu nguvu, tulizingatia utayari wa mwenyekiti mtarajiwa kushaurika na mwenye kubeba haiba ya chama katika sura ya Kitaifa ili vijana wote wajisikie kwamba BAVICHA ni sehemu yao.

  Lengo kuu la Bavicha ni kuratibu, kuhamasisha miundombinu na raslimali katka mchakato huu wa mabadiliko kupitia vijana wote Tanzania kwa ajili ya kuking'oa chama cha Mapinduzi. Nilizingatia hilo, Bavicha ni kubwa kjuliko Saanane, ni kubwa Kuliko Greyson na ni kubwa kuliko kiongozi au Mtu yeyote ndani ya chama Chetu.

  Hapa wazo langu lilikuwa ni maslahi ya Bavicha kwanza, maslahi ya vijana kwanza. Kama ni kuwa mateka basi nilishikwa mateka na hisia zangu za kutaka kujitoa sadaka kwa ajili kujenga uongozi wa Bavicha uliotukuka.

  Mengi yamesemwa, mengi yameandikwa kwa nia haramu na halali. Wapo waliopandikizwa hisia chafu kimaslahi zaidi. Hili siwezi kulijadili kwa sasa, haitakuwa jambo la busara na sababu ninazo tena nzito tu.

  Sasa kama kujadili namna ya kuunganisha nguvu ni kampeni, basi nakubali nilikiuka kanuni naomba nisamehewe. Najua wana JF mlikuwa na imani sana na mimi, naomba imani hiyo muendelee kuwa nayo.

  Sijawahi kukisaliti chama changu kama inavyopandikizwa kwa nguvu zote na baadhi ya watu ambao wasiojiamini, waliofunikwa na ushabiki na ombwe la fikra.

  Kupitia uchaguzi huu nimeamini sisi kama taifa tuna demokrasia yetu ni changa.


  Nilipotangaza kwamba naunganisha nguvu na wagombea wengine, na niko tayari kuitoa sadaka nafasi yangu ya kuwa mwenyekiti, vijana wengi waliumia, walilia, walisononeka kwani walikuwa na imani kubwa nami.

  Wengine walisema umetusaliti, wengi sasa wamenielewa ila tu natoa wito kwao waendelee kushirikiana na uongozi uliopo. Bavicha ni kubwa kuliko ubinafsi wetu.

  Lakini niwahakikishie, dhamira yangu ni njema na roho yangu ni safi. Nitaendelea kuipigania demokrasia ndani ya chama chetu ili tuzidi kukomaa na ili tuwe mfano kwa vyama vingine si ndani ya Tanzania tu na hata Afrika kwa ujumla.

  Vyombo vya habari vinatoa matamko au habari ambazo ni General sana. Naheshimu sana Tasnia ya habari katika kukuza demokrasia, nasizitiza Sikupewa fursa ya kujinadi na kujenga hoja mbele ya wapiga kura kwani ilionekana nimekiuka maadili.

  Kwa hiyo sijashindwa uchaguzi, sikuingia katika sanduku la kura kwa kuwa nilituhumiwa kukiuka maadili.
  Naomba niishie hapo kwa sasa.

  Je tuhuma zote juu yako ni za kweli? Je, Mazingira ya uchaguzi yalikuwaje?

  Tuhuma za Rushwa si kweli, ila pia naona waandishi wengine wamekuwa General sana. Wamemnukuu katibu mkuu vibaya kwani hata yeye alisema hakuna tuhuma zozote zilizoletwa juu yangu kuhusu hili.

  Mimi ni mkweli, sijwahi kutoa rushwa, labda rushwa ya hoja.

  Tuhuma za Kupokea wajumbe: Sijawahi kupokea wajumbe.

  Tuhuma kama hizi msingi wake ni nini?

  Kuwagawa vijana kimakundi: Sasa tafsiri ya kuwagawa vijana ni nini? Mimi sina makundi, labda kundi ambalo liliniunga mkono ambalo si kundi Rasmi. Hata wanaJF walionipa imani ni miongoni mwa kundi hilo.

  Sasa utagombeaje uongozi kupitia mchakato wa kidemokrasia kwa kushindana kwa hoja bila kuwa na kundi litakalounga mkono hoja zako? Hili ni suala litakalojadiliwa ndani ya chama chetu ili tusonge mbele.

  Tafsiri tata kama hizi zinatumiwa vibaya kwa makusudi au kimkanganyiko (comfusion) katika kukandamiza demokrasia, ni suala litakalojadiliwa ndani ya chama. Nimeweka sawa upotoshaji unaofanywa

  Je kujitoa katika uchaguzi ni kosa? Natambua kama mwanasiasa wafuasi wangu walikuwa na imani na mimi katika kusimamia hoja nilizokuwa nazo kwa ajili ya Bavicha.

  Katika maaamuzi niliyofikia nilizingatia maslahi ya chama, BAVICHA na vijana wa Tanzania kwa ujumla katika harakati zetu za mabadiliko

  Sikuwahi kushiriki katika hila za Rushwa, Vurugu (Kama ninavyoona jitihada za kuniunganisha katika hilo). Kwanza hilo ni kosa la jinai, nalaani mpango huo haramu wa kutumia vurugu na vitisho, hiyo si Demokrasia

  Tuhuma za kuwa pandikizi: Hilo nitalijadili, misimamo yangu haitaweza kuruhusu mimi kutumika hata kidogo, tuhuma hizo hazinihusu, kama yupo anayenihusisha nazo basi ana ajenda yake. Msiimamo yangu ipo wazi, siku zote napinga kuwa mateka wa kifikra.

  Kuna mambo mengine ambayo ningependa tuyajadili ndani ya chama chetu.Tafadhali sana naomba mvute subira kwa hili. Ila sitaki kutoa siri za vikao.

  Mapenzi yangu kwa CHADEMA hayana kipimo, mapenzi yangu kwa Tanzania hayana Kipimo.

  Naomba niishie hapa kwa sasa, kwani naelekea maeneo ya Sabasaba kwa ajili ya kuweka mambo sawa na kuponyesha majeraha yaliyotokana na uchaguzi huu.

  Nipo katika jitihada hizi kwa utashi wangu na kwa mapenzi mema ya chama changu. Tafadhali nivumilie
  ni katika hili.

  Naomba mnisamehe kwa makosa yoyote ya spelling kwani nimeandika haraka haraka

  Asanteni sana.

  Nasizitiza sijawahi kukisaliti na sitakaa nikisaliti chama changu, sijatawahi kuwa mateka wa kifikra wa mtu yeyote.

  Youths for Radical change
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Unajua wamekuwa kwa kipindi kirefu wakileta udaku kutaka kuchafua jamvi ambalo watu wengine limekuwa kama chuo kikuu kwetu unachukua,maarifa na ufahamu wa hali ya juu katika jamvi hili,sasa yeye anakuja na personal assination,kwa mgomea kwa vile wanamuona yuko strong labda sijui,lakini baada ya ushindani mshindi na washindwa si wanarudi meza mmoja na kuendeleza libeneke la chama chao kwa manufaa ya wananchi,sasa anakuja mtu mmoja anasambaza post moja katika kila thread iliyofunguliwa hata ukimchukia mtu huna naamna nyingine ya kumwambia si amupelekee PM Ben tujue moja
   
 16. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  do you have a point??
   
 17. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ninashangazwa sana na watu wanaolazimisha dogo asiweke mambo sawa hapa jamvini.
  Kwenye maelezo yangu nimemuelekeza kwamba, asijitetee, nikitambua akichukua njia
  hiyo hawezi kuiepuka dhambi ya majibizano hadharani, na nimemuelekeza kwamba
  atuombe msamaa wana JF AS A COMMUNITY, na sio wana CHADEMA
  kwa vyovyote vile huko ziko njia nyingine za kuweka sawa mambo pindi yanapofikia
  au yanapojili mambo kama hayo yaliyomkuta Ben.

  Pia ikumbukwe, nimemuambia yeye specifically kutoka ha heshima tuliyoanza kumpa
  mahali hapa, Hivyo naomba niongeze kwamba, tunaomba atuheshimu pia kwa kutokaa
  kimya.Hivyo namsihi tena ajitokeze, kukaa kimya kutafanya ionekane ni kweli sasa,
  anapaona hapa ni kama kituo cha polisi, na akumbuke kwamba, maombi haya ni
  kutokana na imani kubwa ambayo bado tuko nayo kwake achilia mbali kabisa
  hayo anayohusishwa nayo sababu, kama tulivyo sisi, na yeye kama binaadamu
  wote tunakosea. Na katika misingi ya heshima yunayompa akumbuke, NAPE hajawahi
  kushauliwa kuweka mambo yake sawa katika Jamii hii, wala Ridhiwan, wala Beno Malisa,
  Wala kashigila, wala Laulence Masha, sababu hao tuliishawatapika siku nyingi sana,


  Kama Mwanasiasa, na as long as Siasa is concerned, analazimika kurespond kwa busara
  kubwa sana (na ndio mategemeo yangu na wana JF wengine makini of course), Mifano
  ya hasara za kukaa kimya ni mingi, akamuulize Lowasa na hata CHAMA CHAKE pale
  kinapovutwa kwenda kwenye siasa sizizo ni tija, huwa kina respond, kwa busara nyingi
  sana (Tumshukuru Mungu).

  Mwanasiasa Kijana na Matata wa Africa ya Kusini kupitia chama cha ANC, kuna wakati
  alikengeuka na kukwaruzana na viongozi wa chama chake katika namna iliyopita kipimo
  sababu utata ni asili yake, Julias Malema, wapo waliomshahuri kukaa kimya, lakini kwa busara
  ya kipekee alijitokeza na kutuma ujumbe ufuatao kwenye mtandao, ili waafrica kusini wote
  wasome na wamjudge.

  "I, Julius Malema, apologise to the President of the ANC and the Republic, comrade Jacob Zuma and to the membership of the African National Congress and the public in general for the statements and utterances that I made on 11 April 2010 at the ANC Youth League Limpopo Provincial Congress implying that the ANC Youth League has taken a position against the President of the ANC.

  "I accept that these statements had the effect of undermining the stature of the President of the African National Congress and of the Republic. It further may have had the effect of undermining the confidence of our people in the leadership of the ANC and of creating serious divisions and breakdown of unity in the organisation.

  "I make this apology unconditionally as I accept that as a leader of the ANC and of the ANC Youth League my conduct and public utterances should at all times reflect respect and restraint. I accept one of the key principles of Congress leadership as outlined in Through the Eye of the Needle, a policy document adopted by the 51st and 52nd National Conferences of the ANC, that “an abiding quality of leadership is to learn from mistakes, to appreciate weaknesses and to correct them.”

  "I have learned from this mistake and therefore submit myself to the discipline of the ANC."

  Nategemea response yako katika misingi hiyo
   
 18. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #18
  May 30, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hii ndiyo kwa lugha rahisi inaitwa ukomavu wa kisiasa. Hongera sana ben. Nimependa sana maelezo yako.
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nadhani hii hoja haina nafasi tena, Uchaguzi umekamilika na kufana, ilikuwa lazima apatikane mmoja kuchukua nafasi hiyo sasa hatuwezi kusema baada ya Uchaguzi tena sisi hapa JF tuanze kumuhoji mmoja mmoja kama kwamba kunataka kufanya uchaguzi upya au tunaka kukata rufaa, mambo yote yaliyotoke ndio uchaguzi wenyewe na yameisha na uchaguzi Ben alishaongea tokea alipoenguliwa na maneno yake yapo hapo JF kama rekodi yake baada ya uchaguzi.

  Tukitaka kufanya kuwa kuenguliwa kwa Ben ni hoja tena hapa tutakuwa hatuutendei haki huo uchaguzi maana aliingia kwa ama kupata au kukosa! Labda kama amekutuma kuanzisha hii hoja kwa maana ya kuwa hakuridhika na matokeo! Tokea awali hata mimi binafsi niliwashangaa sana maana nyie rafikize pia mmechangia kumuangusha Ben sana, maana alianza kampeni humu Jamvini na nyie hamkumkanya bali mlimuunga mkono na kuachia mambo yaende mrama!

  Siku zote Kiongozi akikosa nafasi, kama alikuwa anagombea kwa dhati na nia nzuri basi hakukosa yeye bali wananchni ndio waliomkosa maana hawatapata nafasi ya kufaidi uwezo na utendaji kazi wake.

  Labda kama kuna mambo mengine mapya ambayo unayajua zaidi basi nakushauri yaweke wazi hapa.
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ben nchi hii ilivyoharibika tunawategemea nyie vijana muikomboe nchi yetu nzuri ili sisi wakaazi wake tuishi kwa amani na neema tele,umeongea maneno mazuri na ya ukomavu,nikutakie heri katika kuendeleza gurudumu la mabadiliko weka moyoni kwamba nyie vijana mumeshika usukani wa mustakabali wa taifa letu
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...