Ben Saanane kuhamia ACT - Wazalendo siku ya Ijumaa

Ben Saanane kuhamia ACT - Wazalendo siku ya Ijumaa

Status
Not open for further replies.
Watu walewale, jana aliitwa mbeba sumu leo shujaa nasubiri kesho sijui watamwitaje.
 
Ukombozi wa taifa hili utaletwa na MIMI na WEWE.
 
Kama ni kweli haitajiki Chadema,ana haki ya kuhamia chama kingine tena itakua ni uamuzi wa busara.
 
Laki si noti, kwani malengo ya chama cha siasa ni nini? Naona umecheka huku moyoni una huzuni. Kwani nyie mnaoposti habari za Ben kwenye chama chenu mgombea nini? Au unafki!!
 
Ndio hata Nuhu alipokuwa anatengeneza safina wengi waligoma, hawakujua nyakati, majira wala saa ya ukombozi. Ndio hv CDM ndio safina na sisi ndio wajenzi, hao wakina Zitto na wenzake ndio hao watakaoangamia. Time will tell.
 
Mbona nyie hamuendi ACT? Mnabaki kuwaomba wenzenu waende au ndio hivyo aisifiae mvua imenyea.
 
Kipaji hakiongozi mtu tuache kudanganyana, na hakuna mtu asie na kipaji duniani. Ndio maana utasikia John alikuwa anacheza mpira lkn hakuupendelea, mara Laki si pesa ni mwanasiasa mzuri ila aliishia kuposti jf. Ndio hivyo msituongopee jamani, ongeleeni ziara zenu zinazo anza kesho.
 
Ukiona manyoya jua kaliwa. Si kawaida kwa Ben Saanane kukaa kimya hivi na hasa kwa post inayomhusu,

Kama ni ya kweli,kila la kheri bro.Sisi tupo kwenye jahazi la ukombozi la CHADEMA mpaka mwisho wa dahari!!

Na haya maneno ya kuwekana kwenye ANXIETY namna hii Ben hayafai,umeshakua kiumri.
 
Last edited by a moderator:
Ben Saanane ni kijana mwerevu, ana haki zake kama Mtanzania mwingine kujiunga na chama chochote cha siasa kwa utashi wake. Naamini kama amekubaliana na mission pamoja na vission ya ACT ya uwazi, uwajibikaji, uzalendo na kutumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya taifa zima, basi si ajabu akajiunga ACT

Siasa ni safari, Dr Slaa alikuwa CCM sasa yuko CHADEMA

Lissu alikuwa NCCR sasa yuko CHADEMA
Lema alikuwa TLP sasa yupo CHADEMA
Zitto alikuwa CHADEMA, sasa yupo ACT

Kwa hiyo si ajabu kwa Ben Saanane kuhamia chama chenye dira na muelekeo cha ACT

Sawa kabisa,ni kama Lowasa atakavyoenda Act pia.Kwani kuna tatizo?
 
Hizi siasa za mitandaoni hovyo kabisa. Ben mwenyewe Mimi nimemjulia hapa hapa jf tena kwa jina tu wala sura yake siijui. Aondoke, asiondoke hana madhara kama wengine mnavyofikiri. Impact yake itakuwa humu mitandaoni hasa hapa jf. Lakini huku field hana madhara...
 
Ben Saanane ametekwa au?

Yupo sana
User Name: Ben Saanane
User Title: JF Senior Expert Member
Last Activity: Today 22:41

Nafikiri hivi alivyokaa kimya ni Vizuri sana maana ndio mda wa kukamata wanafiki wote maana hapa hata hajasema uamzi anaokwenda kuchukua kuna Makamanda wameshaanza kumkejeli kana kwamba si chochote si lolote wakati juzi kati tu hapa walikuwa wanamwagia sifa kemu kemu hapa ndo ndio wakati wa kujua rafiki wa kweli na wale wanafiki wanafiki
 
Last edited by a moderator:
Hajaondoka tu? kinachomfanya avute mda kitu gani? ukishaona mahali hapakufai ondoka haraka mambo ya kuvuta mda ni utoto na ujinga tu
 
Lowasa akienda act kura yangu kaikosa

Ben ni bora umwache zitto na maigizo yake, kama kuhama ni bora ccm kuliko act (hiki chama hakina future na hakiwezi kufikia hata robo ya malengo yake). Uta haribu maisha yako kama mwampamba na shonza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom