Nami naungana na mleta mada Greenwhich kwa pongezi kwa Ben Saanane. Hata mimi nimempongeza sana wakati nikichangia thread ya hao masalia kuhamia CCM leo hii. Kuhusu Zitto Kabwe sikubaliani na wewe kwamba atakuwa amebadilika kwa kushiriki kazi za chama hasa matembezi ya tarehe 10/2/2013!! Naweza kusema ni fix tu!!! Zitto hayuko na CDM kizalendo, yuko pale kwa maslahi ya wanaomtumia!! Kilichamfanya Zitto pengine ashiriki yale maandamano na kumshambulia spika ni kwa bile ule ulaji wake kupitia Kamati aliyokuwa anaiongoza ya kuandalia utendaji na matumizi ya mashirika ya umma POAC ilibomolewa na yule Spika wetu mpendwa!!!! Hii si dalili njema kwa Zitto na SSM yake!!! Kwa mantiki hi alikuwa analilia ulaji na si kulaani ama uendeshaji mbovu wa bunge from his heart au kushutumu kuwa Dr. Slaa alikuwa Rais halali kama Science ya Uchakachuaji isingekuwepo!!!! It doesn't click in my head!!! Ninaamini sana yale aliyoyasema Ben Saanane na sasa yanatimia!!! Kwani ile evidence ya communication ya simu na Zitto si iko wazi? Ni kwa vile CDM si chama cha kukurupuka hata Zitto alitakiwa awe kundi la kupokelewa SSM leo japo his mission failed!!! or aborted!!!
Long Live CDM!!! Hakuna kukata tamaa, wahamie SSM na vyama vingine vyote ili wabaki wazalendo wenye uchungu na hii nchi!! Maisha yamekuwa magumu na umaskini wa kukithiri kwa sababu watu wachache kupitia katika mirija ya kinyonyaji wananyonya watanzania bila huruma!!! Bora hata mbu na kupe, hata kunguni wakinyonya sana huwa wanazidiwa damu wanakufa!!!! Deeply, regreting tunakoelekea!!!
Ule umoja na uzalendo umekufa na tulichofanya ni kuliua Azimio la Arusha na kuja na Azimio la Zanzibar lililosabisha ubepari wa hali ya juu, wizi, ubadhirifu wa mali ya umma na matabaka lukuki, yakiwemo, maskini wa kutupwa leo hii hana nafasi kwa tajiri wa nchi hii, ni second citizen!!!