Spike Lee
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 625
- 272
Nadhani wewe ndiye unaishi kwa kukariri dada wewe gfsonwin. Hili liko dhahiri kwamba serikali yenu ya ccm imeshindwa kabisa kuwahudumia watanzania.
So fara sisi kama wananchi tunafanya mambo mengi sana kuisaidia serikali mambo ambayo kimsingi yalipaswa kufanywa na serikali.
Jambo la kwanza na muhimu zaidi tunalipa kodi, tena kwa taarifa zilizopo mwezi wa november na december 2012 TRA wameweza kukusanya kodi inayofikia kiasi cha shilingi trilioni moja kwa mwezi, sas utaona kuwa fedha zipo za kuweza kuhudumia wananchi katika miradi yao ya kijamii kama maji, afya na elimu kwa kutaja chache.
Wakati sis tunalipa kodi na kujitolea kuisaidia serikali nyie wa ccm na serikali yenu mnakwiba fedha zetu na kwenda kuzificha nje ya nchi, mnatengeneza miradi feki na kila aina ya hujuma katika fedha za umma. sasa tumefika mahali tunasema hatuwezi kukaa kimya ccm wanafuja fedha zetu na huduma za kijamii zinadorora, lazima tuwalazimishe kutuhudumia kwakuwa huo ni wajibu wao.
Wananchi walijitolea kujenga shule za kata na zahanati katika kata na vijiji/mitaa, serikali ilipaswa kutoa vifaa na wataalamu lakini hadi leo hii tunafikia hatua ya 60% ya wanafuzi wanafeli mtihani wa kidato cha nne kwa sababui serikali imeshindwa kabisa kutekeleza wajibu wake, imeshindwa kuandaa na kuajiri walimu, imeshindwa kuandaa na kuajiri watumishi wa sekta ya afya na imeshindwa kabisa kuimarisha na kuwekeza katika upatikanaji wa maabara, maktaba na vifaa tiba pam oja na madawa.
Sasa inapotokea mtu unakuja hapa kuitetea serikali ya hovyo kama hii ni dhahirti kwamba wewe mwenyewe unakuwa wa hovyo pia.
Vipi ule mradi wa nembo wa pikipiki Chadema?