Ben anaweza kupotea/zwa ila fikra zake hizi zitaishi

Rutaca

Member
Nov 13, 2014
94
150
Kama mnakumbuka huyu pichani ni kijana mwenye asili ya tunisia aliyejichoma moto baada ya askari kuharibu biashara yake mjini kasserine nchini tunisia.
Kijana huyu ambaye alikuwa amemaliza chuo kikuu na akakosa ajira serikalini akaamua kufanya umachinga ama biashara ndogondogo alikufa kwa kujichoma moto kitendo kilichofanya wananchi wa tumisia kuandamana na kuuangusha utawala wa rais wa wakati huo Beji Caid Essebsi

Mapema mwaka jana kwenye moja ya chombo kimoja cha habari nchini humo kilitangaza kuwa mahakama imehukumu kunyongwa kwa askari 34 ambao tume huru iliyoundwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi mauwaji na utesaji wa raia wakati wa maandamano.na kujiridhisha kuwa askari hao 34 walihusika moja kwa moja kutesa na kuuwa raia.

Mwaka 2013 askari zaidi ya 100 walihukumiwa vifungo mbalimbali nchini misri na wengine 20 walinyongwa kutokana na kukutwa na hatia ya kutesa na kuuwa raia wakati wa maandamano yaliyomuondoa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak.

Wakati aliyekuwa rais wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo akifikishwa mahakama ya kimataifa ICC kujibu mashtaka manne ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu aliyoyafanya baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2010 baada ya kushindwa uchaguzi mkuu askari 74 wamefungwa maisha katika magereza mbalimbali nchini humo kwa makosa ya kutesa na kuuwa raia wakati machafuko nchini humo.

Ni kweli kwamba hata tukiuondoa utawala wa yazid kwa njia ya kidemokeasia hatutabadilisha askari
Ni kweli kwamba waliokuwa askari wakati wa utawala wa YAZID ndio watakuwa askari wakati sisi tukiongoza,Lakini askari wote waliohusika kuuwa na kutesa raia wakati wa utawala yazid kamwe hawataachwa lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria

Hivyo kaa ukijua kuwa kama wewe ni miongoni mwa askari waliotesa na kuuwa raia wasiokuwa na hatia umerekodiwa kwenye orodha maalumu na ipo siku utafikishwa kwenye vyombo vya sheria kesi za jinai hazifutikagi na ndio maana unaona wale askari mgambo wa intarahamwe waliohusika na mauwaji ya kimbali miaka 20 iliyopita kule RWANDA wanafungwa miaka ya leo.

Najua maneno yangu ni machungu kwa baadhi watu wasiopenda ukweli lakini sina namna nyingine ya kufikisha ujumbe huu.

PLAY FOR LEMA.
MDUDE nyagali
sumu ya nyigu

 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,374
2,000
Wanakasirika basi wakiona hivi,kukutambua wanataka,TEHAMA kichwani hawana,wakienda kwa melo wanaaambiwa majina yanaelea mawinguni hata yeye hayajui!!!
 

NAKEMBETWA

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
3,523
2,000
Mbona hujaweka hizo fikra?

Hata Afrika kusini aliwahi kuuwawa kijana anaitwa Steve Biko, ila mpaka leo anaishi kwenye fikra za raia!
 

Macos

JF-Expert Member
May 12, 2008
1,936
2,000
Nimesoma mahala kwenye Facebook wanasema baadhi ya mada zake Saanane zimeondolewa kwenye FB . Hasa zile za masuala ya PHD.
Hii maana yake kuna mtu ana access na account yake
Au watekaji bado wanayo simu yake hivyo wanao uwezo wa kuingia kwenye page yake au wame mtesa mpaka ametoa password yake.
Jee hii ina faida gani katika uchunguzi wa mahali alipo ?
familia yake isaidiwe kuwasiliana Interpol kuomba FB kusaudia katika uchunguzi.
FB ni wagumu lakini ikipatikana hati ya Mahakama kuomba FB wasaidia kujua Location gani ilitumika last time ku access Account ya Ben.
FB wanao uwezo kutoa IP address ilotumika na exact location simu au laptop ilipo tumika.
Msisubiri serikali wakuchunguzieni. Chadema tafuteni private investigator kutoka nje isaidieni familia yake kupata ukweli. Familia yake ni pekee wanaweza saidiwa na FB . ..
Matamko hayasaidii ..clue muanze wapi imejileta wenyewe.
Chadema amkeni kama hamhusiki kwani ukweli mmelichukulia too lightly hili la Ben
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom