Belle9 kaja na Love Potion

Sunbae

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
254
176
Habari zenu waungwana,

Msanii bora wa RnB Tanzania ambaye nyota yake inazidi kung'aa siku hadi siku amekuja na kiba kipya kinaitwa Love Potion. Kulingana na ukurasa wake wa Instagram Belle9 ataachia kibao hicho siku ya mkesha wa Valentine Day katika ukumbi wa ky Night Life (MASAKI).

Love-Potion-Artwork.png
 
Haya ni maelezo kutoka ukurasa wa Facebook wa fans wake.

Furahia Valentine’s Day ukiwa na umpendaye kwa burudani nzuri ya muziki toka kwa mkali wa R&B Belle 9 atakaekuimbia nyimbo zake zote kali zitakazopigwa na live band huku ukipata chakula na vinywaji vilivyoandaliwa kuendana na mahadhi ya siku hii ambayo
itaongozwa na mshindi wa Big Brother Africa Idris Sultan pia ukisindikizwa na Millian, Bella & The Band.

Utapata wasaa maalum wa wewe kumchagulia au kumuimbia wimbo yule umpendaye.

Yote haya ni siku ya Jumamosi 13.02.2016 kuanzia saa mbili usiku katika ukumbi wa Sky Nightlife kwa kiingilio cha Sh 20,000 kawaida na Sh 50,000 VIP ambapo wapendanao 20 wa kwanza kuwasili watapata chupa ya champagne bure. Wahi tiketi yako sasa.
 
Huyu jamaa atleast siku hizi anapata hadhi yake..Alisahaulika kidogo

Ruttashobolwa Nakumbuka umewahi kuanzisha uzi kuhusu kuhusu huyu dogo..Dogo nyota yake imeanza kung'ara upya
 
Sikuwahi kufahamu Belle9 kama ndie aliyetoa wimbo unaimbwa "acha waongee shauri zao"… hadi pale jirani yangu alipopiga nyimbo hiyo kwa siku 3 mfululizo.
 
Huyu jamaa atleast siku hizi anapata hadhi yake..Alisahaulika kidogo

Ruttashobolwa Nakumbuka umewahi kuanzisha uzi kuhusu kuhusu huyu dogo..Dogo nyota yake imeanza kung'ara upya
Ni kweli kaka, nadhani promo zaidi kwa jamaa inahitajika, nyimbo zake ni nzuri sana.
 
Ni kweli kaka, nadhani promo zaidi kwa jamaa inahitajika, nyimbo zake ni nzuri sana.
Sure..Dogo yupo poa sana..Nadhani alijitenga na wadau ndo mana mambo yakawa yanamwendea doro..
 
Sure..Dogo yupo poa sana..Nadhani alijitenga na wadau ndo mana mambo yakawa yanamwendea doro..

Kuna nyimbo zake 3 za mwanzo huwa nikiamua kuzisikiliza hazinichoshi - Masogange, Sumu ya Penzi, Unanifaa.

Dogo yuko vizuri sana.
 
Kuna nyimbo zake 3 za mwanzo huwa nikiamua kuzisikiliza hazinichoshi - Masogange, Sumu ya Penzi, Unanifaa.

Dogo yuko vizuri sana.
Alianza vizuri sana aisee..Inasikitisha kuona Masogange ni maarufu kuliko Belle9 Teh
 
Back
Top Bottom