Beijing kuvutia tena macho ya watu duniani kutokana na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111315275197.jpg

Mwezi Agosti mwaka 2008, mji wa Beijing uliandaa michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto, ambayo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, na kupongezwa na jamii ya kimataifa. Miaka 13 baadaye, mwezi wa Agosti kwa mara nyingine tena, baada ya kufungwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, mji wa Beijing umevutia tena macho ya watu duniani, kwani maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi itakayofanyika mjini humo mwezi Februari mwakani yamepamba moto. Beijing utakuwa mji wa kwanza duniani kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto na ya Majira ya Baridi.

Hivi sasa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yameingia kwenye awamu ya mwisho. Ujenzi wa majumba na viwanja vya mashindano kwa ajili ya michezo hiyo ulikamilika mwanzoni mwa mwaka huu. Kwa mujibu wa mpango uliowekwa, mashindano kadhaa ya majaribio ya kimataifa yatafanyika, na wanariadha pia watafanya mazoezi katika majumba na viwanja hivyo kuanzia mwezi Septemba hadi Novemba. Kutokana na janga la COVID-19, Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itawasiliana kwa karibu na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki na mashirikisho mbalimbali ya michezo hiyo kuhusu hatua za kuzuia virusi, na kutathmini maandalizi kwa pande zote.

Hivi sasa, dunia bado inakabiliwa na janga la COVID-19, na virusi vipya vinavyobadilika vinaleta changamoto zaidi. Kwa kuchukua hatua madhubuti, China imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti maambukizi ya virusi, na kurejesha hali ya kawaida ya uzalishaji na maisha ya watu. Bila shaka Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi itakayofanyika mwaka ujao italeta changamoto kubwa kwa China, kwani watu wengi wataingia nchini humo kutoka nchi za nje. Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing Cai Qi, alipokagua majumba na viwanja vya mashindano ya Olimpiki mjini Beijing, alisema kukinga vizuri virusi vya Corona ni sharti muhimu la kufanikisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing. Ili michezo hiyo ifanyike kwa usalama, Kamati hiyo pia ilipeleka ujumbe wake katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo ili kujifunza uzoefu wa kukabiliana na janga la COVID-19.

Olimpiki ni familia moja kubwa. Katika mkesha wa ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach aliitaka miji ya Beijing na Tokyo ishirikiane na kusaidiana, ili kuongeza ufuatiliaji wa Michezo ya Olimpiki. Bach alieleza matumaini yake kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing “itaendelea kuwa na nguvu”, akisema Kamati yake itaendelea kushirikiana na Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, ili kusukuma mbele kazi mbalimbali za maandalizi, na kuhakikisha kuwa michezo hiyo inafanyika kwa usalama.

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itakuwa michezo ya tatu ya Olimpiki iliyofanyika au itakayofanyika kwa mfululizo katika kanda ya Asia Mashariki ndani ya miaka minne. Idara ya Habari ya Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing imesema, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Pyeongchang iliyofanyika mwaka 2018 nchini Korea Kusini, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya Tokyo iliyofanyika mwaka 2021 huko Japani, na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itakayofanyika mwaka 2022 nchini China haiwezi kutenganishwa. Anasema, michezo hiyo ni kama mbio za kupokezana, kuanzia Pyeongchang, Tokyo imeongeza kasi, na Beijing itafikia kilele. Amesema michezo hiyo itaonesha utamaduni wa Asia kwa dunia nzima, na anatumai kuwa, Beijing itaweza kufikia hitimisho la mafanikio kwa michezo hiyo ya Olimpiki.
 
Back
Top Bottom