aspen
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 501
- 166
Vifaa vya Ujenzi viko vya aina nyingi! Kuna vyakuanzia ujenzi na finishing we unataka kujua vyaaina gani?
~Tofali linaanza bei 700 mpaka 2000
~Cement mfuko 13500 mpaka 14000
~mchanga yebo 45000(evarage unaweza kupiga tofali mifuko 4),selela 90000 mifuko 10 na mende 180 vol 15.8m3 mifuko 22
~nondo mm12 sh 16000 na mm16 sh 30000
~kuchimba msingi wa sq110 ardh ya kawaida ni 60000
~kujenga tofali kozi ya chini mpaka ya 4 ni sh 200 kujenga ya 5 mpaka ya 8 sh 250 hadi 300 za juu
~kumwaga zege ni sh 10000 kwa kichwa mpaka liishe fundi atakushauli idadi ya watu ili liishe mapema si unaju zege alilali.
Mkuu la 700 linapatikana wapi si litakua ni mchanga mtupu?Mkuu mbona bei zako ndogo sana hiyo nyumba inayojengwa ni ya kiwango cha kijijini au ni kwenye miji mikubwa kama Dar?
Mkuu la 700 linapatikana wapi si litakua ni mchanga mtupu?Mkuu mbona bei zako ndogo sana hiyo nyumba inayojengwa ni ya kiwango cha kijijini au ni kwenye miji mikubwa kama Dar?
Bei ya vifaa inategemea na maeneo unayojenga,maeneo mengine mchanga/maji vinapatikana kiurahisi so bei inashuka
Experience yangu ya Chamazi/Mbande
Cement 14000-15000
Tofali 700-1000
Maji -3500-5000 @ pipa
Misumari -3500-4000 @kg
Mbao ft 10-12,000-13,000 kukodisha mbao 1500-2000 kwa siku
Nondo mm 12-16,000-17,000,mm 16 29,000-30,000
Mchanga lori tani 18-120,000-140,000
Wana JF nimeuanzisha huu uzi makusudi kujua bei ya vifaa mbalimbali ya ujenzi wa nyumba naomba tuwe tunaweka bei ya vifaa tofautitofauti kusudi wanayojenga kwa awamu wajue pa kuanzia
Mod naomba usiunganishwe na ile ya Gharama ya kujenga tanzania
Inatakiwa useme nyumba ya kawaida kwa maana gan! Ili kujua rum ngapi kuna toilete ngapi hii itafanya kujua pia zitahitajika Hand wash Basin ngapi Ukishajua hivyo ndo unapiga Hesabu Pipe ngapi utatumia pamoja na Fittings zake! Ukisema nyumba2 yakawaida watu tunatofautiana Wengine nyumba ya kawaida kwao ni Ghorofa 1 or ya chini bt Rum 12 nk! Funguka Kiongoz!
mwakani tayar mkuuNitapita tena mwakani
Au mwngine ni ya kawaid bt vyumba vyote vitatu ni self contained so lazma gharama za plumbing ziwe kubwa kuliko
Mkuu naona umevitundika hapo kwenye avatar yako, naomba tafadhali unipe mchanganuo wa vifaa na gharama ya ufundi wa plumbinh, kibanda changu kipo katika hatua za kuingiza maji ndaniMimi nadili na vifaa vya finishing hasa mabomba na maSink hivyo vyakuanzia cna ujanja navyo ngoja tuwasubiri wadau wengine!