Bei ya sukari nchini yashuka kwa Sh,1500

Bei ya sukari nchini yashuka kwa Sh,1500

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,870
Reaction score
5,755
Bei ya Sukari nchini imeanza kutengamaa baada ya kushuka kwa wastani wa sh 900 hadi 1,500 kwa kilo kutokana na viwanda kuanza uzalishaji pamoja Serikali kuingiza takribani tani 70,000 kutoka nje ya nchi kufidia upungufu uliyokuwepo.

Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti la Mwananchi jijini Dar es Salaam na mikoani unaonesha kiwa sehemu kubwa sukari inauzwa kwa wastani wa sh.2400 kutoka zaidi ya sh.3,500 iliyokuwepo miezi miwili iliyopita.

Kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kunatoa ahuweni kwa Wananchi wengi waliolazimika kutoboa mifuko yao ili kumudu bidhaa hiyo muhimu katika uandaaji wa vyakula mbalimbali pamoja na chai.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
 
Attachments

  • 20160811_081403.jpg
    20160811_081403.jpg
    177.1 KB · Views: 123
View attachment 379442
Bei ya Sukari nchini imeanza kutengamaa baada ya kushuka kwa wastani wa sh 900 hadi 1,500 kwa kilo kutokana na viwanda kuanza uzalishaji pamoja Serikali kuingiza takribani tani 70,000 kutoka nje ya nchi kufidia upungufu uliyokuwepo.
Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti la Mwananchi jijini Dar es Salaam na mikoani unaonesha kiwa sehemu kubwa sukari inauzwa kwa wastani wa sh.2400 kutoka zaidi ya sh.3,500 iliyokuwepo miezi miwili iliyopita.
Kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kunatoa ahuweni kwa Wananchi wengi waliolazimika kutoboa mifuko yao ili kumudu bidhaa hiyo muhimu katika uandaaji wa vyakula mbalimbali pamoja na chai.
Source: Gazeti la Mwananchi.

NImenunua sukari week jana kilo 3000 hiyo ya 1500 iko wapi niifuate
 
Huyo mwandishi na mhariri wake wamepewa bahasha hao!!. Huo utafiti wameufanya eneo gani au kwa familia za wafanyakazi wa viwanda hivyo!.

**vinginevyo mtoa mada utakuwa ume_take chance "kuwa wa kwanza ku_post" wkt dip wameeleza eneo la utafiti.
 
Habari njema.. na ishuke zaidi ya hapo kwa vile tunazalisha hapa hapa Tz
 
1500 per kg iyo sukari labda imetoka China na imetengenezwa kutokana na chupa za maji zilizotumika
Kwani wapi palipoandikwa kuwa sukari kilo moja ni sh 1500??

Ni vema ukasoma habari kabla kuanza kuchangia!!

Habari inasema bei ya SUKARI imeshuka kwa wastan wa sh 900 mpaka sh 1500, haisemi kuwa bei ya SUKARI ni sh 1500 laahasha!!

Kama ilikuwa ikiuzwa sh 4000 na sasa inauzwa sh 2500 na maeneo mengine ni 2400, Kuna kupungua kwa bei kwa wastan wa sh 900 mpaka 1500.
 
Walio andika hiyo taarifa wamepotosha
Bei imeshuka kwa sh 900 kutoka 3500 hadi kufikia 2400
 
Kimara kuelekea bonyokwa ni 2600tsh/kg , mbona hilo punguzo halijafika... Tusubir tuone hiyo neema...
 
Back
Top Bottom