BEI ya petrol inaweza kushuka

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
gazeti l la Rai Feb 17, 2011. ktk gazeti hilo nimejionea sababu halisi za kupaa kwa bei za mafuta nchini. Nimekua nikisikia Burundi na nchi zinazopitisha mafuta yao hapa nchini bei zao ziko chini. Tz Mambo yako hivi: Bei ya kuagiza 720/=, Sumatra,Tipper, Tbs, Demurrage 411/= Kodi ya mapato, excise duty, Ewura levy 363/=. hii ni kwa ufupi mlolongo ni mrefu sana kwa lita hiyo moja tu ya mafuta.je, ni lazima tuwe na wakusanya kodi wote hawa? je, nchi jirani nao wanafanya hivi? Mbona tunauana?
 
Inaweza sana kushuka kama tax base ikipanuliwa. Tatizo ni kwamba biashara ya mafuta ni kati ya taxable activity kubwa TZ. Sehemu kubwa ya Bil 400 wanazojitapa kukusanya kwa mwezi zinatoka huko.
 
gazeti l la Rai Feb 17, 2011. ktk gazeti hilo nimejionea sababu halisi za kupaa kwa bei za mafuta nchini. Nimekua nikisikia Burundi na nchi zinazopitisha mafuta yao hapa nchini bei zao ziko chini. Tz Mambo yako hivi: Bei ya kuagiza 720/=, Sumatra,Tipper, Tbs, Demurrage 411/= Kodi ya mapato, excise duty, Ewura levy 363/=. hii ni kwa ufupi mlolongo ni mrefu sana kwa lita hiyo moja tu ya mafuta.je, ni lazima tuwe na wakusanya kodi wote hawa? je, nchi jirani nao wanafanya hivi? Mbona tunauana?

naweza nikawa sijaelewa hapa....unamaanisha bei itapungua siku za karibuni au kutokana na ushauri wako unawataka wahusika wapunguze bei?........maana kichwa cha habari yako kimenipa mshtuko wa furaha kidogo
 
Unajua mafuta yanapopita hapa nchini kwenda nchi jirani hayalìpiwi kodi, Kwa hiyo kwao wao hawalipi kodi kubwa kama hapa kwetu
 
60 % ya bei tunayonunua mafuta huwa ni kodi za serikali!utashangaa malawi,uganda,kenya,zambia bei ya mafuta ipo chini kuliko sisi!bajeti ya serikali inategemea sigara,bia,mafuta,ushuru wa magari miaka nenda rudi!badala ya kuimarisha utalii,madini,export ya mazao
 
uctarajie bei kushuka hiyo ni kama bp ya kupanda aishuki ata kwa dawa
 
Bajeti ya upinzani Bungeni kila mwaka huwa inataja vyanzo vingi tu vya mapato lakini serikari ni dormant wao ni mafuta, sigara na bia. Nadhani huko kwingine kuna maslahi yao au la basi ni ulemavu tu wa akili za wakubwa huko serikarini.

Nani wa kuikoa Tanzania!?, watu wa mwambao maendeleo yao binafsi yanawashinda je yatakuwa ya kuongoza nchi!? Hapo nasikia kakwapua hata kale ka-akiba alikojitahidi kukajenga fisadi Mkapa.
 
Back
Top Bottom