bei ya ndoa inayodumu@@

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,099
Mpaka kifo kitakapotutenganisha! Kama upo kwenye ndoa na upo kwenye tatizo kubwa, shida au mgogoro wowote na unajisikia kama ni wewe mwenyewe tu mwenye Matatizo ya ndoa, ukweli hupo mwenyewe kwa sababu kutokuwa na Matatizo hakufanyi ndoa kuwa imara bali ndoa huwa imara kwa sababu wanandoa wanajua jinsi ya kupambana na Matatizo kwa pamoja vizuri.

Ndoa imara na zenye afya zinajua jinsi ya kupambana na hali ngumu.
Ni kawaida kila ndoa kukutana na mambo magumu katika safari ya maisha duniani.
Wakati mnaendelea na mahusiano iwe uchumba au ndoa mnaweza kukutana na tuta kubwa la ugonjwa, kuachishwa kazi, kupoteza nyumba, kifo cha mmoja katika familia yenu kama vile wazazi, biashara kuyumba kabisa au kufirisika, hapo utafanyeje?
Tumesikia mara nyingi sana watu wakiwakimbia wapenzi wao au wake zao au waume zao pale moja ya hayo linapotokea.

Ukweli ni kwamba huwezi kujua ndoa yako au uchumba wako ni imara kiasi gani hadi pale utakapojaribiwa.

Matatizo yakitokea mara nyingi huweza kuvunja mahusiano vipande vipande mume huku na mke huko au wachumba kila mmoja kuachana na mwezake.
Lakini habari njema ni kwamba, wanandoa au wachumba ambao wanaweza kupita katika ugumu wowote pamoja kwa kushikamana kama super glue huwa na mahusiano imara yaliyoyoshikamana kwa nguvu za ajabu na kuwa na upendo imara kuliko mwanzo.

Wengi hujiuliza kwa nini hili litokee kwetu tu?
Kwa nini Mungu amenitupa kiasi hiki?


Mary mwalimu wa shule ya msingi huko Njombe anasimulia kwamba mume wake amefirisika biashara yake na baadae wakapata pigo lingine nyumba yao ikaungua moto yote pamoja na mali zote.
Iliwalazima kujihifadhi kwa majirani, hata hivyo anakiri kwamba hakuna wakati wamewahi kuwa karibu na kujisikia kitu kimoja tangu waoane miaka 5 iliyopita, kwao Matatizo yamejenga ndoa yao.

Ndoa si kunywa soda kila siku ukipata kiu, si kuwa na pesa kila siku, ndoa ni kazi, kazi inayohitaji kujitoa, hata hivyo matokeo ya kushirikiana pamoja hasa wakati wa shida kwa kushikamana bila kujali ugumu unaotokea ndoa huwa imara na yenye afya ya ajabu.

Wengine likitokea tatizo kwenye ndoa au uchumba solution ni kuacha na kutafuta mwingine, huo ni ujinga, kila binadamu ana Matatizo yake mapya kabisa na ovyo kabisa.

Jaribu kufikiria kwa nini ulimkubali na kuona anakufaa?


Are you the part of the problem or part of the solution?
 

Gaga

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
4,562
1,941
huyo bibi harusi hiyo nguo kaazima? mbona imemvaa hivo, by the way nimependa hii thread, majaribu katika mahusiano ndio hujenga misingi imara. inakuweka vizuri kwa majanga yanayofata hayatakuwa yanakubabaisha kama uliweza kupita la kwanza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom